Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uuzaji wa Pombe Unalindwa na Watawala wa Waislamu, Lakini Maisha ya Waislamu Hayalindwi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Abu Dhabi imefungua kiwanda chake cha kwanza cha uzalishaji Pombe nchini Imarati. Vibali vimetolewa kwa biashara hii. Imarati imeondoa ushuru wa 30% kwa bidhaa za pombe. Sheria za utoaji leseni kwa maduka ya pombe pia zimehafifishwa. Sababu ya hili, ni kupiga jeki sekta ya utalii na kuunda upanuzi wa kifedha na ujumuishaji utamaduni.

Maoni:

Huku Waislamu wakiteseka kwa kukosa chakula cha msingi na dawa, viongozi mabilionea wa Ummah wanajishughulisha na machaguo ya burudani za wasiokuwa Waislamu, huku wakipigia debe haramu kwa Waislamu katika eneo hilo.

Vitendo hivi vya usaliti lazima vifichuliwe kwa sauti kubwa na wazi wakati Ummah duniani unapopitia mashambulizi yanayoongezeka. Marekani na Uingereza zimeanzisha kampeni mpya za mashambulizi ya mabomu nchini Yemen ambayo yameweza kutatiza njia za meli za umbile la Kiyahudi. Ni matendo ya kijasiri ya Waislamu binafsi binafsi ndiyo mbayo yamechukua msimamo na sio jeshi zima chini ya Khilafah.

Hatukubali matumizi ya kiholela ya rasilimali zetu na majeshi yetu kuachwa kukaa bila ya kuchukua hatua, Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha ndugu na dada zetu kutelekezwa kwa maadui.

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ وَلِيًّا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisaa: 75].

Hadith ya Mtume (saw) imeeleza kuwa sisi ni mwili mmoja na ikiwa kiungo kimoja kitauma mwili mzima hutetemeka kwa homa. Hata hivyo, ni joto la moto wa jahannam tu ndilo litakalokutana na watawala wanaopuuza maneno ya Quran na Sunnah. Ni lazima tuinue wito wa kufanyia kazi ufumbuzi wa kweli ili Ummah huu usifanyiwe vitendo hivi vya kudhalilisha hadharani na madhalimu kuichekelea Dini ya Uislamu na kusherehekea ushindi juu ya ardhi na akili zetu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Imrana Mohammad

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu