Jumatatu, 13 Rajab 1446 | 2025/01/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 21/11/2020

China Yaiona Fursa ya Kibiashara ambayo Amerika Imeikosa kwa Sababu ya Ulafi wa Kirasilimali

Siku siku ya Ijumaa, Rais Xi Jinping wa China, akiwa ametia saini makubaliano makubwa zaidi ya kibiashara ulimwenguni, Ushirikiano Kamili wa Kiuchumi wa Kikanda (RCEP), alisema kwamba "atazingatia vyema kujiunga na Makubaliano Kamili na ya Maendeleo ya Ushirikiano wa Kati ya Pasifiki [CPTPP]", kulingana kwa Newsweek. Hakuna yoyote katika makubaliano yanayoijumuisha Amerika.

Rais wa Amerika Barack Obama alifanya kazi kwa bidii wakati wa kipindi chake ili kuunda Ushirikiano wa Kati ya Pasifiki (TPP) ili kuimarisha biashara kati ya mabara ya Amerika na Asia, akitia saini makubaliano hayo mnamo 2016. Lakini, bila shaka, TPP ikawa jukwaa la kuongezeka kwa ubepari wa Kirasilimali ikitoa fursa kubwa zaidi kwa kampuni za kimataifa za Amerika kunyonya nguvu kazi na masoko ya nchi zinazo endelea. Umma wa Amerika ulipinga, sio kwa sababu ya unyonyaji wa wengine lakini kwa sababu wamekuja kuona matumizi ya nguvu kazi ya bei rahisi ya nchi zingine kama yenye kuwanyima wafanyikazi wa Amerika kazi. Matokeo yake, TPP ikawa ni suala kuu la uchaguzi mnamo 2016, na wagombea wote wa urais walilazimika kuahidi kujiondoa kutokana nalo, Rais wa Amerika Donald Trump akifanya hivyo baada ya kuingia afisini mwaka uliofuata. Sasa inaangukia kwa China kufaidika ambapo Amerika ilipoteza.

Magharibi ya Kirasilimali inahitaji "biashara huru" lakini kwa kweli huitumia hii kwa ajili ya miundo ya kibepari kwa ulimwengu mzima. Ni Uislamu pekee, chini ya Khilafah, ambao uliasisu kikweli biashara wazi ya kiulimwengu kwa zaidi ya miaka elfu moja, nidhamu hii ya kimataifa, ikiwa sababu ya halisi ya kuongezeka kwa ufanisi wa Magharibi kabla ya ujio wa Urasilimali karibu miaka mia mbili iliyopita.

Pakistan, Afghanistan, Sudan, Ufaransa

Wiki hii, Pakistan iliona maandamano makubwa yanayounganisha mji mkuu yanaokadiriwa kufikia makumi ya maelfu na kuitishwa na Allama Khadim Rizvi kupinga tabia ya matusi ya Ufaransa kwa Mtume (saw) lakini uangaziaji wa vyombo vya habari ulizuiliwa kabisa na serikali ya Pakistan. Matembezo yalidhibitiwa mno ndani na nje ya mji mkuu, na matumizi ya mtandao yalizuiliwa katika maeneo mengi. Kiongozi aliye katika kiti cha magurudumu na mgonjwa alikufa muda mfupi baada ya kushiriki katika maandamano yaliyofanyika kwa vifaa vichache wakati wa baridi, Mwenyezi Mungu akubali kujitolea mhanga kwake, amsamehe, na amwinue. Janaza yake jijini Lahore pia ilikusanya makumi ya maelfu lakini kwa mara nyengine tena uangaziaji wa vyombo vya habari uko chini mno. Vyombo vya habari, iwe ni katika nchi za Kiislamu au Magharibi, vinadhibitiwa kikamilifu na serikali hata wakati vinamilikiwa kibinafsi. Kwa kweli, Umma wa Kiislamu umejitolea kwa nguvu kwa Uislamu na uko karibu kuusimamisha tena lakini vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa vinadhibitiwa vikali ili kuzuia muonekano wowote wa hili.

Mujahidina wanapata faida kubwa nchini Afghanistan huku Waamarika wakiendelea kuondoa vikosi vyao pamoja na shambulizi la wiki nzima kusini mwa Afghanistan, kulingana na Washington Post. Kama zilivyo juhudi zote za kibepari za Kimagharibi, udhibiti wa Amerika wa Afghanistan umesababisha tu ghasia kali kutoka kwa watu wa Afghani. Magharibi wanadai kuleta maadili ya jumla ya kiulimwengu ambayo yanawanufaisha wote. Lakini maadili kama uhuru na demokrasia ni vielelezo ambavyo havina uhalisia wowote wa kivitendo ima Magharibi au mahali pengine. Uhuru ni upotoshaji wa hali moja ya utawala wa binadamu, ambao ni haja ya kutambua haki za watu. Na demokrasia ni upotoshaji wa jambo jengine, ambalo ni haja ya serikali kuwajibika hadharani. Lakini utawala bora ni gumu zaidi kuliko haya, na Magharibi hutumia tu maadili kama haya kuficha unyonyaji wao wa kibepari wa Kirasilimali nyumbani na ng'ambo. Umma wa Kiislamu umeikataa Magharibi na maadili yake. Kilichobaki ni kudhihirika kivitendo kwa ukataliwaji huu kwa umbo la Dola ya Khilafah Rashida ya Kiislamu kwa njia ya Mtume (saw).

Putin wiki hii aliidhinisha mipango ya serikali ya kuunda kituo cha majini nchini Sudan, kulingana na Al-Monitor. Sudan iko chini ya udhibiti imara wa Amerika, huku jeshi linalosaidiwa na mkono wa Amerika likiwa katika udhibiti kamili wa baraza kuu la enzi linalosimamia serikali ya Sudan. Kwa hivyo, tangazo hili lazima lionekane kama mfano mwingine wa Amerika kuajiri kwa uaminifu na kupanua shughuli za jeshi la Urusi kuunga mkono malengo ya Amerika na kukabiliana na ushawishi wa Ulaya. Ingawa wanashirikiana katika hadhara, dola za Magharibi zinabakia kuwa mahasimu na washindani, kama vile zilivyokuwa nyakati za Kikristo, kwa wafalme wa Ulaya na wakuu wakishindana huku wakidai utiifu kwa papa mmoja na kanisa moja. Hata katika kina cha vita baridi, Amerika ilihiari kuunda tafrija na adui yake mkuu Umoja wa Kisovieti ili tu kukabiliana na ujanja wa wahasimu wake huko Magharibi, ambao walitaka kufaidika na mizozo ya dola kuu zenye nguvu. Migogoro hii ya ndani ya Magharibi lazima ichunguzwe kwa karibu na viongozi wa Kiislamu na wanasiasa, kwani inatoa nafasi kwa dola ya Kiislamu itakayosimamishwa kupanda mara moja hadi kiwango cha dola kuu yenye nguvu katika maswala ya kiulimwengu.

Na huku Ufaransa inakiendelea kutekeleza mipango yake mikali dhidi ya Uislamu, Rais Emmanuel Macron wiki hii aliwapa viongozi wa Kiislamu ndani ya Ufaransa wiki mbili kuchora mkataba wa "maadili ya kijamhuri" ambao, kulingana na Middle East Eye lazima ujumuishe utambuzi wa maadili ya jamhuri, kufafanua kwamba Uislamu nchini Ufaransa ni dini na sio harakati ya kisiasa, na kukomesha ushiriki wa kigeni katika misikiti ya Ufaransa. "Ninaweka imani yangu kweni na nyinyi ni wadhamini wa imani yangu", Macron aliliambia Baraza la Ibada za Waislamu la Ufaransa mnamo Jumatano. "Ikiwa wengine hawatatia saini mkataba huu, tutavua matokeo kutokana na hilo." Nchi za Magharibi zitafeli katika miundo yao kwa jamii za Waislamu wanaoishi ndani yao. Mbinu hizi za kimabavu ni ushahidi mwingine tu kwamba Magharibi tayari imeshindwa vita vya kifikra na Uislamu.

Biden Atopewa Wito wa Kubadili Ile Inayoitwa 'Mikataba ya Amani' ya Trump

Ilhan Omar, mwanachama wa Baraza la Wawakilishi la Amerika, wiki hii alimwomba Rais Mteule wa Amerika Joe Biden kubadili mikataba ya amani ya Mashariki ya Kati iliyokamilishwa na Rais Trump wa Amerika, akisema kuwa hii sio mikataba ya amani bali ni mikataba ya silaha, inayowezesha nchi kama hizo kama Imarati katika vita vyake katika nchi zingine za Waislamu kama Yemen.

Kile ambacho Ilhan Omar anashindwa kutambua ni kwamba Amerika ndiyo iliyo nyuma ya serikali hizi za Kiislamu na vita ambavyo zimo ndani yake, na kwamba Amerika inapata kutoka kwao sio tu kushiriki kwao katika vita kama hivi bali pia ufadhili wao kwavyo. Kwa kuongezea, Amerika inataka sana kuona nchi za Kiislamu zikikubali uwepo wa uovu, upandikizaji wa mgeni katika nchi zao, umbile haramu la Kiyahudi ambalo limerithi dori na madhumuni ya umbile haramu la Kimsalaba ambalo lilikuwepo kwa muda mfupi katika ardhi hii hii miaka elfu moja iliyopita. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utainuka na kusimamisha dola yao, kuunganisha ardhi za Waislamu, kumfukuza kafiri wa kigeni, kuyakomboa maeneo yote yaliyokaliwa na wageni na kubeba nuru ya Uislamu kwa ulimwengu mzima.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu