Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ziara ya Biden ya Dakika za Mwisho Afrika: Kuimarisha Ajenda ya Ukoloni na Unyonyaji wa Marekani

(Imetafsiriwa)

Habari:

Jumatano ya tarehe 04/12/2024 Rais wa Marekani Joe Biden alihitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Angola. Katika siku ya mwisho ya ziara yake, Biden alitembelea mradi wa Ukanda wa Lobito, mradi wa reli inayojengwa kwa ufadhili wa Marekani yenye kilomita 1,300 inayoanzia Zambia kwenye utajirim kubwa wa madini ya shaba hadi bandari ya Lobito kusini magharibi mwa taifa la Angola. Pia, Biden alifanya mkutano na maraisi wa Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Zambia na Makamu wa Rais wa Tanzania (VOA Africa 05/12/2024).

Maoni:

Ziara ya Biden nchini Angola inalenga kuimarisha ajenda ya ukoloni pamoja na unyonyaji wa rasilimali za Angola na nchi jirani nyuma ya pazia la mpango unaoitwa Uwekezaji wa Kigeni (FDI).

Mnamo Juni 2022, Marekani ilitangaza lengo la kukusanya dolari bilioni 200 kupitia PGII (Ushirikiano wa Miundombinu na Uwekezaji wa Kimataifa) kuimarisha miundombinu, nishati, kimwili, kidijitali, afya na miundombinu inayohimili hali ya hewa, kwa lengo la kuimarishwa uwekezaji katika maeneo muhimu ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na Ukanda wa Lobito.

Pia, wakati wa kikao cha Jukwaa la Kimataifa la Ukuaji wa Uchumi (Global Gateway) mwezi Oktoba 2023, Muungano wa Ulaya (EU) na Marekani zilitia saini - pamoja na Angola, DRC, Zambia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Fedha la Afrika (AFC) - Mkataba wa Makubaliano (MoU) unaohusiana na uendelezaji wa Ukanda wa Lobito na Reli ya Zambia -Lobito.

Hakika huu si mradi kwa ajili ya maslahi na maendeleo kwa watu wa Angola na Afrika, bali ni unyonyaji wa kimagharibi na ajenda ya ukoloni.

Reli hii ya Lobito ni njia ya kimkakati itayounganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yenye utajiri wa rasilimali nyingi na Angola kupitia Zambia, hadi bandari ya Lobito kwenye Bahari ya Atlantiki likiwa lango kuu la kupeleka rasilimali kwa mataifa ya kikoloni.

Ukanda huo (wa Lobito) ambao kwa kiasi kikubwa uko chini ya Marekani utaruhusu usafirishaji wa haraka wa madini ya kobalti na shaba, miongoni mwa madini mengine, yanayochimbwa kutoka mji wenye utajiri wa madini ya kimkakati wa Kolwezi wa DRC hadi mataifa ya magharibi. Kwa hiyo, mradi huu ni kwa ajili ya kuwezesha maslahi ya kibepari ya kikoloni.

Inaonekana pia sababu nyingine nyuma ya ziara ya mwisho ya Biden kwa Afrika nchini Angola kuwa ni jaribio la kudhibiti ushawishi wa China nchini Angola, Afrika ya Kati na Afrika kwa ujumla.

Kulingana na Jarida Jornal de Angola, kutoka mwaka 2018 hadi Machi 2022, China ilikuwa miongoni mwa wawekezaji watatu wakubwa nchini Angola. Umoja wa Falme za Kiarabu uliongoza uwekezaji wa kigeni (FDI) kwa dolari milioni 351.7, ikifuatiwa na Uingereza kwa dolari milioni 283.1, ilhali China iliwekeza dolari milioni 225.

Mnamo Septemba 2024, Shirika la Uhandisi la serikali ya China (China State Engineering Corporation) lilitia saini makubaliano ya kuendesha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), njia nyingine ndogo ya reli katika ukanda huo wa Lobito ambayo inanufaisha sana wawekezaji wa China na kiungo cha Zambia ya kati na bandari ya Dar-es- Salaam nchini Tanzania.

Kwa hivyo, kwa Marekani kukabiliana na athari na ushawishi wa kiuchumi wa China katika eneo hili inalazimika kufadhili mradi wa Ukanda wa Lobito, na raisi Biden alilazimika kufanya safari katika wiki zake za mwisho kabla ya kuondoka ikulu ya Marekani (Whitehouse)

Marekani haitasitisha miamala yake ya kishenzi ya kibepari nchini Angola, ambapo kuanzia miaka ya sabiini, alikuwa akiwaunga mkono waasi wa UNITA ambao walisababisha mauaji, ukatili na uharibifu mkubwa wa Angola hadi miaka ya 2000 pale maslahi ya Marekani yalipopatikana.

Dola ya Kiislamu ya Khilafah ndiyo pekee yenye uwezo na nguvu ya kukomesha unyonyaji wa kibepari wa kikoloni kwa wanadamu. Kuregeshwa kwa dola hiyo kutakuwa ni ukombozi wa kihistoria wa ulimwengu wa Kiislamu na mataifa mengine dhaifu yanayoendelea kama vile Angola nk.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu