Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni 

Je, Kirusi cha Korona ni Adui wa Watu Wote?

Habari

Katika kongamano la video alilofanya Raisi Erdogan pamoja na mameya juu ya "kupambana" dhidi ya virusi vya Korona ambavyo vimeikamata Uturuki na ulimwengu kwa jumla, alivitangaza virusi vya Korona  kama adui kwa kila mtu, akafafanua mkakati wake wa kupambana navyo na akasema “Kwa hali hii ya ghafla sote tunapambana na adui mjanja ambaye anatishia mustakbali wa nchi yetu na maisha ya watu wetu . Adui aliye mbele yetu anaitwa virusi vya Korona. Njia pekee ya kumshinda adui huyu ni kwa kushikana pamoja. Tunaweza kulishinda hili tishio pekee kwa mshikamano. Leo ni siku ya kukumbuka udugu wetu wa milele, kuweka pembeni tofauti zetu zote za kisiasa, kikabila na kimadhehebu. Leo ni siku ya kuungana pamoja dhidi ya adui wetu sote, kama vile inavyo kuwa katika vita vya uhuru”

Maoni

Ni kana kwamba Raisi Erdogan hazungumzii kuhusiana na kirusi kidogo mno kiitwacho COVID- 19 kisicho onekana kwa macho yetu ya kawaida isipokuwa kwa darubini ya kieletroniki, bali nguvu vamizi ambayo inatishia kuharibu mustakbali wa nchi yetu na maisha ya watu wetu, mlowezi, kundi la wauaji wenye silaha za maangamizi makubwa au sio hivyo?

Lau kama angalitoa wito huu dhidi ya mvamizi Mwamerika na kuhimiza taifa zima kushikamana kwa pamoja kupambana dhidi ya Mwamerika, na kama angekuwa wa kwanza kuanzisha vita hivi, tungemthamini Raisi huyu kikweli kweli na kutembea nyuma yake hatua kwa hatua dhidi ya adui wa kila mtu, Mwamerika .Kama angetoa wito huu dhidi ya umbile la Kiyahudi “Israel”, uchafu ambao upo ndani ya Palestina na Mashariki ya Kati kama vile uvimbe ulojaa usaha kwa zaidi ya miaka sitini, kila Muislamu anaye ishi nchini Uturuki na watu kutoka nchi zote za Waislamu wasinge baki majumbani, bali wangekuwa wenye kuandamana kuelekea Al-Aqsa ili kuisafisha ardhi hiyo iliyo barikiwa kutokana na uchafu huu. Lakini Erdogan haoni kundi hili kubwa la waovu na wauaji ambao wameeneza ufisadi kwenye ardhi kama adui wa kila mmoja, lakini anaona ugonjwa wa virusi hivi kama adui kwa kila mtu ambao kwa hakika husafiri katika mabara kama mtihani kwa wanaadamu.

(ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ)

“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu” [Ar-Rum 41]

Sielewa vipi Erdogan ameweza kulinganisha kati ya virusi vya Korona na adui katika vita vya uhuru vinavyo piganwa na vijana wa Ummah wa Kiislamu dhidi ya wavamizi walio kuja kutoka Magharibi na kuugawa ulimwengu wa Kiislamu.

Korona sio roboti iliyo tengenezwa na mwanaadamu, au silaha ya maangamivu wala adui kama hivyo. Ikiwa Raisi kweli anaamini kwamba Korona ni silaha ya kibaolojia iliyo tengenezwa katika mazingira ya kimaabara - na hatudhani ni hivyo - basi anatakiwa kumlenga adui halisi aliye kitengeneza, na sio kirusi cha Korona. Mapambano dhidi ya kirusi hiki yanahitaji kuchukua tahadhari dhidi ya majanga kwa utambuzi na utabiri, kutafuta madawa kwa ajili ya matibabu; Mwanzo kabisa ni kumtegemea Mwenyezi Mungu. Na ina hitajika kuwakumbusha watu hili. Inahitajika karantini inayo stahiki ili kuepusha kusambaa kwa virusi hivi na kukidhi mahitaji msingi ya watu wetu ambao hawawezi kufanya kazi katika kipindi hiki.

Vilevile inahiji tupate funzo kutokana na ukweli kwamba kirusi hiki kimedhihirisha kuanguka kwa nidhamu ya kirasilimali inayo tawala ulimwengu mzima, na kuiona hii kuwa ni fursa ya kuirudisha Khilafah Rashidah, nidhamu ya utawala wa Kiislamu.   

Tusisahau kwamba Mwenyezi Mungu ndiye pekee anayejua kheri na shari ya kirusi hiki.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mahmut KAR

 #Covid19   #Korona  كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 16 Aprili 2020 14:51

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu