- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Unyonyaji Mbaya wa Bima ya Afya na Takaful
(Imetafsiriwa)
Habari:
Tangazo la hivi majuzi la Chama cha Bima ya Uhai ya Malaysia (LIAM), Shirika la Takaful la Malaysia (MTA), na Jumuiya ya Bima Jumla ya Malaysia (PIAM) la kuongeza bima ya afya na malipo ya takaful kwa kiwango kikubwa mno cha 40% hadi 70% ni jambo la kushangaza. Dhihirisho la ulafi wa kirasilimali. Ingawa mashirika haya yanahusisha kupanda kwa gharama za matibabu na kuongezeka kwa mahitaji ya huduma ya afya, nia halisi ni dhahiri: kuongeza faida kwa gharama ya umma.
Maoni:
Hatua hii, huku kukiwa na hali ya kuongezeka kwa gharama za maisha, inafichua umbile poraji la mfumo wa kirasilimali, ambao unastawi kwa kunyonya mahitaji ya binadamu. Kinachojulikana kama uhalali wa ongezeko hili - kupanda kwa gharama za madawa, teknolojia iliyoendelea ya matibabu, na mishahara ya juu katika sekta ya afya - inaangazia tu jinsi upataji faida wa urasilimali umejikita kwa kina ndani ya huduma muhimu. Watoaji bima, wakitiwa moyo na sera zisizo wazi za udhibiti za Benki ya Negara ya Malaysia, huongeza malipo kwa upande mmoja, bila kujali sauti na mihangaiko ya watu. Ushirikiano wao na hospitali za kibinafsi kuongeza gharama kupitia njia kama vile Barua za Dhamana (GLs) unaonyesha zaidi ufisadi wa kimfumo uliokita ndani ya urasilimali. Licha ya kuvuna faida kubwa—ongezeko la RM8.4 bilioni mwaka wa 2024 pekee—mashirika haya yanadai hata zaidi kutoka kwa umma, yakitumia vibaya bila aibu mfumo mbovu.
Uislamu kwa upande mwingine unatoa ruwaza inayokinzana kabisa kwa ajili ya huduma ya afya – yenye mizizi ya huruma, usawa, na uwajibikaji. Huduma ya afya haionekani kama fursa kwa wale wanaoweza kumudu lakini kama haki ya kimsingi kwa kila mtu, bila kujali mali, dini, au hadhi ya kijamii. Katika mfumo wa utawala wa Kiislamu (Dola ya Khilafah), serikali inachukua jukumu kamili la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa raia wote. Rasilimali kutoka kwa utajiri wa umma (Baitul Mal) zinasimamiwa kwa usawa ili kufadhili huduma za afya kwa wote, na matajiri hutozwa ushuru inapohitajika tu kusaidia mahitaji ya jamii.
Hii sio nadharia bali ni kielelezo kilichothibitishwa cha utawala. Historia inashuhudia mafanikio yasiyo na kifani ya mifumo ya afya ya Kiislamu chini ya Khilafah. Umar ibn al-Khattab (ra), kwa mfano, binafsi alihakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ya matibabu waliyohitaji, huku Hospitali ya Qalawun katika karne ya 13 Cairo ilionyesha ubora wa Kiislamu katika huduma ya afya. Ikitoa matibabu bila malipo kwa wote, ilipokea maelfu ya wagonjwa kila siku, bila kujali rangi au dini. Wagonjwa walitunzwa hadi kupona kabisa, wakisaidiwa kwa chakula, nguo, na usaidizi wa kifedha wakati wa matibabu yao. Hii inasimama kinyume kabisa na vitendo vya kinyonyaji na vya kifisadi vya mifumo ya afya ya kiraslimali ya leo.
Mfumo wa kirasilimali, pamoja na kulenga faida bila kuchoka, hauna uwezo wa kutoa huduma ya afya ya kina, yenye usawa. Umeyafanya mateso ya wanadamu kuwa bidhaa, ukiwaacha maskini kujitunza wenyewe huku ukitajirisha mashirika na kipote chao cha washirika. Ufisadi huu wa kimfumo, unaochochewa na ulafi na kutokuwa na ubinadamu, ndio chanzo kikuu cha mgogoro wa kiafya unaotukabili leo.
Uislamu, kama mfumo kamili wa maisha, hutoa suluhisho pekee linalowezekana. Kwa kuweka ustawi wa watu mbele na kusimamia rasilimali kwa uadilifu na haki, mfumo wa Kiislamu unatokomeza unyonyaji unaoendelezwa na urasilimali. Khilafah inahakikisha kwamba huduma ya afya si mzigo tena bali ni haki iliyohakikishwa, inayoiondoa jamii kutoka katika masaibu yaliyoletwa na ukandamizaji wa kibepari. Ni wakati wa kukabiliana na kufeli kwa urasilimali na kutaka kuregeshwa kwa mfumo wa Kiislamu—mfumo uliothibitishwa kutoa haki, utu, na kujali kwa wote. Ni chini ya Khilafah pekee ndipo tunaweza kujenga jamii ambayo huduma ya afya inahudumia ubinadamu, sio faida.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia