- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ni Nani Anayeupiga Vita Ummah?
(Imetafsiriwa)
Habari:
Takriban watu 24, wakiwemo watoto, wameuawa katika milipuko katika eneo la kijijini la Khyber Pakhtunkhwa kaskazini magharibi mwa Pakistan, na kusababisha wito wa uchunguzi wa tukio hilo. Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mauaji ya raia hao wakiwemo wanawake na watoto. (aljazeera.com)
Maoni:
Mauaji ya hivi majuzi ya takriban watu 22 katika Bonde la Tirah sio tu yameibua mshtuko mkubwa miongoni mwa watu, pia yamewafanya kuhoji uhalisia wa suala hilo. Huku Waislamu kote duniani wakiwa tayari wamechanganyikiwa na kimya cha uongozi wao kuhusu mauaji ya halaiki yanayoendelea mjini Gaza, kushuhudia matukio ya aina hii kutachochea moto dhidi ya watawala katika nyoyo za watu. Tukio hilo lilishuhudiwa na kurekodiwa zaidi na wenyeji, ambao wanataka kuzuia kurudiwa kwa uhamishwaji wa raia, ni tukio la kutisha ambalo linabakia katika kumbukumbu ya pamoja ya wakaazi wa eneo hilo. Mazingira ya ndani yanafurika hadithi za zamani wakati Wapashtun walilipiza kisasi dhidi ya Ubeberu wa Uingereza, na kuwapa hadhi ya kishujaa kama walinzi wa Ardhi na Sheria ya Kiislamu. Serikali ya Khyber Pakhtunkhwa ambayo inatoka kwa upinzani imedai “mizinga na mabomu yalirushwa” kwa wenyeji. Maoni miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo, viongozi wa kisiasa na wazee wa kabila yanatokana na kutiliwa shaka na uoga kutokana na operesheni za awali, na kusababisha vifo vya raia na kuhama makaazi yao. Ili kuepuka uharibifu wa aina hii, wazee wa eneo hilo walifanya jitihada za kushikilia Jirga iliyofeli kwa uongozi wa wanamgambo, ambapo walitaka utabikishwaji wa Sharia, katika eneo la Waziristan hadi Bajaur. Hili ni onyesho la vipengee vyote vinavyotaka kutawala eneo hili, serikali, upinzani na jeshi. Wote wa tatu kwa mara nyengine tena wamewasaliti watu na hivyo wamemsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw).
[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَآؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيما]
“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [An-Nisaa’: 93].
Katika historia ya Kiislamu, tunayo mifano pindi utakatifu wa damu ya Muislamu ulipokiukwa. Hata hivyo historia pia inarekodi nyakati ambapo viongozi wa Kiislamu waliinuka kutetea na kulipiza kisasi mateso ya watu wao. Ulimwengu ulimshuhudia Salahuddin Ayyubi akiwanyenyekesha Makruseda na Sultan Qutuz akiwashinda Wamongolia huko Ain Jalut. Lakini historia pia inatuonya: wakati wowote Waislamu walipogeuziana panga zao wao kwa wao, iliacha majeraha ndani zaidi— mwangwi wa mgawanyiko na huzuni ambao unasikika katika vizazi.
Uislamu ni dini ya uwazi na ina kanuni za wazi kabisa za kupigana.
Imepokewa kutoka kwa Abu Musa (ra): أن أعرابيا أتى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله الرجل يقاتل للمغنم، والرجل يقاتل ليذكر، والرجل يقاتل ليرى مكانه؟ Alikuja bedui mmoja kwa Mtume (saw) na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtu mmoja anapigana kwa ajili ya ngawira, mwengine anapigana ili apate umaarufu, na wa tatu anapigana kwa ajili ya kujionyesha.” Riwaya nyengine ni: يقاتل شجاعة، ويقاتل حَمِيّة “Mmoja anapigana kwa ajili ya kuonyesha ushujaa wake, mwengine anapigana kutokana na fahari ya familia yake.” Riwaya nyengine ni: ويقاتل غضبًا، فمن في سبيل الله؟ “Mtu anapigana kwa hasira.” Akauliza: “Ni nani kati yao anayepigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu?” Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «من قاتل لتكون كلمة الله هي العليا، فهو في سبيل الله» “Mwenye kupigana ili Neno la Mwenyezi Mungu litukuzwe, huyo ndiye anayepigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu.” [Al-Bukhari na Muslim].
Pakistan kwa uwezo wa kijeshi ilionao inaweza kuwa nguvu kwa Umma wa Kiislamu. Wapiganaji kutoka maeneo ya kikabila wanaweza kuwa jeshi la Ummah. Badala yake uongozi wake wa wasaliti unaendelea kuingiliana na vigogo na maafisa wa adui, kufichua siri zetu, kuuza rasilimali zetu na kutafuta mwongozo, kuunga mkono uingiliaji kijeshi wa Magharibi na kiuchumi katika ardhi za Waislamu. Ni kwa maslahi ya ulimwengu wa kimagharibi na watumwa wake kunyamazisha sauti inayotaka sharia. Vikosi vya Usalama vya Pakistan lazima vifafanue sababu ya ‘Operesheni Sarbakaf’ iliyozinduliwa mnamo tarehe 29 Julai 2025 dhidi ya wanamgambo wa TTP (Tehreek Taliban Pakistan) na ISKP (Islamic State Khurasan Province) katika eneo la Bajaur. Makundi haya pia lazima yaelewe kwamba Sharia inatabikishwa na Dola chini ya uongozi wa mtawala muadilifu, ambaye ana uwezo sio tu wa kutangaza bali kutabikisha na kulinda na kueneza sheria. Iwapo kama inavyodaiwa wapiganaji hawa wa kikabila watakuwa tatizo kwa Dola basi Dola itawashughulikia kwa mujibu wa hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) na itaweza kuwafanya mfano kwa khiyana yao. Sababu ya kimya cha Serikali ni kwa sababu haijui simulizi yoyote ambayo ufundi wake utawaridhisha wananchi.
Ni Khilafah kwa njia ya Utume ambayo kwa mara nyengine tena haitatekeleza tu Shariah bali itahakikisha kwamba inamfikia kila moyo wenye papatiko la kuitafuta katika hali yake safi kabisa. Waislamu, wa maeneo ya kikabila na katikati ya dunia lazima wafanye kazi kwa ajili ya kusimamisha Khilfah kwani hiki ndicho kitambulisho pekee cha kweli kwa ulimwengu huu ambacho kitawasaidia kujishindia akhera.
[إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُم بَيْنَ النَّاسِ بِالْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ الْهَوَى فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ إِنَّ الَّذِينَ يَضِلُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا نَسُوا يَوْمَ الْحِسَابِ]
“Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.” [38:26]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan