Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kizungumkuti cha Syria: Kati ya Ukosefu wa Utambuzi na Tumaini la Kweli

(Imetafsiriwa)

Habari:

Baada ya miaka 14 ya vita na ukandamizaji, Syria inaonekana iko tayari kwa mabadiliko huku utawala wa Bashar al-Assad ukianguka na vikosi vya upinzani, vinavyoongozwa na Abu Mohammad al-Julani, vikichukua Damascus. Hata hivyo, matumaini ya mustakabali mzuri zaidi yanavurugwa na ushawishi mkubwa wa dola za nje kama vile Marekani na Uturuki, ambao zinaongoza njia ya Syria chini ya mifumo ya kisekula, inayoungwa mkono na Magharibi kama vile Azimio 2254 la Umoja wa Mataifa. Hili linazua maswali muhimu sana kuhusu iwapo tumaini la kweli linaweza kuwepo bila kukataa utawala wa kigeni na kuzipa kipaumbele kanuni za Kiislamu.

Maoni:

Matukio haya yanatulazimisha kutafakari juu ya maumbile ya tumaini la kweli na dori ya mkanganyiko wa kifikra katika hali mbaya ya sasa ya Syria.

Ukosefu wa utambuzi unaregelea mvutano wa ndani unaotokea wakati unapokabiliwa na imani au vitendo kinzani. Kwa upande wa Syria, hili linadhihirika kwa wale wanaotarajia mustakabali mwema pamoja na Uislamu wakati huo huo wakikiri kuendelea kwa dola ya kisekula na ya kidemokrasia, na kwamba dola za Magharibi kama vile Marekani na Azimio 2254 la Umoja wa Mataifa zinasalia katika udhibiti. Azimio hili linasisitiza kwamba Syria lazima ibaki kuwa dola ya kisekula, ambayo kimsingi inahakikisha kwamba wahusika wa kikoloni ambao wameidhibiti nchi hiyo kwa miaka mingi wanahifadhi ushawishi wao. Maneno ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken wakati wa mkutano wa hivi majuzi nchini Jordan yanathibitisha hili. Blinken alisisitiza umuhimu wa kile kinachoitwa mustakabali wa umoja na kidemokrasia kwa Syria, akisisitiza utawala wa Marekani na washirika wake. Juu ya hayo, utawala wa kihalifu wa Bashar al-Assad unaonekana kuondoka kupitia mlango wa mbele, na kurudi kwa mlango wa nyuma kwa sura nyingine.

Zaidi ya hayo, mkanganyiko huu wa kifikra husababisha wengi kukumbatia mradi wa Julani bila kutoa ukosoaji wa kweli. Wanahusisha uungaji mkono huu, miongoni mwa mengine, na matumaini, licha ya kulegeza msimamo wazi wa kuchagua mtindo wa kisekula juu ya utawala wa Kiislamu na utegemezi kwa dola za nje. Hili linaendeleza dhana potofu kwamba mustakabali mwema unaweza kupatikana bila kwanza kuweka kanuni za Kiislamu katikati.

Katika Uislamu, matumaini ni muhimu, yanayounganishwa kwa kina na itikadi (aqeeda) ya Kiislamu, lakini pia yanafungwa na masharti. Matumaini ya kweli yanahitaji hatua na kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) huku yakitimiza juhudi zote za kusimamisha kanuni za Kiislamu. Kukuza matumaini bila kufikia masharti haya—kama vile kukubali serikali ya kisekula na ya kidemokrasia chini ya utawala wa Magharibi—ni udanganyifu. Haipelekei kwenye ushindi bali inapelekea kwenye muendelezo wa kujisalimisha kwa miundo ile ile ya kikoloni.

Hali ya sasa nchini Syria inadhihirisha kwamba matumaini ya kweli si tu hamu ya mabadiliko bali pia nia ya kuoanisha mabadiliko haya na maadili ya Kiislamu. Hii ina maana kwamba Waislamu nchini Syria lazima wasizisujudie dola za Magharibi bali wajitahidi kwa ajili ya mujtamaa unaotawaliwa na Uislamu.

Watu wa Syria tayari wamejitolea sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua inayofuata. Hili linahitaji juhudi za pamoja kukataa utawala wa dola za nje na kutodai chochote isipokuwa suluhisho la Uislamu.

Katika ulimwengu ambapo Marekani na dola zengine zenye nguvu duniani zinaendelea kuamuru mustakabali wa nchi kama Syria, ni muhimu kutambua kwamba tumaini la kweli haliko katika kukubali masharti yao. Tumaini la kweli lipo katika kumwamini Mwenyezi Mungu (swt) na kutenda kwa mujibu wa mwongozo Wake. Hapo ndipo Syria inaweza kupata ushindi wa kweli na mustakabali unaoheshimu mihanga ya watu wake.

Matukio nchini Syria yanatumika kama mfano mchungu lakini wenye kufundisha jinsi ukosefu wa utambuzi na fikra ya matumaini unaweza kupotosha taifa. Ni muhimu kuyachukua mafunzo haya na kuelewa kwamba tumaini la kweli si matamanio ya kufikirika tu bali ni juhudi madhubuti zinazofungamana na kanuni za Kiislamu. Mwenendo wa sasa wa kukumbatia bila ukosoaji mradi wa Julani unaangazia hatari za matumaini ambazo hazijakita mizizi katika masharti ya Kiislamu. Watu wa Syria sasa wana fursa ya kugeuza matumaini haya kuwa uhalisia kwa kuchagua njia isiyo sujudia dola za nje bali iliyojitolea kikamilifu kwa Uislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu