Jumatatu, 18 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mauaji ya Kinyama ya Rafah

Je, kuna ubinadamu wowote uliosalia duniani, achilia mbali katika Majeshi ya Waislamu?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Doha - Mei 27, 2024: Dola ya Qatar inalaani vikali shambulizi la bomu la 'Israel' ambalo lililenga kambi inayohifadhi watu waliokimbia makaazi yao huko Rafah katika Ukanda wa Gaza na kuacha makumi ya mashahidi na majeruhi; ikilizingatiwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa ambao utaongeza maradufu mzozo wa kibinadamu unaozidi kuwa mbaya katika Ukanda huo uliozingirwa.

Wizara ya Mambo ya Nje inasisitiza haja ya mamlaka za ‘Israel’ kushikamana na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki wa kutaka kusitishwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Rafah; na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za dharura kuzuia dhamira ya mauaji ya halaiki, kutoa ulinzi kamili kwa raia, na kuzuia vikosi vya uvamizi kutekeleza mipango yao inayolenga kuwaondoa kwa nguvu raia kutoka mji huo ambao umekuwa kimbilio la mwisho la mamia ya maelfu ya watu waliokimbia makaazi yao katika Ukanda wa Gaza.

Wizara hiyo inaeleza wasiwasi wa Dola ya Qatar kwamba shambulizi hilo la mabomu litafanya juhudi za upatanishi zinazoendelea kuwa ngumu, na kuzuia kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji vita wa mara moja na wa kudumu katika Ukanda wa Gaza na kubadilishana wafungwa kwa wafungwa; hivyo kuzidisha madhara ya vita hivi na athari zake kwa usalama wa kikanda na kimataifa. (State of Qatar Foreign Affairs)

Maoni:

Mauaji ya Rafah yalitokea bila kuadhibiwa kisheria.

Picha nje ya kambi ni za kuogofya. Mauaji ya kinyama ya eneo la kibinadamu lililotengwa kwa ajili ya waliokimbia makaazi yao lililipuliwa na kuteketezwa kwa moto. Picha za watoto wasio na vichwa na miili iliyoungua ikilipuliwa vipande vipande huku mhalifu huyo wa Kiyahudi akishambulia kwa mabomu makao hayo. Uzito wa maangamizi makubwa haupimiki!

Wakati huo huo, tunayo Jordan ambayo inasisitiza ‘kulaani kwake bila shaka vitendo hivi’, kama ilivyotangazwa na msemaji wa ubalozi Sufian Qudah ambaye alivitaja kama ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na sheria za kimataifa za kibinadamu, vinavyokiuka maadili yote ya kibinadamu na kiakhlaqi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema katika hotuba yake kwenye televisheni. "Shambulizi la Jumapili dhidi ya Rafah, ambalo lilikuja baada ya amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, limefichua hali ya usaliti na umwagaji damu ya dola ya kigaidi."

Je, asili hii ya usaliti na umwagaji damu haikufichuliwa kwa ulimwengu wote!? Ni kauli ya kufedhehesha iliyoje ambayo inakejeli Ummah wote wa Kiislamu. Kiwango cha utelekezwaji mbele ya macho ya ulimwengu mzima na muhimu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu pia ni Al-Qahhar Al-Muntaqim na mayowe ya Rafah na Gaza hayatakosa kusikilizwa Naye (swt).

[إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ]

“Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.” [Al-Buruj:12] Kinachohitajika si maneno bali ni amri kwa jeshi zima kuhama ili kuangamiza kabisa umbile la Kiyahudi na kuwaokoa watu wanaoungua na ardhi ya Palestina.

"Tunawasilisha uhalifu huu mpya kwa mahakama za kimataifa ili kutilia nguvu ushahidi wa kuubana uhalifu huu wa kivita na kuwafungulia mashtaka," Katibu Mkuu wa Umoja wa Kiarabu Ahmad Abul-Gheit alisema. Je, unahitajika ushahidi zaidi kwa mahakama za kikafiri tu kukabiliana na kutokuchukuliwa hatua kutokana na utawala wa wafadhili?! Hakika, ni tabia yao ya kishenzi na chuki yao kwa Waislamu.

Ukatili unaofanywa kwa makusudi mbele ya nchi jirani za Kiislamu na kile ambacho watu wa Rafah wanapata kama malipo ni "shutma kali"!!! Hivi ndivyo mhalifu Netanyahu na genge lake walivyotangaza tangu mwanzo, ilhali bado majeshi ya Waislamu yamebakia kupooza. Je, hii itawasaidia nini isipokuwa kutoa idhini kwa umbile hilo katili kuua watu wasio na hatia zaidi na kuangamiza Ukanda wote wa Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa sababu watakachopata ni kauli nyingine ya maneno matupu! Tawala za Waarabu zinatosha kutumia X kutuma mitandaoni wakijifanya kana kwamba hawana majeshi. Watu wa kawaida huingia kwenye mitandao ya kijamii kulaani na kupinga sio serikali zinazodai kuunga mkono Palestina!

[لِيَجْزِىَ ٱللَّهُ كُلَّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ]

“Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi kwa yale iliyo yachuma. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” [Ibrahim:51]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Manal Bader

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu