Jumamosi, 14 Muharram 1446 | 2024/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mkuu wa Majeshi Azuru Ujerumani huku Inasambaza Silaha kwa Umbile la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 24 Mei 2024, kitengo cha habari cha jeshi la Pakistan kilisema kuwa, “Mkuu wa Majeshi yuko katika ziara rasmi katika Jamhuri ya Shirikisho ya Ujerumani... Uongozi wa Ujerumani ulitambua dori ya Jeshi la Pakistan katika mapambano dhidi ya Ugaidi.” [1]

Maoni:

Ziara ya mkuu huyo wa jeshi nchini Ujerumani ilionyeshwa kwenye vyombo vya habari kana kwamba ilikuwa mafanikio. Je, kuna nini hasa cha kupendeza kuhusu ziara hii?

Ni Ujerumani ambayo inasambaza kikamilifu silaha ambazo umbile la Kiyahudi hutumia kuwaua shahidi wanawake na watoto wa Gaza. Mnamo tarehe 11 Machi 2024, Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm ilisema, “Marekani ilichangia asilimia 69 na Ujerumani kwa asilimia 30 ya uagizaji silaha wa ‘Israel.’” [2]

Hata hivyo, baada ya Ujerumani kuunga mkono kikamilifu ugaidi wa kutisha unaofanywa na umbile la Kiyahudi, mkuu wa jeshi la Pakistan alikutana na maafisa wa Ujerumani ili kujadili kupigana na ugaidi!

Ujerumani ndiyo imelilinda jeshi la Kizayuni tangu mwanzo wa vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Gaza. Hata hivyo, mkuu wa jeshi la Pakistan alikutana na Dkt. Tobias Linder, Waziri wa Mambo ya Nje katika Afisi ya Shirikisho la Mambo ya Nje, ambaye alituma ujumbe kwenye Twitter mnamo 10 Novemba 2023, “Ujerumani inasimama kidete upande wa ‘Israel’ na kusisitiza haki ya ‘Israel’ ya kujilinda yenyewe na watu wake.” [3]

Ni Ujerumani ambayo inapigia debe kwa uchangamfu suluhisho la dola mbili la Marekani, ambalo linasalimisha zaidi ya 80% ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa umbile la Kiyahudi. Hata hivyo, mkuu huyo wa jeshi la Pakistan alikutana na Inspekta Jenerali wa Ulinzi wa Shirikisho wa Ujerumani, Jenerali Carsten Breuer, ambaye anahusika na “Miongozo ya Sera ya Ulinzi ya 2023” ya Ujerumani, ambayo inasema, “haki ya Israel kuwepo ni muhimu sana. Usalama wa Israel ni maslahi ya kitaifa ya Ujerumani.” [4]

Kwa hivyo, huku silaha za Ujerumani zikiirarua miili ya watoto wa Gaza, mkuu wa jeshi anatabasamu kwenye kamera, na kupeana mikono na mikono iliyolowa damu ya uongozi wa Ujerumani. Kwa hivyo tunawezaje kufurahia ziara hii kama mafanikio? Tunawezaje?!

Huu ndio uhalisia wa kufedhehesha wa makamanda wa kijeshi wa majeshi ya Waislamu leo. Wanadumisha ushirikiano na wale wanaopigana na Waislamu moja kwa moja, au kuwasaidia wengine kufanya hivyo. Hakika, dola ya Kiyahudi inategemea kamba kutoka kwa watu, ambazo zinapanuliwa karibu kabisa na Marekani na Ujerumani pekee. Bila ya kamba hizi, askari waoga wa Kiyahudi hawakuweza kusimama mbele ya wapiganaji walio na silaha duni ndani ya Palestina, achilia mbali jeshi moja la Waislamu. Makamanda hawa wa kijeshi wanashirikiana na makafiri, licha ya kuwa Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahina 60:9].

Makamanda hawa wa kijeshi ni wepesi wa kuitikia wito wa dola za Magharibi wa kuwapiga vita Waislamu kwa jina la kupigana na ugaidi, lakini wanapuuza amri ya Mwenyezi Mungu (swt) ya kuwafukuza maadui zetu popote pale walipotufukuza. Hakika Mwenyezi Mungu (swt) ameifanya kuwa ni faradhi ya Shariah kukomesha unyakuzi wa ardhi za Waislamu wa makafirini. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]  “Na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:191]. Amri hii ya Mwenyezi Mungu (swt) inahusiana na ardhi yoyote ya Waislamu, huku ardhi ya Palestina ikiwa ni ardhi ya Al-Masjid Al-Aqsa, Kibla cha Kwanza, Haram iliyotakaswa, mahali pa Isra'a na Miraj ya Mtume (saw), ambavyo viunga vyake Mwenyezi Mungu (swt) amevibariki mpaka Siku ya Kiyama!

Khiyana ya uongozi wa kijeshi wa Waislamu umevuka mipaka yote. Wameichafua sifa ya majeshi ya Waislamu mpaka ikawa nyeusi ya kaniki, huku maafisa wa kijeshi wakiinamisha vichwa vyao chini kwa aibu. Wameleta fedheha juu ya Ummah ambao una mamilioni ya askari wanaostahiki haki ya kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili ya kifo cha kishahidi na ushindi. Wamehakikisha kwamba watu waoga zaidi kuliko watu wote, Mayahudi, wako huru kuwapiga mabomu, kuwapiga risasi na kuwabaka Waislamu katika ardhi ya Mitume (as) kwa zaidi ya miezi saba. Hakika sasa inatosha. Ni juu ya Umma wa Kiislamu na majeshi yake kuwang'oa wasaliti na kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni Khilafah Rashida ndiyo itakayokusanya majeshi kwa ajili ya ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa. Kwa hivyo, enyi maafisa wa jeshi la Pakistan, njooni na mshirikiane na Hizb ut Tahrir kubadilisha udhalilifu kuwa ushindi, na mateso kuwa sherehe.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Maregeleo
[1] https://www.ispr.gov.pk/press-release-detail?id=6862

[2] https://www.sipri.org/media/press-release/2024/european-arms-imports-nearly-double-us-and-french-exports-rise-and-russian-exports-fall-sharply

[3] https://x.com/tobiaslindner/status/1722733486694441339

[4]https://www.bmvg.de/resource/blob/5701724/eacb54dfc428b6808c9088402de91836/verteidigungspolitische-richtlinien-2023-data.pdf

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu