- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa Vya Habari 04/08/2021
Vichwa vya habari:
Amerika Yaongoza Mashambulizi ya Anga dhidi ya Taliban
Bei ya Mkate Yaongezeka nchini Misri
Uingereza Ipo Upande Wako, Boris Johnson Amwambia Kiongozi wa Upinzani wa Belarus
Maelezo:
Amerika Yaongoza Mashambulizi ya Anga dhidi ya Taliban
Katika kukabiliana na mafanikio ya hivi karibuni ya Taliban kuichukua miji mikubwa ya Afghanistan, Amerika imefanya mfululizo wa mashambulizi, yanayooneka kutoa matumaini ya kupunguza mashambulizi na kutoa muda kwa serikali ya Afghan kujibu mashambulizi hayo. Taliban imekuwa ikipata mafanikio katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu katika miji mikuu ya mikoa. Mashambulizi ya anga ya Amerika yanashambulia maeneo hayo, yakilenga zaidi Herat, Kandahar, na Lashkar Gah, ambayo maafisa wameiita ni miji iliyo “hatarini mno”. Hadi sasa, mashambulizi hayo hayajafanikiwa kuwazuia Taliban kuingia katika miji, au kushindania udhibiti pamoja nao. Yote haya yanajiri kufatia makubaliano kati ya Taliban na Amerika yaliyofanyika mwezi Aprili iliyopita.
Misri Kupandisha Bei ya Mkate
Mnamo siku ya Jumanne Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi alisema ilikuwa ni "muhimu" kupandisha bei ya ya mkate uliopewa ruzuku nchini. Wamisri milioni sitini ni sehemu ya mpango maalumu wa ruzuku ya mkate na hutengewa mikate mitano kwa siku, na kila mkate mmoja hugharimu pauni 0.05 za Misri sawa na dolari (0.0032). Wakati wa ufunguzi wa miundombinu ya uzalishaji wa chakula, Sisi hakuweka wazi ni kwa kiwango gani gharama zitaongezeka lakini akalalamikia bei. "Muda umefika sasa wa kuongeza bei ya mikate ya senti (Piaster) tano... ni ajabu kuuza mikate 20 kwa bei ya sigara," alisema Sisi. Misri ndio nchi inayoagiza ngano kwa wingi duniani, na mkate umekuwa ni kadhia msingi katika nchi hii. Karibu miaka mitano iliyopita, maandamano ya hasira yaliripuka nchi nzima baada ya serikali kukata ruzuku ya mkate ili kupambana na mgogoro wa kuichumi. IMF imefanya kuondolewa kwa ruzuku hiyo kama sharti la Misri kupokea misaada wowote zaidi wa kifedha. Tangu Sisi na jeshi kuchukua hatamu za utawala mnamo 2013 serikali hiyo ya kijeshi imeirudisha nchi chini na kama walivyokuwa watangulizi wake utawala huo unatumia mkono wa chuma kudumisha utangamano wowote.
Uingereza Ipo Upande Wako, Boris Johnson Amwambia Kiongozi wa Upinznani wa Belarus
Uingereza ipo upande wa viongozi wa upinzani wa watu wa Belarus wanaojaribu kuangusha utawala dhalimu unaoongozwa na Alexander Lukashenko, Boris Johnson alisema. Waziri Mkuu huyo alithibitisha uungaji mkono wake kwa Sviatlana Tsikhanouskaya, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kurudisha demokrasia katika jamii iliyovurugika katika nchi hiyo iliyopo Mashariki ya Ulaya. Akiwa mwenyeji wa Tsikhanouskaya katika makao yake ya Downing Street masaa machache baada kiongozi wa kundi moja linalowasaidia Wabelarus kukimbia mateso kukutwa amekufa katika bustani moja mjini Kyiv, mji mkuu wa Ukraine, Johnson alisema Uingereza ipo nyuma ya mapambano ya Tsikhanouskaya dhidi ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu na kuuliwa kwa wanaharakati wa demokrasia. “tupo upande wako sana, tukisaidia kile unachofanya. Tumejizatiti kusaidia haki za binadamu na haki za raia wa Belarus,” alimwambia mnamo siku ya Jumanne. Tsikhanouskaya alitilia mkazo nguvu ya azimio hilo la Johnson la uungaji mkono, amesema ilikuwa “muhimu mnamo kufahamu kwamba moja ya nchi zenye nguvu zaidi duniani inaunga mkono Belarus”. Tangu uchaguzi wa 2020 ambao wengi nchini Belarus waliushuku, upinzani umekuwa ukitafuta uungaji mkono wa kigeni ili kumuangusha rais anayeungwa mkono na Urusi. Belarus ni moja ya mataifa machache yanayoegemea upande wa Urusi.