Ijumaa, 27 Shawwal 1446 | 2025/04/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuangazia Miaka 31 ya Mauaji ya Halaiki ya Rwanda

(Imetafsiriwa)

Habari:

Tarehe 7 Aprili 2025, Rwanda ilifanya kumbukumbu ya miaka 31 ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Inakadiriwa kuwa takriban Wanyarwanda milioni moja hususan kutoka kabila la Watutsi waliuawa ndani ya takriban miezi mitatu ya mauaji ya halaiki.

Maoni:

Mauaji haya ya halaiki ni kielelezo cha mfumo mchafu wa kibepari unaowagawa watu, ambapo kupitia ukoloni uliwagawanya watu ambao awali walikuaW wakiishi pamoja, wakiwa wameungana na kushirikiana.

Kuja kwa ukoloni mwishoni mwa karne ya 19 M, Rwanda kama yalivyo maeneo mengine yote yaliyotawaliwa liliingiziwa na wakoloni mgawanyiko kwa misingi ya kikabila (maeneo mengine yaligawanywa kwa msingi wa dini, rangi, nk.) kati ya makabila mawili makuu ya Wahutu na Watutsi. Baada ya uhuru wa bendera wa mwaka 1962 mgawanyiko ambao ulipandwa na kukuzwa na ukoloni ulikuwa umeiva na ulikuwa ni bomu lililotegwa likisubiri kulipuka tu.

Mwishowe, mwaka 1994 Mauaji ya Halaiki yalifanyika ambayo yalilenga zaidi kulinda maslahi ya wakoloni wa Magharibi. Serikali ya Rais Habyarimana iliyokuwa na Wahutu walio wengi iliungwa mkono na Ulaya, hususan Ufaransa, Ubelgiji na Uingereza kupitia Zaire (DRC Congo na Tanzania). Kwa upande mwingine, waasi wa upinzani wa Kitutsi wa “Rwandan Patriotic Front” wa Kagame wao waliungwa mkono na Marekani kupitia Uganda.

Kwa hiyo, mataifa ya kikoloni ya Magharibi yaliwasukuma baadhi ya watawala na waasi ndani ya Afrika Mashariki kushiriki katika mauaji ya halaiki ya kihistoria huku wao Wamagharibi wakitazama tu ili kutimiza ajenda yao ya kikoloni na ya kinyonyaji, wakijiweka pembeni na misimamo yao ya uwongo kwamba wao ni watetezi wakubwa wa haki za binadamu, kama hali kama hiyo mbaya zaidi inayoendelea sasa huko Gaza.

Inasikitisha sana kwamba baada ya miaka 31, kile kile kilichofanya mauaji ya halaiki kuibuka ndani ya Rwanda bado kipo. Mauaji ya halaiki, mapinduzi ya kisiasa yanayoungwa mkono na wakoloni, kamwe hayakufanya na hayatofanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya watu nchini Rwanda.

Rwanda bado ipo tete katika mgawanyiko mkubwa kati ya makabila mawili makuu - Wahutu na Watutsi. Haishangazi kwamba uchu wa ukoloni unaweza kulazimisha mapinduzi mengine au mauaji ya halaiki katika siku zijazo ili kujiimarisha na kulinda zaidi maslahi yao (wakoloni).

Vyovyote iwavyo, ukweli ulio wazi ni kwamba kuikomboa Rwanda na ulimwengu kiujumla, mfumo mbadala unahitajika ambao ni Uislamu chini ya dola yake ya Khilafah. Kwa kuwa uwongo wa demokrasia wala ukatili wa udikteta havina uwezo wa kuiokoa Rwanda. Kwa sababu mawili hayo (demokrasia na udikteta) ni pande mbili za sarafu moja ya ubepari.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Kufeli kwa Ruwaza ya Burundi 2025

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu