Alhamisi, 19 Sha'aban 1445 | 2024/02/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kukata Mafungamano na Shujaa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Islamabad: Afisa mmoja wa uhamiaji wa Pakistan alithibitisha Ijumaa kuwa kila Muafghani anayetafuta hifadhi anayesubiri kuondoka kwenda nchi ya tatu atatozwa zaidi ya $800 kwa kupitisha muda wa visa zao au kutomiliki hati za kukaa kihalali. (voanews.com)

Maoni:

Pakistan imekuwa mwenyeji wa mamilioni ya wakimbizi wa Afghanistan tangu mwishoni mwa miaka ya 1970 na 1980, na sasa ghafla serikali ya Pakistan imeamuru Waafghani milioni 1.7 wasio na hati kuondoka nchini, kati ya hawa, 250,000 tayari wameondoka kupitia mpaka wa Torkham. Sababu ya kufukuzwa inasemekana kuwa kuhusika kwao katika uhalifu kama kujilipua, ingawa hakuna ushahidi wowote uliotolewa.

Urafiki wa kidanganyifu wa kisiasa kati ya Pakistan na Afghanistan ulianza katika enzi ya Zia-ul-Haq na uhusiano ulijengwa juu ya Mujahidina Waafghan kwa ujasiri kupigana na USSR na hatimaye kuwafukuza kutoka Afghanistan. Katika Vita vya Miaka Tisa (1980-1989) mzozo huo ulikuwa umegharimu maisha ya takriban raia milioni 1 na wapiganaji wapatao 125,000. Huu ulikuwa ndio wakati ambao wakimbizi wengi waliingia Pakistan na bado walishikilia jina la Mujahidina wa Wapakistani, ambao la kusikitisha sasa wamebadilika kuwa magaidi. Beji hii ya ugaidi iliwekwa wakati Taliban hawa hawa walianza kupigana dhidi ya uvamizi wa Marekani. Hapa tunahitaji kuelewa kuwa kupotea huku kwa maisha na kuhamishwa haikuwa kwa sababu ya udhaifu wa Afghanistan lakini kwa sababu ya uhadaifu na udanganyifu wa adui wa ndani. Mfano hapa unaweza kutusaidia kuelewa jinsi Waislamu wenye nguvu wanaweza kuwa pindi wanapounganishwa pamoja katika utiifu wa Mwenyezi Mungu (swt).

Katika Vita vya Afghanistan vya 1845, wanajeshi wenye nguvu wa Uingereza 160,000 waliangamizwa kikamilifu mikononi mwa Waafghani mashujaa kwenye ardhi ya Afghanistan huku mtu mmoja tu akinusurika, daktari kitaaluma. Aliruhusiwa kuishi ili tu kumwezesha kutoa hadithi ya kifo chao na uharibifu kwa mabwana zao - Ufalme wa Uingereza - ambapo alitoa. Funzo alilojifunza na Raj wa Kiingereza lilikuwa kwamba "kamwe kutojiingiza katika aina yoyote ya misheni hiyo tena".

Huu ulikuwa wakati wa upinzani wakati Ummah wa Kiislamu kote ulimwenguni alipokuwa ukijaribu kukwepa makucha ya wakoloni. Hawakugawanywa katika Dola za Kitaifa na adui wao alikuwa wa mmoja pia. Sasa hali ya kila nchi ya Kiislamu iliyokuwa chini ya utawala wa kikoloni na sasa Dola ya Kitaifa ni kama mfano wa Nabii Yusuf (as). Pindi ndugu zake walipomtupa kwenye kisima. Kuna funzo katika hili kwa Waislamu wote wanaoteseka kwa njia moja au nyengine. Funzo ni la Subra na ujasiri huku wakimtegemea Mwenyezi Mungu (swt).

[فَلَمَّا ذَهَبُوا بِهِ وَأَجْمَعُواْ أَن يَجْعَلُوهُ فِي غَيْبَتِ الْجُبْ وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ لَتُنَبِّنَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَذَا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ]

“Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao hili, na wala wao hawatambui.” [12:15].

Ummah wa Kiislamu lazima waelewe kuwa utiifu wa kweli kwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndio utakaoutoa nje ya shimo la giza ambalo umetupwa ndani yake. Badala ya kumchukia na kumsukuma mbali kaka yako Muislamu kwa sababu ya kabila lake au kumbandika majina ya kikatili kutachelewesha zaidi kusimama tena kwa Khilafah kwa njia ya Utume. Waafghani hawa hawa wanaweza kuwa nguvu kwa Ummah wa Kiislamu na kuulinda dhidi ya adui ambaye ameshughulishwa kuwapiganisha wao kwa wao kwenye kambi tofauti tofauti.

[وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ]

“Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu” [2:45]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu