Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kwa kuogopa Kuondolewa Madaraka Haraka, Serikali ya Hasina imejisalimisha kwa matakwa ya Marekani kupitia kutangaza mtazamo wake rasmi wa Indo-Pasifiki

(Imetafsiriwa)

Habari:

Bangladesh mnamo Jumatatu ilifichua rasmi mtazamo wake wa nukta 15 za Indo-Pasifiki unaotazamia kuwepo kwa Indo-Pasifiki huru, wazi, yenye amani, salama, na jumuishi siku moja kabla ya kuanza kwa ziara ya mataifa matatu ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina nchini Japan, Marekani na Uingereza. Mgao wa pamoja wa eneo la Indo-Pasifiki katika Pato la Taifa la kimataifa, kukithiri katika biashara ya kimataifa, hatua zilizoimarishwa za hali ya hewa na mabadiliko ya teknolojia yanayoongezeka yanaweza kuwa viashiria muhimu vya kuhakikisha ustahamilivu na ustawi wa muda mrefu wa Bangladesh,' waziri wa serikali wa mambo ya nje Md Shahriar Alam alisema. Mtazamo na ushirikiano wa Bangladesh wa Indo-Pasifiki ni pamoja na 'Kuimarisha uaminifu na heshima ya pande zote, kuanzisha ushirika na ushirikiano, na kukuza mazungumzo na maelewano kwa lengo la kuhakikisha amani, ustawi, usalama na utulivu kwa wote katika Indo-Pasifiki' na 'kuimarisha taratibu zilizopo juu ya usalama na amani wa baharini katika Indo-Pasifiki' (The New Age, Aprili 24, 2023).

Maoni:

Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikiishinikiza Bangladesh kushiriki kikamilifu katika Mkakati wa Indo-Pasifiki. Kujiunga kwa Bangladesh kwenye Mkakati wa Indo-Pasifiki kumejadiliwa kwa muda mrefu katika Mazungumzo ya Ushirika kati ya Bangladesh na Marekani na pia katika mfululizo wa ziara za maafisa wa Marekani. Baada ya kufuatiliwa kwa miaka mingi, Bangladesh mnamo Jumatatu hatimaye ilitangaza 'Mtazamo wake wa Indo-Pasifiki', ikibainisha kwamba inazingatia utulivu na ustawi katika Indo-Pasifiki kuwa "sababu muhimu" katika kufikia Ruwaza ya nchi ya 2041. Washauri kipote cha watawala na wanaounga mkono Marekani na wanafikra nchini Bangladesh wanaona kutolewa kwa mtazamo kamili kuhusu Indo-Pasifiki kama diplomasia mahiri na ya wakati unaofaa kuwasilisha Bangladesh kama mdau changamfu, anayevutiwa na anayewajibika katika eneo hilo. Wanaomba watu waungane mikono na Marekani katika mradi wao wa Indo-Pasifiki ili kupata 'manufaa ya kiuchumi' ya fursa za baharini katika Ghuba ya Bengal. Kwa kusisitiza ushiriki katika mkakati wa Marekani wa Indo-Pasifiki ili kuileta Bangladesh karibu na washirika wakuu wa biashara na uwekezaji, ajenda yao mbaya ni kuficha vitisho ambavyo kongamano hili la Marekani litaleta kwa ubwana wa Umma!

Tayari ni dhahiri kwamba kwa kushiriki katika mkakati wa Marekani wa Indo-Pasifiki, Bangladesh itatumika kama kibaraka katika mzozo wa Marekani na China. Lakini serikali dhaifu ya Hasina inaipa Marekani uhuru zaidi wa kuweka uwepo imara katika Ghuba yetu ya kimkakati ya Bengal. Sheikh Hasina tayari amekubali kusaini mikataba ya ulinzi kama vile Mkataba Mkuu wa Usalama wa Taarifa za Kijeshi (GSOMIA) na Mkataba wa Upataji wa Huduma Mtambuka (ACSA) ambao umeandaliwa na Marekani kwa madhumuni maovu ya kuigeuza Bangladesh kuwa kituo cha kijeshi cha Jeshi la Marekani, pamoja na kufanya mafunzo ya kijeshi na mazoezi katika eneo la Indo-Pasifiki kwa jina la ushirikiano wa usalama. Ukweli wa mambo ni kwamba, serikali fisadi ya Hasina inahisi vitisho na hofu ya kuondolewa madarakani na Marekani. Kwa hivyo serikali ya Hasina imesalimu amri kwa mpango huu muovu wa Marekani na imekubali kujiunga na Jukwaa la Indo Pasifiki ili kuifurahisha Marekani ya kikoloni ili kusalia madarakani tena katika uchaguzi ujao. Hata hivyo, hakuzingatia vitisho ambavyo mpango huu utaleta kwa ubwana wa Ummah na hatari yake mbaya ya siasa ya kijiografia. Mbali na hilo, hajali katazo kali la Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta’ala la kuunganisha utawala wa wakoloni makafiri juu ya Ummah kutokana na kushiriki katika vikao hivyo. Yeye (swt asema,

[وَلَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]

“wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini. [Al-Mumtahanah: 2].

Watawala kama Sheikh Hasina daima watatumia ardhi yetu, rasilimali zetu za kimkakati na kijeshi kama nishati katika vita vya mabwana wao wakoloni. Kwa sababu hawana ndoto ya kuwatawala maadui wa makafiri-washirikina kupitia sera imara ya kigeni. Sera yao ya kigeni ya kupiga magoti haina lengo jengine ila kukilinda kiti chao cha ufalme kwa kukubali ubabe wa Marekani ya kibeberu na washirika wake wa Asia Kusini. Hivyo, njia pekee ya kutoka katika hali hii ya aibu na idhlali ni kurudisha mfumo wa ulimwengu wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashid kwa njia ya Utume ambayo haitaruhusu dola zozote za kibeberu kutumia ardhi, rasilimali za kistratijia na za kijeshi za Waislamu kama nishati ya vita vyao vya ubwana. Dola ya Khilafah itajiimarisha duniani kote kupitia sera madhubuti ya mambo ya nje iliyowekwa na Shari ́ah. Kwa vile Khilafah italeta Mfumo Mpya wa Ulimwengu, haitakubali shinikizo la dola yoyote kubwa, kuwa sehemu ya shirika lolote la kimataifa au miungano yao ya kijeshi. Badala yake, itatumia China, India na Marekani dhidi ya kila mmoja ili kuangamiza utawala wa Marekani na dola zengine ulimwenguni, pamoja na katika eneo hili. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [As-Saff: 9].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Sifat Newaz

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu