Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Programu za Chanjo kwa Watoto Zinaendelea huko Gaza wakati Vyakula, Dawa na Mafuta vyote Vimezuiwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Gazeti la ‘The Telegraph’ linaripoti kuwa Unicef ilipeleka chanjo nusu milioni Gaza ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya utotoni. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaonya juu ya hatari ya maambukizi miongoni mwa wakimbizi wa ndani milioni 1.9 wa Gaza.

Maoni:

Kwa kuzingatia kwamba Umoja wa Mataifa umeshindwa kabisa katika sera zake zote za kulinda haki za binadamu; Wanawake, Watoto, Wakimbizi, Wasio na hatia katika vita, Wanyama na Ikolojia.

Mtu lazima azingatie kwamba hatua ya ghafla ambayo programu ya chanjo inasukumwa bila kizuizi chochote si chochote ila ni khiyana nyingine ya kuharakisha vifo vya watoto. Hakuna wasiwasi kwa afya na usalama wakati silaha za kemikali na mabomu yenye uharibifu mkubwa yametanda katika miji yote, na kuifanya kuwa vumbi.

Mauaji ya halaiki huko Gaza ndio shambulizi pana lililonakiliwa kwa kina zaidi katika historia ya ulimwengu. Hatuna uhaba wa ushahidi wa uhalifu uliofanywa, na hakuna njia ya kukataa viungo vya mwili vya watoto ambavyo zimetapakaa katika mitaa yote ya Gaza. Na bado kipaumbele cha kuudhi cha Mataifa yanayotoa wito wa “amani” na “haki” ni kutuma “chanjo”. La hasha, hili linaweza kuwa ni jaribio jengine lao la kibiolojia ambalo litatumika kama ushahidi wa silaha mpya za kuua Ummah huu wa Muhammad (saw).

Hatudanganyiki na jaribio hili la uongo kwa wanadamu. Tunajua ni Khilafah pekee ndiyo yenye ukweli kwa wajibu wake wa kulinda haki za binadamu na haina ajenda ya ulafi na malengo ya kifedha.

Tunatoa wito kwa Ummah kuwawajibisha viongozi wa Waislamu kwa kuruhusu uhalifu zaidi dhidi ya damu ya Ummah kwa kutozuia matumizi ya chanjo hizo bandia, na tunakataa masuluhisho yao yasiyo halali kwa njia ya mazungumzo na kujifanya na mipango ya upatanishi dhidi ya maadui wa Uislamu. Tunaongozwa na maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu (swt) anapotuonya juu ya mipango ya uwongo ya amani ya watu waovu wa dunia hii pale (swt) anaposema;

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـكِن لاَّ يَشْعُرُونَ]

“Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.” [Al-Baqara: 11-12].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Imrana Mohammad

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu