Alhamisi, 05 Rabi' al-awwal 1442 | 2020/10/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa vya Habari 03/10/2020

Vichwa vya Habari:

Donald Trump Amesafirishwa kwenda Hospitali kwa Matibabu Baada ya Kugunduliwa ana Covid-19

Mapigano Yazuka katika Maandamano ya Kupinga Serikali Nchini Misri

Amerika Yasalia kuwa Mnunuzi Mkubwa Zaidi wa Bidhaa za Pakistan

Maelezo:

Donald Trump Amesafirishwa kwenda Hospitali kwa Matibabu Baada ya Kugunduliwa ana Covid-19

Rais wa Amerika Donald Trump amepelekwa katika hospitali moja ya kijeshi kwa ajili ya matibabu baada ya kugunduliwa ana Covid-19, afisa mmoja wa Ikulu ya White House alisema mnamo Ijumaa, huku kampeni yake ya uchaguzi na idara yake ziking'ang'a kuzoea mkengeuko usio wa kawaida katika urais wake matata. Bwana Trump, mwenye umri wa miaka 74, atakaa katika Kituo cha Kitaifa cha Matibabu cha Kijeshi cha Walter Reed huko Bethesda, Maryland, kwa siku chache zijazo kama hatua ya tahadhari, afisa huyo alisema. Madaktari walihimiza hatua hiyo ili Bw Trump apate huduma ya haraka endapo itahitajika, afisa huyo alisema. Bwana Trump alionekana akipanda helikopta ya rais ya Marine One katika Ikulu ya White House mnamo Ijumaa jioni. Rais alituma video kwenye mtandao wa Twitter akiwashukuru watu kwa msaada wao, na kuongeza kuwa anadhani kuwa "anaendelea vizuri sana". Bwana Trump hakuhamisha madaraka kwa Makamu wa Rais Mike Pence kama ambavyo marais wengine wakati mwingine wamefanya wakati wa matibabu, kulingana na afisa mmoja wa Ikulu ya Whitehouse. Mgeuko wa hivi karibuni ulikuja baada ya daktari wa Ikulu ya White House Sean Conley kuandika kwamba rais "angali amechoka lakini katika hali nzuri". Dkt. Conley alisema rais amepewa jaribio la kingamwili la Regeneron, pamoja na zinki, vitamini D, famotidine, melatonin na aspirini. Bwana Trump, ambaye amepuuza tishio la janga la maambukizi ya virusi vya korona tangu mwanzo, aliandika kwenye Twitter mapema Ijumaa kwamba yeye na mkewe Melania wanakwenda karantini baada ya vipimo kuonyesha wana virusi hivyo, ambavyo vimeua zaidi ya Waamerika 200,000 na kuharibiwa vibaya uchumi wa Amerika. [Chanzo: The National].

Kwa miezi kadhaa, Trump amepuuza ukali wa Covid-19 na kuwakejeli watu kwa kuvaa barakoa. Hivi sasa wiki chache tu kabla ya uchaguzi, Trump ameshambuliwa na virusi hivi na kuna nafasi nzuri kwamba anaweza kukosa uwezo na hivyo kudhoofisha mchakato mzima wa uchaguzi. Uasisi wa kisiasa wa Amerika kwa kazi ya mikono yao wenyewe unaharibu msimamo wa Amerika nyumbani na ng'ambo.

Mapigano Yazuka katika Maandamano ya Kupinga Serikali Nchini Misri

Mwanamume mmoja Mmisri ameuawa katika mapigano kati ya waandamanaji na polisi wakati wa maandamano katika kijiji kimoja kusini mwa Cairo dhidi ya Rais Abdel Fattah el Sisi. Maandamano madogo yanayopinga serikali yamefanyika katika siku za hivi karibuni katika vijiji vichache katika maeneo kadhaa ya nchi, kulingana na video zilizosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, haswa na wapenzi wa kundi lililopigwa marufuku la Ikhwan al-Muslimina. Vyanzo vya matibabu katika hospitali ya Al Ayat huko Giza, nje ya mji mkuu wa Cairo, vilisema "mwili wa mtu mmoja uliokuwa na majeraha ya risasi usoni na kifuani ulifikishwa hospitalini usiku wa Jumamosi". Mawakili maarufu wenye kutetea haki walisema kwenye mtandao wa Facebook kwamba zaidi ya watu 150 walikamatwa katika maandamano hayo. Misri ilipiga marufuku maandamano chini ya sheria ya uzuizi mnamo 2013 kufuatia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais Mohamed Morsi. Nchi hiyo pia tangu 2017 imekuwa chini ya hali ya dharura inayoweza kurejeshwa upya, ambayo makundi ya kutetea haki yanasema imeruhusu serikali kukandamiza wapinzani. Maandamano hayo madogo yalikwenda sambamba na kuongezeka kwa hasira, haswa katika maeneo ya vijijini na ya kipato cha chini, dhidi ya wingu la kampeni za serikali za kukomesha ujenzi haramu, ambao umewataka watu kulipa faini ili kuhalalisha umiliki wa nyumba zao. Katika wiki za hivi karibuni, wito pia ulitolewa kutoka kwa mfanyabiashara aliye uhamishoni Mohamed Ali, akiwataka watu waingie mabarabarani dhidi ya Sisi na serikali yake. Ali, mwanakandarasi wa ujenzi na mwigizaji imara, alikuwa ameingia kwenye uwanja wa kisiasa wa Misri mwaka jana wakati video alizochapisha kwenye mitandao ya kijamii zikimkashifu Sisi na kipote cha jeshi kwa ufisadi zikisambaa mno. Mnamo Septemba 20, 2019, mamia ya watu waliingia mabarabarani jijini Cairo na maeneo mengine ya nchi kuitikia wito wa Ali, ikipelekea majibu mazito kutoka kwa vikosi vya usalama. Makundi ya kutetea haki yalisema wakati huo kwamba watu 4,000 walikamatwa, wakiwemo wasomi mashuhuri, wanaharakati na mawakili. [Chanzo: TRT].

Licha ya namna ambavyo Sisi anajaribu kwa nguvu kuwakandamiza raia wa Misri, wataendelea kuasi. Enzi ya utawala dhalimu wa Misri ilianza kudhoofika kwa kuanguka kwa Mubarak na inazidi kudhoofika wakati wa utawala wa Sisi. Ni suala la muda tu kabla ya Khilafah Rashida kujitokeza.

Amerika Yasalia kuwa Mnunuzi Mkubwa Zaidi wa Bidhaa za Pakistan

Amerika imesalia kuwa sehemu kuu ya uuzaji bidhaa nje wa Pakistan katika mwezi Agosti ambapo nchi ilipata mapato ya $ 334.5 milioni mnamo Agosti, hata waliposhuhudia punguzo ikilinganishwa na $ 341.08 milioni katika kipindi hicho hicho cha 2019. Kulingana na data iliyotolewa na Benki Kuu, Pakistan ilipokea $ 671.75 milioni kutoka Amerika wakati wa Julai-Agosti, ikilinganishwa na $ 714.63 milioni katika miezi sawia na hii ya 2019 - ikisajili kupungua kwa asilimia sita. Uingereza ilikuwa mnunuzi wa pili mkubwa kutoka Pakistan kwa $ 129.17 milioni mnamo Agosti, chini ya asilimia 6.1 zaidi kwa $ 137.56 milioni katika kipindi sawia na hiki mwaka jana. Kwa upande mwingine, usafirishaji wa bidhaa za Pakistan kwenda Ujerumani uliongezeka kwa asilimia 6.75 hadi $ 111.79 milioni mnamo Agosti, kutoka $ 104.725 milioni mwezi huo huo wa 2019. Ikafuata China ambayo ilinunua bidhaa zenye thamani ya $ 93.649 milioni kutoka Pakistan katika mwezi uliofanyiwa uhakiki, ikishuka kwa asilimia 25.88 zaidi ya $ 126.345 milioni katika kipindi kama hicho mwaka jana. Imarati ilifuata kwa karibu ikinunua bidhaa za Pakistan zenye thamani ya $ 93.219 milioni mnamo Agosti, chini na asilimia 6.51 ikilinganishwa na $ 99.714 milioni mwezi huo huo wa 2019.

Wakati huo huo, usafirishaji bidhaa kwenda Afghanistan uliongezeka kwa asilimia 5.36 mwaka hadi mwaka hadi $ 60.975 milioni mnamo Agosti, kutoka $ 57.873 milioni. Kwa upande mwingine, Pakistan bila kushangaza iliagiza bidhaa nyingi kutoka China kwa $ 783.365 milioni mnamo Agosti, ikipanda kwa asilimia 1.84 kutoka $ 769.235 milioni mwezi huo huo wa 2019 huku ikitumbukia kwa asilimia 28.88 ikilinganishwa na $ 1.101 bilioni mnamo Julai. Uagizaji kutoka Imarati pia uliongezeka kwa asilimia 3.78 mwaka hadi mwaka hadi $ 559.544 milioni mnamo Agosti, kutoka $ 539.154 milioni huku Dubai ikipata mgao mkubwa zaidi ya thamani hiyo. Nchi hiyo ilinunua bidhaa zenye thamani ya $ 192.378 milioni kutoka Singapore wakati wa Agosti, ambayo iliwakilisha kupungua kwa karibu asilimia 7 mwaka hadi mwaka dhidi ya mwezi sawia na huu kwa takwimu ya mwaka jana ya $ 206.788 milioni. [Chanzo: Dawn News]

Pakistan ina matatizo mawili makuu kuhusu mkakati wake wa uuzaji bidhaa nje. Kwanza, Pakistan haina usafirishaji wa kutosha wa bidha nje ili kupata pesa za kigeni kulipia uagizaji. Pili, uuzaji mkubwa wa bidhaa nje wa Pakistan unategemea dola kuu, ambapo inaweza kufunga mlango kwa mauzo ya nje ya bidhaa ya Pakistan. Sababu zote mbili zinachangia mgogoro wa kuendelea wa mizani ya malipo ya biashara za kimataifa.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu