Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Khilafah Itakomesha Maangamizi ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 3 Oktoba 2024, ‘Pakistan Today’ iliripoti, “Nathan Porter, mkurugenzi wa ujumbe wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa wa Pakistan, alionya kwamba kifurushi cha hivi karibuni cha uokoaji cha dolari bilioni 7 kinaweza kuwa fursa ya mwisho ya nchi hii ikiwa mageuzi yaliyopendekezwa yatatekelezwa kwa nia ya kweli.” [Chanzo]

Maoni:

Pakistan ndio tu imeingia kwenye programu yake ya 25 na mpango wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, kufuatia kukamilika kwa masharti magumu chini ya Mpangilio wa Miezi tisa wa Kudumu kwa Muda (SBA). Waziri Mkuu ameelezea kuridhika kwake, kana kwamba hii ilikuwa sababu ya sherehe [Chanzo]. Hata hivyo, ili kuelewa athari za mpango wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ni muhimu kutambua migogoro iliyokita mizizi iliyosababishwa na uliberali mamboleo, au kwa usahihi zaidi ukoloni mamboleo, masharti ndani ya mipango ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa.

Athari za uharibifu za programu zinazofuatana za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa zinaonyeshwa katika takwimu za kiuchumi. Pato halisi la Taifa la Pakistan limepungua kutoka $316.5 bilioni mwaka 2018, hadi $298.2 bilioni mwaka 2023, ikionyesha kupungua kwa sekta ya ndani. Huku mfumko wa bei ukiwa wastani wa 11.5% kila mwaka, idadi kubwa ya watu wenye kipato cha chini wanakabiliana na mapigo mazito zaidi ya mgogoro huu wa kiuchumi wa muda mrefu. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, wastani wa akiba ya fedha za kigeni za Pakistan imemudu miezi mitatu na nusu tu ya uagizaji bidhaa kutoka nje, huku deni la nje limepanda hadi 42% ya Pato la Taifa. Kwa viwango vya riba vikiwa katika 17.5%, gharama za kukopa kwa biashara na viwanda ni kubwa. Kutokana na mtego wa madeni, karibu 75% ya mapato ya kodi ya Pakistan hutumika kwa malipo ya riba, hivyo basi kubakisha pesa chache kwa ajili ya elimu, afya na maendeleo. [Chanzo]

Kando na tarakimu, hali halisi ya kijamii na kiuchumi nchini Pakistan ni mbaya mno. Kuna pengo kubwa kati ya matajiri na raia wanaohangaika. Gharama ya mahitaji ya kimsingi imepanda sana. Familia hujitahidi kukidhi hata mahitaji yao ya kimsingi. Kupanda mara kwa mara kwa bili za matumizi na gharama za usafirishaji huongeza mzigo. Biashara zinakabiliwa na matatizo, mahitaji ya wateja yanapungua, huku gharama za uendeshaji zikipanda, zikichochewa zaidi na ushuru mkubwa. Watu wanakimbia nchi.

Mipango ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ndiyo chanzo cha uharibifu wa uchumi duniani kote. Mgogoro nchini Pakistan ni sheria, na sio chengine. Masharti ya mpango wowote wa IMF huwanufaisha wakopeshaji wa kimataifa juu ya vipaumbele vya ndani. Mipango inaelekeza rasilimali kutoka kwa malengo muhimu ya maendeleo hadi kujenga akiba ya fedha za kigeni. Hii inaingiza nchi katika mzunguko wa ukopaji na uregeshaji, na kuongeza utegemezi kutoka nje. Hatua za kushughulikia taasisi za fedha ambazo hazina mitaji midogo zimeundwa ili kulinda maslahi ya wakopeshaji. Ili kudhibiti utozaji wa deni na upungufu wa fedha, serikali inakopa mara kwa mara kutoka kwa benki za biashara, na hivyo kutengeneza mzunguko mbaya wa deni.

Kisha kuna orodha ndefu ya masharti kuhusiana na uchumi. Mfuko wa Fedha wa Kimataifa unasisitiza juu ya ubinafsishaji wa mashirika ya serikali, ikiwa ni pamoja na mashirika katika sekta muhimu kama vile kilimo, nguo, viwanda na elimu. Ubinafsishaji hudhoofisha uwezo wa serikali wa kusimamia viwanda na kukidhi mahitaji ya jamii. Hivyo serikali inakuwa tegemezi zaidi kwa mikopo. Masharti kuhusu biashara na masoko yanapendelea mashirika makubwa ya kimataifa, na kufanya kuwa vigumu kwa makampuni ya ndani kushindana. Uchumi unategemea sana uagizaji kutoka kwa dola kubwa, haswa katika sekta kama nishati, nguo, magari, vifaa vya elektroniki na dawa. Kuondolewa kwa ruzuku kunahamisha mzigo zaidi kwa umma. Kuhusu sera za kustahamili tabianchi, zinapendelea teknolojia za kigeni, na kuongeza utegemezi wa nje.

Kwa kuzama katika mikopo inayotegemea riba, huku uchumi ukiwekwa rehani ipasavyo, serikali inaweza basi kupunguza viwango vya riba, katika jaribio la kuchochea uwekezaji na ukuaji. Mara nyingi, hii inasababisha boom ya muda mfupi, ikifuatiwa na kupasuka kwa kuponda. Kisha, serikali inarudi kwa wakopeshaji kwa mikopo zaidi.

Mipango ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni mzigo kwa wanadamu wengi. Ni hukmu za Kiislamu pekee zitakazotekelezwa na Khilafah Rashida ijayo ndizo pekee zinazoweza kuuokoa ulimwengu kutokana na ukandamizaji wa kiuchumi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ]

“Na lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.” [Surah Al-Ma'idah (5:66)].

Khilafah itakomesha unyonyaji wa wakoloni kupitia hukmu mbalimbali za Shariah, ndani ya Pakistan na kwengineko katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Kwanza, kuchukuliwa kwa dhahabu na fedha kama msingi wa sarafu kutakomesha uchapishaji usio na mwisho wa fedha za fiat (zisizo na thamani ya dhati), na kuvunja utawala wa dolari, kuleta utulivu wa biashara ya kimataifa na kupunguza nakisi ya biashara.

Pili, Khilafah itakataa malipo yote ya riba ya nje na ndani, na kuukomboa uchumi kutoka kwa mizigo dhalimu ya madeni.

Tatu, Khilafah italeta mali za umma kama nishati na madini chini ya usimamizi wa dola, kupunguza gharama kwa umma na kuzalisha mapato kwa hazina ya dola, ili kupunguza kutegemea kodi na mikopo.

Nne, Khilafah itaondoa kodi za kidhalimu, na kutekeleza ushuru wa Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Kharaj, Jizya, na Zakat, ili kuhakikisha ukusanyaji wa mapato, bila ya kuwalemea masikini na wenye deni.

Tano, miundo ya kampuni ya Uislamu na hukmu za Shariah zinazofungamanisha umiliki wa ardhi na kilimo chake hurahisisha ushiriki katika uzalishaji wa kilimo na viwanda.

Hakuna kuepukana na masaibu ya kiuchumi isipokuwa kwa kusimamishwa Khilafah kwa Njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Affan – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu