- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kuwakataa Wanariadha wa ‘Israel’: Kipimo Halisi cha Msimamo Madhubuti wa Indonesia?
(Imetafsiriwa)
Habari:
Indonesia: Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ilikataa rufaa ya Shirikisho la Michezo ya Viungo (Gymnastics) la ‘Israel’ (IGF) kuruhusu wanariadha wake kushiriki Mashindano ya Dunia ya Sanaa za Gymnastiki jijini Jakarta, Indonesia, kuanzia Oktoba 19–25, 2025. Serikali ya Indonesia iliwanyima viza wachezaji sita wa mazoezi ya viungo wa ‘Israel’, ikionyesha uungaji mkono kwa Wapalestina na shinikizo la ndani. IGF ilkata rufaa kwa CAS na Shirikisho la Kimataifa la Gymnastiki (FIG), ikiomba hatua za kuhakikisha ushiriki au kubatilisha michezo hiyo. CAS ilitupilia mbali rufaa zote mbili, na FIG ilisema haina mamlaka juu ya maamuzi ya visa. Indonesia ilithibitisha tena msimamo wake, ikiegemea katika sera yake ya kigeni na hisia za umma. (Chanzo: en.antaranews.com)
Maoni:
Uamuzi wa Indonesia wa kukataa ushiriki wa wanariadha wa ‘Israel’ katika Mashindano ya Ulimwengu ya Gymnastiki ni hatua ya kupongezwa na ya kimaadili. Inaonyesha msimamo thabiti wa Indonesia kuelekea ‘Israel’. Hatua hii inapaswa kuzingatiwa kama hatua ya awali kwa Indonesia kuchukua msimamo thabiti na madhubuti kuhusu uwepo wa umbile la Kiyahudi nchini, sio tu katika michezo lakini pia katika maeneo mengine kama vile uchumi, utalii, elimu na kwengineko.
Ingawa Indonesia mara kwa mara imeonyesha uungaji mkono mkubwa kwa uhuru wa Palestina na haina mahusiano rasmi wa kidiplomasia na umbile la Kiyahudi, mahusiano yasiyo rasmi yanaendelea kuwepo. Katika miaka ya hivi karibuni, wanariadha kadhaa wa ‘Israel’ wameshiriki mashindano nchini Indonesia licha ya kukosekana kwa mafungamano rasmi ya kidiplomasia. Miongoni mwao ni Misha Zilberman, mchezaji wa badminton ambaye alishiriki katika Mashindano ya Dunia ya BWF ya 2015 jijini Jakarta; Yuval Shemla, mpanda mlima ambaye alijiunga na Kombe la Dunia la Kukwea la IFSC 2022 jijini Jakarta; na Mikhail Yakovlev, mwendesha baiskeli aliyeshinda medali ya shaba kwenye Kombe la Mataifa ya UCI Track 2023. Kwa kuongezea, ujumbe wa wabunge wa Israel ulihudhuria Mkutano wa 144 wa Muungano wa Mabunge (IPU) uliofanyika Bali mnamo 2022, ingawa sio kama wageni rasmi wa serikali ya Indonesia.
Kwa mtazamo wa kibiashara, licha ya kukosekana kwa mahusiano rasmi ya kidiplomasia, shughuli za kibiashara kati ya Indonesia na ‘Israel’ zinaendelea kupitia waunganishi wengine kama vile Singapore na Hong Kong. Mnamo 2024, uagizaji wa Indonesia kutoka ‘Israel’ ulifikia takriban dolari milioni 54.2, ukijumuisha hasa mashini za kimekaniki, vifaa vya umeme, zana za macho na bidhaa za dawa. Wakati huo huo, mauzo ya Indonesia kwa ‘Israel’ yalifikia karibu dola milioni 236, na bidhaa muhimu ikiwa ni pamoja na viatu vya ngozi, mafuta ya nazi, na bidhaa za nguo. Vile vile, katika sekta ya utalii, maelfu ya raia wa ‘Israel’ wameruhusiwa kuzuru Indonesia, huku Waindonesia wengi pia wakisafiri hadi umbile la Kiyahudi.
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa msimamo wa Indonesia kuelekea Israel haujakuwa thabiti kabisa. Kwa hivyo, kukataliwa kwa hivi majuzi kwa wanamichezo ya viungo wa ‘Israel’ kunafaa kuashiria mwanzo wa sera thabiti na ya kina dhidi ya ‘Israel’ katika sekta zote. Hata hivyo, ikiwa kukataliwa huku hakufuatiwi na uthabiti mpana zaidi, kunazua swali muhimu: je, uamuzi huo ulichochewa kweli na mshikamano kwa Palestina, au ni jibu tu kwa shinikizo la umma linalopinga uwepo wa Israel nchini Indonesia?
Itakuwa ni jambo la kusikitisha ikiwa shinikizo la umma ndilo sababu pekee. Hali kama hiyo itaashiria kwamba msimamo wa serikali ya Indonesia kuhusu Palestina hauna ikhlasi na kwamba Indonesia haina tofauti na nchi zengine zinazoiunga mkono Palestina kwa maneno huku zikidumisha mahusiano ya kivitendo na umbile la Kiyahudi.
Hali hii inapaswa kutumika kama tafakari kwa umma wa Indonesia – kuendelea kuhimiza serikali kuchukua hatua kwa maneno na vitendo kwa uthabiti. Zaidi ya hayo, inapaswa kuwa funzo kwa jamii pana ya Kiislamu kwamba maadamu serikali katika ulimwengu wa Kiislamu zitaendelea kujifunga na maslahi ya kitaifa, masuala ya kibinadamu na Kiislamu yataendelea kuwekwa kando. Kwa hiyo, Waislamu lazima wasiyafunge mapambano yao kwa masuala ya muda mfupi tu bali wajitahidi kusimamisha utawala wa Kiislamu unaojitolea kikweli kwa maslahi ya Umma wa Kiislamu duniani.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb utTahrir na
Abdullah Aswar