Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sio kila chenye Kumetameta ni Dhahabu
(Imetafsiriwa)

Habari:

- Watawala wa nchi za Waislamu wanakimbizana kumpongeza Trump.

- Kundi la vijana wa Kiislamu na wafuasi wao wakabiliana na mashabiki wa kandanda wa Kiyahudi jijini Amsterdam.

Maoni:

Tawala dhalilifu za vibaraka zimesisitiza kuthibitisha, kwa yakini, kwamba ni tawala ambazo si za Ummah, huku Ummah ukiwa si sehemu yake. Katika kupambana waziwazi na hisia za Waislamu, zilikimbilia kumpongeza Rais Trump wa Marekani baada ya kutangazwa ushindi wake katika uchaguzi huo. Zilikimbilia kumpa majukumu yao ya utiifu na uaminifu, na kusahau kuuawa kwa watoto wa Waislamu huko Gaza, Lebanon na kwengineko katika vita vya wazi vinavyoongozwa na Amerika, kwa kutumia mali zake, huku wakisahau kauli za bwege huyu katika kuunga mkono kwake wazi kusiko na mipaka kwa Mayahudi. Je, inawezekana kutarajia kwamba zabibu zitatoka kwenye miiba?!

Kwa upande mwingine, kundi la vijana wa Kiislamu, na wale waliokuwa na mshikamano pamoja nao, walikabiliana na majambazi wachache wa Kiyahudi, waliokuja kuunga mkono klabu yao inayocheza Amsterdam. Hii ilikuwa ni baada ya kufanya uchokozi na kuimba miito dhidi ya ndugu zao nchini Palestina. Ni katika tukio ambalo linathibitisha umoja wa hisia za Waislamu na matarajio yao ya kukombolewa kutoka kwa tawala duni za Ruwaibadha. Inathibitisha kwamba kinachowazuia Waislamu kuwanusuru ndugu zao, ni watawala waovu, ambao wamedhibiti shingo zao, kwa uungaji mkono wa wazi kutoka kwa Magharibi yenye chuki, inayokufuru Uislamu na watu wake.

Kuna mandhari mbili za kipekee.

Mandhari ya kwanza inaakisi utovu wa adabu na ufidhuli wa watawala duni Ruwaibadha wa Waislamu. Inaakisi kupuuza kwao hisia za Waislamu, ikiwa ni pamoja na hasira na maumivu yao kwa yale wanayoyaona ya jinai za Marekani na Mayahudi, katika vita vyao vya kikatili dhidi ya Palestina na kwengineko. Inaakisi uungaji mkono wa khiyana wa watawala kwa maadui na kujitenga kwao na Umma wa Kiislamu.

Ama mandhari ya pili, inaakisi umoja wa hisia za Waislamu na umoja wa Imani yao. Inaakisi kwamba Waislamu hawaamini mipaka ya kindoto inayowatenganisha, kwani wao ni Ummah mmoja Mashariki na Magharibi mwa ardhi. Waislamu wameunganishwa kwa msingi wa kwamba hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba hapana apasaye kuabudiwa wala kutiiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt). Uchungu wao ni mmoja na furaha yao ni moja. Wako tayari kutoa muhanga maisha na pesa zao ili kuwanusuru ndugu zao.

Enyi Umma wa Kiislamu, enyi Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu, zingatieni bishara njema ya afueni na ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Fuatizeni mulichofanya kwa hatua ambayo italeta malipo makubwa zaidi, inshaAllah. Lengeni usemi wenu na wito wetu kwa wana wenu katika majeshi. Watakeni wakate mafungamano yao na tawala duni na za uhaini. Walinganieni watoto wenu wajifunge na Mwenyezi Mungu (swt), na wasonge kwa Baraka za Mwenyezi Mungu (swt) ili kuikomboa Palestina, na ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu.

Enyi Umma wa Kiislamu, jueni kwamba watawala wenu wamefungamana na maadui zenu. Badala ya kuyaelekeza majeshi yenu kuelekea Palestina ili kuwaokoa ndugu na dada zetu wasichinjwe na kuuawa, wameyatiisha majeshi yenu kwa amri ya adui yenu. Huku Mayahudi, wakiwa na silaha za Amerika na Ulaya wanachinja ndugu zetu, watoto na wanawake, watawala wa duni wanawafanya askari na maafisa wetu wawepo kulinda Mayahudi na maslahi ya Magharibi. Basi Mayahudi wataogopa nini ilhali majeshi ya Waislamu yapo chini ya amri ya wasaliti hawa wadhalilifu?

Enyi majeshi ya Waislamu: Vipi mnawaua ndugu zenu, na mnashirikiana na wauaji wao? Je, vipi munawanyamazia kimya wale wanaokupeni mahitaji ili kuwahudumia maadui wa Dini yenu na Ummah wenu? Leo, muna machaguo mawili. Ima muchague kunyamaza, kutotenda, kuridhika, uharibifu unaofuata, udhalilifu katika dunia hii, aibu na majuto Siku ya Kiyama. Au muchague kutenda kwa kukamata mikono ya hawa mafisadi haramu na kuwazuia, kwa kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume. Kisha mukachague kuwang'oa Mayahudi na umbile lao kutoka Palestina, muishinde Magharibi kafiri na vibaraka wake, na kueneza uadilifu na utulivu katika sehemu zote za dunia, jambo ambalo si gumu kwa Mwenyezi Mungu (swt),

[وَلَيَنْصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Surah Al-Hajj 40].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdul Ilah Muhammad – Wilayah Jordan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu