Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 19/05/2021

Vichwa vya Habari:

• Watawala wa Waislamu Wanapaswa Kuwahami Wapalestina

• Matatizo ya Idadi ya watu

 Maelezo:

Watawala wa Waislamu Wanapaswa Kuwahami Wapalestina

Baada ya kuwekwa wazi kwamba rais wa Amerika amepitisha mauzo ya silaha ya dolari milioni 735 kwa umbile la Kizayuni ili kuishambulia Gaza, baadhi ya wawakilishi kutoka upande wa Democrats wameibua wasiwasi wao kuhusu mauzo hayo. Mwakilishi Gregory Meeks (D-NY), ambaye ndiye kiongozi wa kamati inayoshughulikia mambo ya kigeni, aliwaambia watunga sheria kwamba atatuma barua kwa rais Biden akiomba kucheleweshwa kwa mpango wa kuizuia silaha ‘Israeli’. Lakini alifanya haraka katika mpango huo na kuwaambia waandishi wa habari kwamba anahitaji kufanya   “mazungumzo” kuhusu mauzo ya silaha,” Meeks alisema. “Kesho tutakuwa na mkutano na viongozi wakati ambapo mambo yatajadiliwa na atakaye kuwa na maswali yataulizwa, na hapo ndio kuna umuhimu wa kuizingatia barua.” Amerika imelipa ruhusa wazi umbile la Kizayuni kuwafanya Waislamu itakavyo, inalekeza uso upande mwengine wakati Waislamu wakichinjwa haioni. Hali hiyo ingetosha kwa watawala wa Waislamu kuwahami Waislamu wa Palestina kwa silaha. Kwa hakika hili lingekuwa ni pigo kubwa mno kwa Amerika na Mazayuni.

Matatizo ya Idadi ya watu

Wiki hii mataifa makubwa mawili duniani yameshindwa kuukwepa uhalisia – matokea ya sensa nchini Amerika na China yanaonyesha kuwa nchi zote mbili zinatarajiwa kuanza kupungua katika idadi ya watu kwa haraka zaidi kuliko walivyofikiria. Hiyo ni kwa sababu viwango vya uzazi vinashuka kwa haraka. Huku hilo likitokea, idadi ya watu inazidi kuzeeka, ambayo inaweza kuwa kikwazo kwa uchumi jambo ambalo serikali zinajitahidi kuliepuka. Amerika imeshuhudia kupungua kwa kiasi kikubwa cha idadi ya watu ikiwa ni matokeo ya kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa, kupungua kwa umri wa kuishi na kupungua kwa uhamiaji. Jumuisha vyote kwa pamoja bado unakuwa na idadi ya watu inayoongezeka, lakini kwa kiwango kidogo mno tofauti na zamani, na wakati huo huo idadi ya wazee inaongezeka zaidi katika Nchi. Takwimu za sensa za Amerika zinaonyesha hivi sasa kuna Waamerika wenye miaka 80 zaidi au kuwa wazee zaidi kuliko miaka 2 au chini zaidi. Sera ya China ya kuzaa mtoto mmoja pia imesababisha kutokuwa mizani sawa kwa idadi ya watu huku wenye kupokea malipo ya uzeeni hivi sasa wakikosa badali ya wafanyakazi wapya. Baada ya kuambiwa kwa miongo mingi kwamba kuna watu duniani wengi duniani uhalisia ni kuwa kasi ya idadi ya watu inashuka na itachukua karne kuanza kupungua. Lakini nchi nyingi za kimagharibi mfano Ujerumani, Urusi na hata Japan tayari zinakumbwa na kushuka kwa idadi ya watu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu