Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni Nani Atakayekomesha Mauaji ya Waislamu na Ubomoaji wa Misikiti Nchini Ethiopia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 2 Juni, kufuatia swala za Ijumaa, Waislamu 3 waliuawa na vikosi vya usalama vya Ethiopia nje ya Msikiti Mkuu, Msikiti wa Anwar jijini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia wakati wa maandamano ya amani ya kupinga uvunjaji wa mamlaka wa misikiti kadhaa nje ya mji na mipango kuvunja mengine zaidi. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na kuwafyatulia risasi waumini ili kuutawanya umati uliokusanyika nje ya msikiti huo. Wiki iliyotangulia, Waislamu 2 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa na vikosi vya usalama katika eneo moja wakati wa maandamano mengine, huku Waislamu 114 pia wakiripotiwa kukamatwa. Baadhi waliripoti kuwa magari ya kubebea wagonjwa hayakuweza kuwafikia waliojeruhiwa kutokana na vikosi kuuzingira msikiti huo.

Maoni:

Katika miezi ya hivi karibuni, takriban misikiti 19 imebomolewa na mamlaka nchini Ethiopia kama sehemu ya mradi wenye utata wa kupanga miji unaohusisha ujumuishaji wa manispaa kadhaa katika eneo la Oromia nje ya mji mkuu na ujenzi wa mji mpya wa Shaggar ambao serikali inadai kuwa utaboresha uchumi na kuipamba Addis Ababa kama eneo la utalii wa mijini. Uamuzi wa serikali wa kubomoa zaidi ya misikiti 30 katika Mji mpya wa Shaggar umeibua hasira kubwa miongoni mwa Waislamu nchini humo ambao wamepanga maandamano mbalimbali kupinga hatua hiyo. Baraza Kuu la Shirikisho la Masuala ya Kiislamu la Ethiopia lilituma barua kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutaka kusitishwa kwa ubomoaji huo lakini iliangukia masikio ya uziwi. Mradi huo pia unahusisha uharibifu wa nyumba na biashara, ambao unaripotiwa kuwaacha maelfu bila makaazi.

Mnamo Aprili 2022, zaidi ya Waislamu 20 waliuawa na zaidi ya 150 kujeruhiwa katika shambulizi katika makaburi ya Sheikh Elias katika mji wa Gondar kaskazini mwa Ethiopia wakati wa mazishi ya mzee mmoja Muislamu. Tukio hilo pia lilishuhudia uporaji wa mali za Waislamu. Wahalifu hao walikuwa Wakristo wenye msimamo mkali. Mnamo mwaka wa 2019, misikiti mingi ilishambuliwa katika mji wa Mota huko Amhara katika wimbi la vurugu dhidi ya Waislamu.

Ethiopia au Habasha kama ilivyokuwa ikijulikana hapo zamani wakati mmoja ilikuwa ni hifadhi kwa Waislamu waliokuwa wakitafuta ulinzi dhidi ya mateso wakati wa Mtume (saw); ihifadhi moja ya misikiti mikongwe zaidi barani Afrika - Msikiti wa Al Nejashi; ina historia tajiri ya Uislamu ambayo inaenea kwa karne nyingi; na ina idadi ya Waislamu zaidi ya milioni 25 - zaidi ya theluthi moja ya wakaazi. Lakini leo Waislamu wanauawa na maeneo ya kidini ya Kiislamu yanaharibiwa katika ardhi hii pasi na serikali, uongozi, mtawala aliye na utashi wa kisiasa kukomesha dhulma hii, ingawa Mtume (saw) amesema:

«قَتْلُ الْمُؤْمِنِ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ زَوَالِ الدُّنْيَا» “Kumuua muumini ni jambo kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kuondoka dunia nzima.” Hatutarajii chochote kutoka kwa serikali za Magharibi na UN isipokuwa maneno matupu ya kulaani. Hatutarajii chochote kutoka kwa tawala za sasa na watawala wa ulimwengu wa Kiislamu ambao wamethibitisha mara kwa mara kwamba hawana uchungaji wa kweli kwa utukufu wa damu ya Kiislamu au Uislamu.

Leo hii, haki za Waislamu nchini Ethiopia zinakanyagwa kama vile zinavyokanyagwa nchini India, Myanmar, Ufaransa na katika nchi nyenginezo duniani bila uongozi wa dhati wa Kiislamu wa kuwalinda. Hali hii haikuwa hivyo kila wakati. Wakati Waislamu nchini Uhispania, Palestina, India na kwengineko walipokuwa wakiteswa huko nyuma, Khilafah iliingilia kati kulinda damu zao na kuwakomboa kutoka kwa madhalimu wao. Ni dola hii pekee ndiyo yenye utashi wa kisiasa na uwezo wa kuwalinda Waislamu, popote wanapoishi, kutokana na madhara na mateso, kwani Mtume (saw) amesema:

«وإنَّما الإمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِن ورَائِهِ ويُتَّقَى به» “Hakika Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake.” Hata hivyo, tangu kuvunjwa kwa Khilafah mnamo 3 Machi 1924, Waislamu kote duniani wamekuwa kama mayatima, waliotelekezwa, bila ya mlezi au mlinzi.

Baada ya kusimamishwa tena Khilafah kwa njia ya Utume, dola hii itataka kuziunganisha ardhi za Waislamu, rasilimali zao, mali zao na jeshi ili kujenga nguvu kubwa ambayo itatia hofu katika nyoyo za wale wanaosubutu kuwadhuru Waislamu, au kushambulia Dini yao au maeneo ya kidini. Itakuwa na nguvu kubwa za kisiasa, kiuchumi, kimkakati na kijeshi na kujiinua na kuonyesha kwa vitendo badala ya maneno matupu dori yake kama mlezi na ngao ya Waislamu na Uislamu. Hivyo tunawalingania kaka na dada zetu nchini Ethiopia na kote duniani kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha kwa dharura Khilafah ambayo itatangaza pambazuko jipya la usalama na ulinzi kwa Ummah huu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawwaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu