Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Amerika ya Trump Itashindwa Kufanya Kile ambacho Kikongwe Biden Hakuweza Kukifanya
(Imetafsiriwa)

Habari:

“Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametoa kauli kadhaa zenye utata ambazo zinaakisi waziwazi ukubwa wa tofauti katika sera za ndani na nje za Marekani na za Rais anayeondoka wa chama cha Democrat Joe Biden. Kwa upande wa sera ya mambo ya nje, Trump alisema atakomesha kile alichokitaja kuwa machafuko katika Mashariki ya Kati, kusitisha vita nchini Ukraine, na kuzuia kuzuka kwa Vita vya Tatu vya Dunia, bila kueleza jinsi atakavyofanya haya yote...

Tangu 7 Oktoba, “Israel” imekuwa ikiendesha vita vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza, kwa msaada kamili wa Marekani, ambapo zaidi ya Wapalestina 153,000, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, wameuawa na kujeruhiwa, na zaidi ya 11,000 wamepotea, huku kukiwa na uharibifu mkubwa na njaa ambayo imeua watoto na wazee. Mapema mwezi huu, Trump alitishia kwamba ikiwa wafungwa katika Ukanda wa Gaza hawataachiliwa kabla ya kuapishwa kwake Januari 20, kutakuwa na “jahanamu ya kulipia gharama” katika Mashariki ya Kati, na akasema kwamba “wale wanaohusika watashambuliwa vikali zaidi kuliko mtu yeyote kuwahi kushambuliwa katika historia ndefu iliyohadithiwa ya Marekani..."

… Kwa upande wa sera ya ndani, Trump alisema atafanya mabadiliko makubwa jijini Washington, na Republican walio wengi katika bunge la Congress wanaunga mkono uteuzi wake kwa maafisa. Mwezi uliopita, Trump alitangaza wateule wake wa nafasi 20 za juu katika serikali yake, akichagua kundi la maafisa wa kawaida na wasio wa kawaida kwa nyadhifa za juu chini ya wiki 3 tangu uchaguzi wa rais. Machaguo ya Trump yalileta pamoja watu kadhaa wenye usuli wa kifikra unaokinzana, lakini wameungana katika kuunga mkono muundo wa vuguvugu lake maarufu “Make America Great Again,” linalojulikana kwa kifupi “MAGA.”” (Al Jazeera Arabic)

Maoni:

Nembo ya Chama cha Republican ni ndovu, na ndovu ana hadithi nzuri katika historia ya Waislamu. Ndovu walikuwa kikosi chenye nguvu cha mashambulizi ambacho Wafursi walitumia katika vita vyao. Ndovu walibakia katika nafasi hiyo hadi Wafursi walipokabiliana na Waislamu katika Vita vya Al-Qadisiyyah. Waislamu walikizima kikosi hicho kwa kuikata mikunga, na kuwang'oa macho ndovu hao. Haya ndiyo yatakayomtokea ndovu wa Marekani hivi karibuni, mikononi mwa Dola ya Khilafah itakayoanzishwa hivi karibuni, kwa Idhini ya Allah (swt). Ndovu ana hadithi nyingine iliyofikishwa kwetu na Quran Tukufu, wakati Abraha al-Ashram alipoleta ndovu kuibomoa Al-Kaaba. Hata hivyo, hatma yake haikuwa ila ni kwamba Mwenyezi Mungu (swt) aliwateremshia mvua ya mawe kutoka Motoni, hivyo wakabaki ni athari tu baada ya mpepeso wa jicho. Ikiwa Trump ni Abraah al-Ashram au Rostam Farrokhzad, Mwenyezi Mungu (swt) anajua, huku waumini wakisubiri kuona.

Trump huyu anayeahidi kusitisha machafuko, ndiye aliyesababisha machafuko hayo. Nchi yake ndiyo iliyowasha moto wa machafuko. Marekani ndiyo iliyowasaidia Mayahudi kwa aina zote za silaha. Marekani ndiyo iliyopandikiza madhalimu katika nchi nyingi za Waislamu kama vile Bashar al-Far (Panya) na Ibn Salman. Marekani bado inawaunga mkono madhalimu kama Al-Sisi, Erdogan na wengineo. Tusisahau kauli yake na maelezo yake kuhusu Al-Sisi kama “dikteta ninayempenda.” Kwa hivyo, mtu yeyote asifikirie kuwa Trump ni mtu wa amani ambaye atafanikisha amani katika Mashariki ya Kati. Badala yake, Trump anasema kwamba atamaliza machafuko hayo kwa mauaji na ukatili zaidi, kwa mujibu wa sera ya sasa ya Marekani ambayo msingi wake ni mauaji na ukatili dhidi ya watu wa ulimwengu wa Kiislamu, ambao wanaasi dhidi ya madhalimu wao. Hii ni kama alivyoahidi kuifanya “jahanaam” Mashariki ya Kati ikiwa wafungwa wa Kiyahudi huko Gaza hawataachiliwa huru. Kwa hivyo ni kipi kipya katika sera ya Trump, ambayo ni tofauti na sera ya sasa ya Biden?!

Kuhusu faili la Ukraine, Trump atafanya kama kiongozi wa genge anayemtelekeza mmoja wa watu wake Zelenskyy na nchi yake, na kuikabidhi kwa Urusi kwa badali ya faida, ambayo baadhi yake aliipata nchini Syria, na kwa makubaliano mengine ambayo bado atayafanya pamoja na Putin, kiongozi wa mafia wa Urusi.

Ama kuhusu hadithi ya Vita vya Tatu vya Dunia na kuvizuia visitokee, ni kukazanisha misuli tu, na kwa ajili ya matumizi ya ndani na ya vyombo vya habari. Je, ni pande hizo za vita vya dunia ni zipi, ikiwa Marekani sio mchochezi ndani yake?! Iwapo kuna vita vijavyo, Marekani ndiyo itakayoviwakisha, na kama msemo unavyokwenda, سلم العالم من أمريكا وهو بخير “Dunia ambayo ni salama kutokana na Marekani ni kheri yote.”

Chini ya tawala zake mtawalia za Republican na Democratic, Amerika haijaacha juhudi zozote katika kuweka ubabe na sera zake kwa nchi za dunia. Daima hutumia vibaraka na washirika wake ulimwenguni kufikia malengo haya, wakati imeshindwa kufikia mafanikio yoyote kwa nguvu zake yenyewe. Kwa hivyo, Trump hatakuwa na uwezo zaidi wa kufikia mafanikio zaidi katika Mashariki ya Kati na karibu nayo, mbali na njama na kufeli kwa vibaraka wa Amerika duniani. Laiti isingekuwa vibaraka hawa, uoga wao na mbwembwe zao, Trump asingeweza kunyanyua fimbo nene kutishia dunia. Aidha, vibaraka hawa hawaoni kwamba wao wenyewe ni fimbo hiyo. Marekani inawatumia kama silaha chafu kuwasha moto katika nchi za ulimwengu wa Kiislamu. Lau kama vibaraka hawa wangekuwa na busara, wangeweza kupindua utawala wa Amerika kwa kuasi tu utashi wa kichoyo wa Amerika.

Kwa upande wa ndani, Trump hana fimbo ya kichawi ya kushughulikia matatizo ya kiuchumi, kijamii na kiafya yanayoikumba nchi. Mfumo wa kirasilimali umeifikisha nchi katika hali duni, inayoashiria ukiritimba wa mali mikononi mwa kipote kidogo, chini ya asilimia moja. Urasilimali umeifanya Amerika kutokuwa tofauti na dola zilizofeli kote duniani, ambapo watawala wafisadi na kipote teule wanahodhi utajiri wa nchi, huku watu wengine wakiishi katika umaskini wa kutisha. Hiki ndicho kinachotokea sasa nchini Marekani, ambapo wamiliki wa mashirika makubwa wamehodhi utajiri wa Amerika, ambao wengi wake ni utajiri wa ulimwengu, wakati watu wengine wanaishi kwa makombo ambayo mabepari wanawarushia. Hali hii haisababishwi na ufisadi wa mabepari pekee. Badala yake inasababishwa na mfumo wenyewe wa kibepari. Ubepari unatokana na nadharia za kiuchumi kama vile ukiritimba, kujilimbikizia mali, riba na ubashiri. Kwa hivyo, je, mtu mwenye akili timamu angefikiri kwamba Trump anafikiria nje ya sanduku la kibepari, ambalo yeye mwenyewe ni sehemu yake, na ananufaika na ufisadi na muozo wake?!

Kinachotarajiwa kwa mtumishi huyu muovu ni kwamba ataendelea na hali ya sasa ya nchi yake ya uhalifu wa kimataifa na ufisadi wa ndani. Hataweza kufanya zaidi ya yale ambayo nchi yake inafanya katika upande wa uhalifu, kwa kutumia nguvu zake zote ovu zilizotajwa hapo juu. Ataendelea kutumia njia na mbinu zilezile zilizotumiwa na watangulizi wake, watawala wa Marekani. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَى مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّهْهُ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَنْ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَهُوَ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ]

“Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa bwana wake. Popote anapo muelekeza haleti kheri. Je! Huyo anaweza kuwa sawa na yule anaye amrisha uadilifu,naye yuko juu ya Njia Iliyo Nyooka.” [Surah An-Nahl 16:75].

Ulimwengu, Mashariki ya Kati, na watu wa dunia hawataridhika na uamuzi wao huo mpaka mmoja wa kizazi cha Saad bin Abi Waqqas, kiongozi wa Vita vya Qadisiyah aje na kukata mkunga wa Trump na kumng'oa macho yake, katika Vita vyengine vya Qadisiyah, ambavyo pande zake mbili ni dola ya Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume na Amerika na washirika wake, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ateremshe juu ya majeshi yao, makundi ya ndege kama msaada, ili awafanye wasahau minong'ono ya Shetani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu