Jumatano, 08 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Marekani iko katika "Mzunguko wa Kifo wa Kweli. Muda Unayoyoma!"

(Imetafsiriwa)

Habari:

Maoni yaliyochapishwa katika Wakfu wa Urithi wa kihafidhina mnamo tarehe 11 Agosti yenye kichwa "Kushindwa kulipa kwa Jina Jengine: Kwa Nini Deni la Marekani Linafaa Kupunguzwa."

Maoni:

Inafuatia kushushwa daraja kwa hivi majuzi kwa kiwango cha mikopo ya serikali ya Marekani kutoka AAA hadi AA+ na shirika la Fitch. Mwandishi wake anasema kwamba hakuna hatari inayowezekana ya kushindwa kulipa, "lakini haipaswi kupuuzwa." Deni la Marekani limevuka dolari trilioni 32, na linakua kwa kasi inayoongezeka. Lazima kuwe na kikomo kwa kiasi gani deni hilo linaweza kukua kabla ya kutoweza kuepukika. Maoni hayo yalibainisha kuwa “malipo ya riba pekee kwa deni hilo kubwa hutugharimu takriban $1 trilioni - zaidi ya bajeti yote ya Ulinzi - na matumizi yanaendelea kukua. Hicho ni kichocheo cha kufilisika na hatimaye kushindwa kulipa.”

Kushindwa kudhibiti deni kutairegesha Marekani "moja kwa moja hadi kwenye kasi ya mfumko wa bei na kushindwa kulipa kulikojificha kwenye deni la Marekani." Matokeo yatakuwa “mavuno mengi zaidi, ambayo husababisha malipo ya juu zaidi ya riba, ambayo yanamaanisha hata deni linalokua kwa kasi zaidi, na kadhalika—mzunguko wa kifo cha kweli. Muda unayoyoma kabla tufikie hatua ya kutorudi tena.”

Neno ‘kushindwa kulipa kulikojificha’ kunakusudia ukweli kwamba ingawa watu binafsi au makampuni hushindwa kulipa madeni yao waziwazi, serikali zinaweza “kuongeza deni lao kwa kupunguza thamani ya sarafu zao.” Maoni ya Heritage yanaonya kuwa Biden anafanya hivyo hasa huku dolari ikiwa imepunguzwa thamani kwa 16% kuanzia uraisi wake hadi sasa.

Hifadhi ya Shirikisho imekuwa ikijaribu kudhibiti mfumko wa bei tangu mwisho wa 2021, lakini mfumko wa bei bado ni wa juu zaidi kuliko 2% iliyolengwa. Wakati huo huo Marekani inaendelea kutumia kile isichokuwa nacho na hatimaye mtu atalazimika kulipia gharama ya hilo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu