Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Marufuku ya Uingereza ya Hizb ut Tahrir Imepitwa na Wakati

(Imetafsiriwa)

Habari:

Serikali ya Uingereza ilisema kwenye tovuti yake rasmi www.gov.uk, “Hizb ut-Tahrir imepigwa marufuku leo (19 Januari), na kufanya kuwa ni kosa la jinai kuwa mshiriki wa kundi hilo, au kukaribisha uungaji mkono kwake.” [Chimbuko]

Maoni:

Mama wa Uovu, Uingereza, haikuweza kuzuia chuki zake dhidi ya Uislamu na Waislamu, na vilevile dhidi ya ulinganizi wa kusimamisha Khilafah na wito wa kuongeza uungaji mkono kwa waliodhulumiwa. Hiyo, Uingereza ikaipiga marufuku Hizb ut Tahrir, baada ya hatua hii kubakia ikisubiriwa kwa zaidi ya miaka thelathini, tangu kuwasili kwa Shab wa kwanza wa Hizb ut Tahrir nchini Uingereza. Uingereza isingewezaje? Uingereza haikuacha juhudi yoyote, kwa karne nyingi, kupanga njama dhidi ya Khilafah, hadi ilipoweza kuivunja Khilafah, ndani ya siku hizi za Rajab, mwaka wa 1342 H.

Hizb ut Tahrir imepigwa marufuku katika makoloni na hifadhi zote za zamani za Uingereza duniani, kuanzia Jordan, ambapo John Bagot Glubb ("Glubb Pasha"), mtawala halisi wa Jordan, aliipiga marufuku yapata miaka sabiini iliyopita. Hii ilikuwa mara tu Glubb alipopata habari za kuanzishwa kwa Hizb mikononi mwa Sheikh Taqi al-Din al-Nabhani, Mwenyezi Mungu amrehemu. Hizb bado imepigwa marufuku leo chini ya utawala wa mtoto wa mwanamke wa Kiingereza, Abdullah Mwana, na kuendelea hadi Imarati, inayotawaliwa na wana wa Zayed, wafuasi wa Kiingereza, na pia upande wa magharibi kwa nchi za Maghreb ya Kiarabu, na Malaysia hadi Mashariki ya Mbali. Hii ni kutokana na ufahamu wa Uingereza juu ya mradi wa kusimamisha Khilafah ambayo Hizb inaitaka. Popote walipokoloni au kukaa, Waingereza hawawezi kuvumilia hata kusikia kutajwa tu kwa Khilafah. Hawawezi kustahamili kusikia kutajwa kwa dola ya Haki, yenye kuwatawala watu kwa uadilifu. Waingereza ni kama watu wa Lut waliosema, kama Mwenyezi Mungu alivyotaja katika Qur'an Tukufu,

[أَخْرِجُوا آلَ لُوطٍ مِنْ قَرْيَتِكُمْ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ]

“Wafukuzeni wafwasi wa Lut'i katika mji wenu. Hao ni watu wanao jitia usafi!” [An-Naml 27:56].

Haishangazi kwamba Uingereza imeipiga marufuku Hizb ut Tahrir. Badala yake, inashangaza kwamba marufuku hiyo iliakhirishwa, hadi leo. Hata hivyo, ikiwa sababu inajulikana, haishangazi. Kupuuza kwa Uingereza amali za Hizb kwenye kisiwa chake hakukumaanisha, hata kidogo, kwamba iliridhika na uwepo wake. Badala yake, ilifikiri kwamba fikra ya Hizb ilifungika kwa Mashababu na wafuasi wake. Hakukuwa na haja kwa Uingereza kuipa Hizb imani zaidi ya Ummah juu yake, kukusanyika kuizunguka na kubeba fikra zake, kwa kuipiga marufuku. Hata hivyo, ilipodhihirika kwake, hivi majuzi, kwamba Hizb ilikuwa inauwakilisha vyema Umma wa Kiislamu na matakwa yake, kama kiongozi wa kweli wa Ummah, ikiwemo jamii ya Kiislamu nchini Uingereza, Uingereza ilihamaki kwa hasira. Ikamezwa na chuki yake. Kwa hiyo, Uingereza iliyala masanamu yake yenyewe, yaliyowakilishwa na maadili ya uongo ya kile kinachoitwa uhuru na maagizo ya sheria.

Kilichoifanya Uingereza kuipiga marufuku Hizb ni misimamo ya Hizb juu ya vita vya Gaza, na mwito wake wa kuwanusuru Waislamu wa huko, na Uislamu kuwa badali ya hadhara kwa ulimwengu mzima, na kuibuka Hizb kuwa kiongozi mtukufu anayetetea wanyonge na kutoa wito wa afueni kwa walio na dhiki. Hii ni hasa kwa vile wito wa kutokomezwa umbile la Kiyahudi kutoka kwa uwepo wake kwa hakika ni wito wa kuiondoa Uingereza yenyewe katika uwepo. Vita kati ya Ummah na umbile la Kiyahudi kwa hakika ni vita vya msalaba vya Wapiganaji wa Msalaba Magharibi dhidi ya Ummah. Umbile la Kiyahudi si chochote ila mstari wa mbele wa Magharibi katika kupigana na Umma wa Kiislamu. Ni jambia lenye sumu lililotumbukizwa ubavuni mwa Ummah, ambalo linauzuia kutokana na mwamko na kusimamisha Khilafah Rashida ilioahidiwa. Iwapo umbile la Mayahudi litaondolewa, suala la Umma kuandamana hadi kisiwa cha Uingereza, kama wakombozi, litakuwa ni suala la muda tu.

Uingereza ni kinara wa ukafiri duniani na chanzo cha fitna zake. Inafahamu kikamilifu tishio la ulinganizi wa Hizb ut Tahrir kwa hadhara yake, ambayo inakaribia kuporomoka. Hatushangai kwamba nchi nyingine za Magharibi na wafuasi wao walifuata mkondo huo katika kuipiga marufuku Hizb. Mzozo kati ya Hizb na Magharibi umefikia awamu yake ya mwisho ya maamuzi. Hii ni baada ya Ummah kuifahamu Dini yake na kuiacha Magharibi na hadhara yake. Ni baada ya watu wengi wa ulimwengu wa Magharibi kufahamu undani wa mzozo wa kihadhara unaoendelea ulimwenguni, na ubatili wa hadhara ya Magharibi, mbinu zake chafu za kikoloni, na uhalifu wake unaoendelea, ambao haufichiki tena kwa mtu yeyote. Usaliti, vibaraka shirikishi, na ufisadi wa tawala katika nchi za Kiislamu pia haufichiki tena. Unafiki wa waliozihalalisha tawala hizi, zikiwemo harakati, maulamaa, wanahabari na wengineo pia ulifichuliwa... Kwa hiyo, hisia chafu za Uingereza kuhusu ukweli huu ziliifanya wakati huu ifanye kazi yake chafu yenyewe, badala ya kuikabidhi kwa watumishi wake Waarabu na wasio Waarabu. Ilitunga mashtaka na kusuka uongo ili kuhalalisha ukiukaji wake wa maadili yake ambayo tayari yalikuwa ni ya batili, ili kulinda umbile la Kiyahudi, na ushawishi wa Uingereza duniani.

Sababu zilizotolewa na Ufalme wa Charles III, unaowakilishwa na Sunak, ambaye aliunganisha ndani ya moyo wake chuki ya Makruseda na Mabaniani dhidi ya Uislamu, ni sababu ambazo ni sifa kwa Hizb, na sio kwake. Kutoa wito kwa majeshi ya Kiislamu kutaharaki kwa ajili ya Jihad ili kuikomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na kuitakasa kutokana na majisi ya Mayahudi wahalifu, ni heshima kwa Hizb, na kwa kila mtu mwingine anayefanya kazi na kulingania na kutoa wito kwa hilo. Wito wa Jihad kwa ujumla ni wito wa kupigana na nguvu za uovu na kuwakomboa wanadamu kutokana nazo, ili kutawala kwa uadilifu wa Uislamu, Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Ni kitendo kitukufu ambacho kinaweza tu kufanywa na watu watukufu, Manabii (as), Mitume (as) na wale wanaowafuata (as). Jihad si sawa na mapigano ya wakoloni, mithili ya Waingereza, ambao uhalifu wao unashuhudiwa na kila pembe ya dunia, yakiwemo mauaji, utumwa na uporaji wa mali...kuanzia Bara Hindi dogo, hadi bara la Afrika.

Mgogoro kati ya Uislamu, unaowakilishwa na ulinganizi wa kusimamisha dola ya Kiislamu duniani chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir, na ukafiri, unaowakilishwa na dola kubwa za ulimwengu, ikiwemo Uingereza iliyozeeka, umekuwa wazi, na kutamkwa sana. Ummah unawangoja watu wenye nguvu ndani yake, wakiwakilishwa na majeshi, ili kuvipindua viti vya vibaraka wa Waingereza na washirika wao wa Marekani. Unangojea majeshi kutoa nusra yao ya kimada kwa Hizb ut Tahrir, ili kupiga pigo la mwisho kwa nguvu za uovu za kilimwengu, kwa kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni juu ya hili kwamba wito kwa watu wenye ikhlasi katika Ummah huu lazima uelekezwe. Ni kwa ajili hii kwamba majeshi ya Ummah lazima yaitwe kutaharaki mara moja. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[انْفِرُواْ خِفَافاً وَثِقَالاً وَجَاهِدُواْ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللهِ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.” [Surah At-Tawba 9:41].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu