Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kizazi Dhaifu na Mafunzo ya Gaza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Takriban Kizazi (Gen Z) milioni 10 nchini Indonesia hawana ajira au wanajulikana kama NEET (wasio katika ajira, elimu na mafunzo). Ukweli huu unatokana na data ya BPS (2021-2022) ambapo kulikuwa na watu 9,896,019 mnamo Agosti 2023, ambayo ni karibu 21% ya idadi ya watu waliozaliwa kati ya 1997 na 2012. Indonesia haiko peke yake, katika sehemu mbalimbali za dunia pia inaonyesha hali ya NEET kwa vijana ni hali inayoongezeka. Tukiangalia takwimu kwa kila eneo, idadi ya vijana wa NEET duniani kote kuanzia 2005 hadi 2023, ya juu zaidi ni ulimwengu wa Kiarabu (33.28%), ikifuatiwa na Afrika (26.11%) kisha Asia Pasifiki (21.68%) (Takwimu za Idara ya Utafiti).

Maoni:

Hii ni gharama nzito ambayo kizazi cha vijana wa Kiislamu lazima kilipie kutokana na maendeleo yasiyo endelevu yanayotokana na utekelezaji wa uchumi huria wa kibepari. Mfumo huu umeunda kizazi dhaifu - haswa katikati ya maendeleo ya kiteknolojia na kimaada. Tabia hii ya NEET inashangaza sana miongoni mwa maumbile ya utumiaji na ukwepaji ambao pia ni sifa katika kizazi (Gen Z), wasiokuwa ajira lakini pia ni watumizi sana na wanaishi ndani ya puto la mawazo. Kizazi chenye uraibu wa michezo, utazamaji wa kupita kiasi, kuwaomba wazazi pesa, kula, kulala na kujiketia kama maiti zilizo hai wasio na lengo la maisha.

Mamilioni ya matineja na vijana nchini Indonesia wamelengwa kuwa watumiaji wa tasnia ya burudani na mtindo wa maisha kutoka kwa majukwaa mbalimbali ya teknolojia ya kimataifa. Utafiti mwingi umefanywa kuangalia tabia ya kizazi hiki. Kwa mfano, matumizi yao ya michezo ya kubahatisha katika nchi sita za ASEAN yalifichua kuwa kulikuwa na wachezaji milioni 288.5 kutoka kizazi (Gen Z) mnamo 2023, na kukadiria kuwa kutakuwa na milioni 344 katika 2027 (Niko Partners, 2023). Mfano mwingine unaohusiana na tabia ya kizazi (Gen Z) makazini ni matokeo kutoka kwa Randstad Workmonitor mnamo 2022 ambayo yalifichua kuwa asilimia 41 ya wahojiwa wa kizazi (Gen Z) walienea kote Ulaya, Asia Pacifiki na Marekani wangependelea kubaki bila ya ajira kuliko kunaswa katika kazi ambayo haiwafanyi kuwa na furaha. Hawataki kutoa muhanga furaha yao na afya ya akili kwa ajili ya kazi.

Kando na uchunguzi mwingi juu ya tabia ya kizazi (Gen Z), hatuwezi kukataa kwamba kuna kurudi nyuma kwa ubora wa maisha ambayo kizazi (Gen Z) inakabiliana nako katika masuala ya kiuchumi, kijamii, mazingira na hali ya kisiasa ya kimataifa. Wanaishi ndani ya mfumo wa kilimwengu ambao unaendelea kupata majanga mengi. Haya ndiyo haswa Qur’an inayoyaonya kuhusu maʻīshatan ḍhanka, yaani maisha ya dhiki, mateso, vifua vyao ni finyo kwa sababu ya upotofu wao.

[وَمَنْ اَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِيْ فَاِنَّ لَهٗ مَعِيْشَةً ضَنْكًا]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki…” [QS. Tāhā [20]: 124]

Hali hii ndiyo sababu kubwa inayofanya hali ya Ghaza siku hizi ipate nafasi katika nyoyo za vijana, katika ulimwengu wa Kiislamu pamoja na Magharibi ambao umejikita katika usekula. Hili linaweza kuonekana kutokana na ushiriki wao katika harakati za kimataifa zinazounga mkono Palestina katika nchi mbalimbali. Sababu ya ujasiri na ari ya maisha ya watu wa Gaza – imekuwa ni kivutio cha ajabu kwa kizazi kizima cha vijana duniani ambao leo wanaishi katika magonjwa ya akili, uduni na utupu kutokana na mfumo wa kisekula wa kiteknolojia wa kibepari.

Kipekee, teknolojia pia ndiyo muwezeshaji kwa kizazi (Gen Z) kuchukua taarifa kuhusu maendeleo ya Palestina kwa haraka sana. Wanazidi kuvutiwa na hadithi ya kibinadamu ya Gaza, ushujaa wa kiakili wa Waislamu huko, kuna lulu zinazong'aa za watoto wa Gaza ambazo wanataka kujua kuwahusu, mafundisho ya Aqida ya Kiislamu ambayo hutoa uhai kwa moyo wa nafsi zilizo tupu. Lulu za Aqida ambazo Waislamu wanapaswa kuendelea kuzidumisha na kutoa mwangwi kama nishati ya mabadiliko ya kimataifa; mabadiliko makubwa katika mfumo wa kilimwengu kutoka giza hadi nuru, kutoka ujinga wa kisasa hadi utukufu wa Uislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Surat An-Nisa'a aya ya 9,

[وَلْيَخْشَ الَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَافًا خَافُوا عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا اللَّهَ وَلْيَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا]

“Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeli acha nyuma yao watoto wanyonge wangeli wakhofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme maneno yaliyo sawa.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu