Jumatatu, 17 Rajab 1442 | 2021/03/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 09/12/2020

Vichwa vya habari:

Sheikh wa Imarati Anunua Hisa za Timu ya Mpira wa Miguu ya Kizayuni

Maji Yamekuwa ni Bidhaa Mpya

Waislamu Nchini China Walazimishwa Kula Nyama ya Nguruwe

 Maelezo:

Sheikh wa Imarati Anunua Hisa za Timu ya Mpira wa Miguu ya Kizayuni

Sheikh mmoja wa Umoja wa Falme za Kiarabu ameinunua timu ya mpira wa miguu inayocheza katika ligi kuu ya Israel ambayo haina hata mchezaji mmoja wa kiarabu. Hamad bin Khalifa al-Nahyan, bilionea na mwanachama kutoka familia inayotawala Abu Dhabi, atachukua asilimia 49 ya hisa za timu ya Beitar Jerusalem na ameahidi kuwekeza zaidi ya shekels 300 katika miaka kumi ijayo. Dili hii inajiri miezi mitatu tu baada ya Imarati kuwa dola ya kwanza ya kiarabu kuimarisha uhusiano wake na Israel. Nchi hizo mbili, na Bahrain, zilisaini mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia katika Ikulu ya White House ukisimiwa na utawala wa Trump. Nchi za ghuba kwa muda mrefu zimewekeza utajiri wa Ummah katika miradi mibovu au wamekuwa wakisaidia Magharibi. Hivi sasa wanaweka wazi kabisa badala ya kuficha.

Maji Yamekuwa ni Bidhaa Mpya

Hivi sasa maji yamekuwa kama dhahabu, mafuta na baadhi ya bidhaa nyingine zinazofanyiwa biashara katika eneo la Wall Street. Wakulima, mashirika ya uwekezaji na manisapaa mbali mbali hivi sasa waweza kuzuia dhidi ya -- au kuweka dau juu ya –mustakbali wa upatikanaji wa maji katika jimbo la California, ambalo ni soko kubwa zaidi la kilimo nchini Amerika na la tano kwa ukubwa kiuchumi duniani.  Mikataba, ambayo ni ya kwanza ya aina yake nchini Amerika, ilitangazwa mnamo Septemba wakati ambao joto na moto wa porini viliharibu pwani ya magharibi na ukizingatia kwamba California imekuwa ikijikwamua kutoka katika miaka nane ya ukame. Wanakusudia kusaidia wote na ndo maana wanaweka uzio kwa watumiaji wakubwa wa maji, kama wakulima wa lozi na mifumo ya umeme, dhidi ya kupanda kwa bei za maji sambasamba na kupungua kwa wawekezaji duniani kote. Uhuru wa kumiliki unafanya kila kitu kinakuwa ni bidhaa ya kibiashara, kwa muda mrefu maji yamekuwa ni bidhaa inayouzwa na kununuliwa kupitia chupa lakini hivi sasa hata bei yake imekuwa kama kamari, ambapo kama hali ilivyo kwa rasilimali nyengine nyingi gharama yake wengi hawataweza kuimudu dunia nzima.

Waislamu Nchini China Walazimisha Kula Nyama ya Nguruwe

Sayragul, mkulima anayezuiliwa katika kambi maalum ameeleza kwa kifupi namna wanavyolazimishwa kula nyama ya nguruwe katika kambi za mateso za China na katika vituo vya uzuizi. Katika mahojiano ya hivi karibuni yaliyofanywa na Al Jazeera, mwanamke huyo alieleza mengine mengi ya kinyama na aibu ambayo watu wa Uighurs na jamii za Waislamu wachache zinavyofanyiwa. Hilo ni haramu katika Uislamu. “kila ijumaa, tumekuwa tukilazimishwa kula nyama ya nguruwe,” Sautbay alisema. “kwa makusudi kabisa wamechagua siku ambayo ni tukufu kwa Waislamu. Na kama ukikataa, unapata adhabu mbaya mno.” Hivi sasa China ipo katika mgogoro kuhusu umoja wa kindani ikizingatiwa kwamba vita vya kujitenga kati ya Hong Long na Taiwan vimepamba moto. Pamoja na ukuaji wa uchumi China imeshindwa katika jukumu la msingi la kuimarisha umoja wa kindani.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu