- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari 01/08/2021
Vichwa vya Habari:
Tunisia: Amerika Yaitaka Tunisia Kumaliza Mazungumzo na IMF Haraka Iwezekanavyo
Serikali ya Afghan Yakumbana na 'Hali ya Sintofahamu'
Amerika na China Zasema Zataka Kuepuka Mzozo wa Kijeshi, Lakini Hazijaafikana Namna ya Kuuepuka
Maelezo:
Tunisia: Amerika Yaitaka Tunisia Kumaliza Mazungumzo na IMF Haraka Iwezekanavyo
Waziri msaidizi wa wizara ya hazina ya Amerika inayoshughulikia mambo ya Afrika na kanda ya MENA Eric Meyer ameitaka Tunisia kuongoza kasi katika kumaliza mazungumzo na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ili kushughulikia mgogoro wa kiuchumi uliosababishwa na janga la maambukizi la COVID-19. Akipokelewa hivi karibuni na Gavana wa Benki Kuu ya Tunisia (BCT) Marouane Abassi, afisa huyo wa Amerika alikariri utayari wa nchi yake kuisaidia Tunisia katika kuamiliana kwake na taasisi za kifedha za kimataifa, kwa mujibu wa taarifa moja kwa vyombo vya habari iliyotolewa mnamo Jumatano jioni na BCT. Wakati wa mkutano huu uliohudhuriwa na balozi wa Amerika wa Tunisia Donald Blome na mwakilishi mmoja wa Wizara ya Mambo ya Kigeni, Uhamiaji na Watunisia wanaoishi Ng'ambo, gavana wa BCT alisema kwamba hivi sasa anafanya kazi na wadau wote ili kufanikisha mpango wa kuukomboa uchumi. Alitoa matumaini kwamba makubaliano na IMF yatafikiwa haraka iwezekanavyo ili kuweka mpango mpya wa kifedha, akisisitiza kwamba wadau wote wanafahamu "hali tete" inayoikabili Tunisia na umuhimu wa kurudisha matumaini kwa wafadhili na wawekezaji wa kigeni kuhusu uchumi wa Tunisia. Kuhusu mzozo wa kiafya, Abassi amewaomba "Marafiki" wa Tunisia kusaidia juhudi za kupambana na mripuko wa janga la Virusi vya Korona, akikisitiza kuhusu umuhimu wa kampeni ya chanjo kuwa ni kipaumbele kikuu. [Chanzo: Tunis Afrique Press]
Bila aibu Amerika inaitumia IMF kuzitawala nchi nyengine. Kuhusu Tunisia, Amerika inafahamu kwamba nchi hiyo ipo katika mzozo wa kisiasa na bila shaka Washington itaitumia IMF kama chambo kwa ajili ya kuweka mfumo wa kisiasa ambao utaendana na maslahi yake zaidi.
Serikali ya Afghan Yakumbana na 'Hali ya Sintofahamu'
Serikali ya Afghan jijini Kabul itapigana kufa kupona na huenda ikaanguka kwa Taliban baada ya Amerika kukamilisha kujiondoa kwake katika nchi hiyo mwezi Agosti, kwa mujibu wa waangalizi wa serikali ya Amerika wanaofwatilia matukio moja kwa moja. Mbali na tathmini nyingi nyingi za maonyo zilizofanywa na viongozi wa juu wa Amerika na wa Afghan, ripoti mpya kutoka Mkaguzi Mkuu wa Ujenzi Mpya wa Afghanistan (SIGAR) imeelezea hali hiyo kama “hali mbaya” na kuonyesha wasiwasi kuwa vikosi vya usalama vya Afghan havipotayari kuzuia upinzani mkali. "Ni dhahiri kuwa muondoko jumla sio mzuri kwa serikali ya Afghan, ambayo huenda ikakumbana na hali ya sintofahamu iwapo hautashughulikiwa na kugeuzwa," Inspekta Mkuu Maalumu John Sopko aliandika katika ripoti, iliyotolewa mnamo siku ya jumatano. “ANDSF [Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Kitaifa vya Afghanistan] vimechukua tena baadhi ya wilaya na serikali ya Afghan bado inashikilia makao makuu ya mikoa yote 34, ikiwemo Kabul,” aliongezea. “Lakini kutoka kwa ripoti ya umma, ANDSF inaonekana kushangazwa na kutokuwa tayari, na hivi sasa inachechemea.” Tangu raisi wa Amerika Joe Biden kutangaza mwezi Aprili kwamba vikosi vya nchi yake vitaondoka Afghanistan, maafisa wamekuwa waangalifu katika kutaja madhara yatakayoipata serikali ya Afghan. Mnamo Jumapili hii iliyopita tu, kamanda wa komandi kuu ya Amerika, Jenerali Kenneth “Frank” McKenzie, amewaaambia waandishi wa habari jijini Kabul kwamba serikali ya Afghan “inakutana na jaribio kali kabisa.” lakini akaongezea kwamba mbali na jaribio la Taliban kutengeneza hali ya kutokuwa na budi, “hakuna hatma ya wazi katika mapigano haya.” [Chanzo: Voice of America]
Imekuwa ni machungu ya wazi kwa Amerika kuiruhusu Taliban kupata udhibiti zaidi kabla ya suluhu yoyote ya kisiasa. Kuongezea hili, ni ahadi ya Taliban ya kutoitumia Afghanistan kuzihujumu nchi kama China na dola za Asia ya kati, katika hali hii, mtu anaweza kuiona michoro ya suluhu ya kisiasa ikijitokeza. Kufikia hapa, ni muhimu kwa Taliba kuwa werevu kisiasa na kutohadaiwa na mipango ya Amerika ya kuitumia Afghanistan siku za usoni.
Amerika na China Zasema Zataka Kuepuka Mzozo wa Kijeshi, Lakini Hazijaafikana Namna ya Kuuepuka
Pamoja na mikwaruzano na kushutumiana, wanadiplomasia wa Amerika na China walikutana katika mji wa pwani wa Tianjin mapema wiki hii: hakuna anayetaka kuona uhusiano mkubwa zaidi wa duniani ukidorora na kuwa mzozo wa kijeshi. Lakini kulikuwa na itifaki chache juu ya nija imara ya kuepuka janga hili. Na hiyo imewatia hofu wataalamu. Washington na Beijing zimejikuta katika mkwamo wa hasira na kushutumiana kwa miaka kadhaa, lakini hali imekuwa mbaya zaidi tangu mwanzo wa mripuko wa janga la Virusi vya Korona, ikipelekea kunyoosheana vidole kuhusu wapi Virusi hivi vilipoanzia. Mikutano baina ya pande mbili hizi ni michache na iko mbali mbali kati yake baina - na lini itafanyika, mfano ni ule uliofanyika Alaska mwezi Machi, ulikuwa umejaa chuki na kushambuliana. Amerika haina balozi Beijing. Hakuna hatua yoyote ya kufufua uwakilishi wa Amerika uliopo Chengdu au uwakilishi wa China uliopo Houston. Na uteuzi wa balozi mpya wa China nchini Amerika, mbali na kuwa ni hatua nzuri, hatarajiwi kuwa itapunguza taharuki hizo kwa muda mfupi. Kwa sasa uhasama uliopo ni mkubwa kati ya pande hizi mbili. Kubwa linalotawala ni juu ya Taiwan na uwezekano wa kutumika nguvu za kijeshi katika bahari ya kusini mwa China pamoja na athari zipatikanazo kwa pande zote mbili. Wakizungumza huko Tianjin, pande zote zilisema licha ya hali ya sasa ya mahusiano, zinahitaji kujiepusha na makabiliano ya moja kwa moja. Naibu Waziri wa Kigeni wa Amerika Wendy Sherman ametilia mkazo kwamba huku Washington ikikaribisha "Mchuano mgumu," haitafuti mzozo na Beijing. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China Xie Feng alimwambia Sherman watu wa China "wanapendelea zaidi amani." [Chanzo: CNN]
Hakuna uwezekani wa kuwa na vita. Mkakati wa Amerika ni kuidhibiti China kupitia njia za kidiplomasia. Ama China, Beijing iko tayari kuutoboa udhibiti huu kupitia miungano na mikataba ya pande mbili ambayo kimsingi inaangazia biashara.