Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 10/07/2021

Vichwa Vya Habari:

• Taliban Yasema Inadhibiti Asilimia 85 ya Afghanistan

• Waziri wa Kigeni wa China Kuzuru Asia ya Kati kwa Misheni ya SCO ya Amani ya Afghanistan

• Amerika Yasema Maslahi Yake ya pamoja na Pakistan Yanakwenda Mbali zaidi ya Afghanistan

Maelezo:

Taliban Yasema Inadhibiti Asilimia 85 ya Afghanistan

Maafisa wa Taliban mnamo siku ya Ijumaa walisema kuwa kundi hilo la wanamgambo limechukua udhibiti wa asilimia 85 ya eneo la Afghanistan, na wasiwasi wa kimataifa unaongezeka juu ya kupata madawa na usambazaji wake nchi humo. Maafisa wa Serikali ya Afghanistan wameyataja madai kuwa Taliban inadhibiti sehemu kubwa ya nchi kama sehemu ya kampeni ya propaganda iliyozinduliwa na wanajeshi wa kigeni, wakiwemo wale wa Amerika, kujiondoa baada ya miaka 20 ya vita. Vilevile, maafisa wa ndani wa Afghanistan walisema wapiganaji wa Taliban, wakipata ujasiri kwa kujiondoa huko, wameikamata wilaya moja muhimu katika mkoa wa Herat, nyumbani kwa maelfu ya Mashia wa Hazaras walio wachache. Torghundi, mji wa uliopo kasakazini katika mpaka na Turkmenistan, pia ulichukuliwa Taliban kwa usiku mmoja, maafisa wa Afghanistan na Taliban walisema. Mamia ya majeshi ya usalama ya Afghanistan na wakimbizi wanaendelea kukimbia kwenda katika mipaka ya Nchi jirani za Iran na Tajikistan, ikisababisha taharuki jijini Moscow na katika miji mikuu mingine ya kigeni ikihofiwa kundi hilo la itikadi kali huenda likapenya Asia ya Kati. Maafisa wa tatu wa Taliban waliokuwa ziarani jijini Moscow walitaka kuzungumzia wasiwasi huo. “Tutachukua hatua zote ili (wanamgambo) Dola ya Kiislamu (kundi) lisiendeshe shughuli zake katika eneo la Afghanistan... na eneo letu kamwe halitotumiwa dhidi ya majirani zetu,” mmoja wa maafisa hao wa Taliban, Shahabuddin Delawar, aliuambia mkutano mmoja wa wanahabari. Alisema, “nyinyi na jamii nzima ya ulimwengu pengine hivi karibuni mumepata habari kwamba asilimia 85 ya eneo la Afghanistan lipo chini ya udhibiti” wa Taliban. Ujumbe huo huo ulisema siku moja kabla kwamba kundi hilo halitashambulia mpaka kati ya Tajikistan na Afghanistan, hatma ambayo inaangaziwa na Urusi pamoja na Asia ya Kati. Alipoulizwa Taliban inashikilia kiasi gani cha eneo la ardhi, Msemaji wa Pentagon John Kirby alikataa kutoa jibu la moja kwa moja. “kushukilia mipaka au ardhi haimaanishi unaweza kuimudu au kuidumisha kwa muda wote” alisema alipokuwa anahojiwa na CNN. “Na hivyo nadhani ni wakati sasa kwa vikosi vya Afghan kuingia uwanjani - na tayari wapo uwanjani - na kuihami nchi yao, watu wao.” “Wanao uwezo, wanazo nguvu. Sasa ni muda wa kuwa na azma,” alisema. [chanzo: The Dawn]

Ni wazi kwamba chaguo pekee la makusudi walilonalo Amerika ni kuutumia usengeaji wa haraka wa Taliban kuunda muungano mpana ili kusitisha maendeleo ya Taliban. Hivyo, kuwepo usisitizaji wa Kirby pamoja na Biden kuunganisha kwa vikosi  pinzani vya Afghan na kutumia uweo wa jeshi la Afghan kuidhibiti Taliban. Kwa kutumia njia hii, Amerika inataraji kutumia “uimara wa ndani” ili kufikia mpango wa amani. Lakini, chaguo hilo kiasi fulani ni hatari kwani inaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu kama vilivyotokea  miaka ya tisiini.

Waziri wa Kigeni wa China Kuzuru Asia ya Kati kwa Misheni ya SCO ya Amani ya Afghanistan

Huku tishio la kiusalama la kujiondoa kwa haraka Amerika kutoka Afghanistan likienea katika nchi jirani, waziri wa mambo ya kigeni wa China amepanga ziara ya nchi tatu za Asia ya Kati kutokana na mualiko maalumu, na atajadiliana pamoja na maafisa kutoka Shirika la Shanghai Cooperation Organization (SCO) kuhusu hali nchini Afghanistan. Licha ya kukorogwa na hali mapya ya Afghanistan, linazisukuma nchi za kanda hiyo ikiwa ni pamoja na China, kuifuatilia kwa ukaribu. Wachambuzi wanasema kuna changamoto pamoja na fursa kwa China katika hali ya Afghanistan. Kupitia kuijumuisha kadhia ya Afghanistan katika ajenda za SCO, hakutasidia tu Beijing kudhibiti zaidi ghasia zilizoachwa na ombwe la mamlaka katika nchi hii, lakini pia litasukuma mafungamano kati ya China na nchi nyingine za Asia ya Kati kuwa karibu zaidi, walitambua. Diwani wa Serikali ya China na Waziri wa Kigeni Wang Yi atazuru Turkmenistan, Tajikistan, na  Uzbekistan kati ya  Julai 12 na 16 kufatia mualiko wa Mawaziri watatu wa mambo ya kigeni katika nchi hizo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni wa China Wang Wenbin alitangaza hilo mnamo siku ya ijumaa. Pia Wang Yi alipangiwa kuhudhuria kwenye mkutano wa kundi la mawasiliano la mawaziri wa mambo ya kigeni wa SCO-Afghanistan, ambapo watabadilishana mawazo na wanachama wengine wa SCO pamoja na upande wa Afghan kuhusu kuimarisha usalama wa kanda na utulivu, sambamba na kuendeleza shughuli za Amani na upatanisho wa Afghanistan,na kuongeza ushirikiano katika ya SCO na Afghanistan, Wang Wenbin alisema. "uzembe na pupa" ya Amerika katika kujiondoa Afghanistan kumepelekea kuongezeka kwa tishio la kiusalama nchi humo, na hali ya kukosekana utulivu imeanza kusambaa katika kanda nzima, Qian Feng, mkurugenzi wa idara ya uchunguzi katika taasisi ya mikakati ya Chuo Kikuu cha Tsinghua, aliiambia  Global Times. Katika hali hii, nchi za kanda zimeigeukia China, zikitumai kwamba itaunda umoja wa kimkakati kwa ajili ya kushughulika na jambo hili, hayo ni kulingana na Qian. Lakini wachambuzi wangali wanasema kwamba China itakuwa makini sana katika kushughulikia jambo hili, na sio kuruka ndani ya ombwe  la mamlaka lilioachwa na Amerika. "Hatutaingilia, hatuta jaribu kuichukua nchi, bali tutaipa misaada inayohitaji," alisema Qian. Mnamo alhamisi Rais Joe Biden alitetea uamuzi wa Amerika wa kujiondoa kutoka Afghanistan huku hatari ya nchi kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ikizidi kuongezeka. Alisema kwamba lengo la jeshi la Amerika kuwepo pale lilifikiwa tangu tarehe 31 Agosti, mapema kabisa kuliko ilivyotangazwa mwanzo. [chanzo: Global Times]

China inaogopa zaidi Uislamu kusambaa Asia ya Kati kuliko inavyo hofia ombwe la kiusalama lililosababishwa na kujiondoa kwa Amerika. Kinaya ni kwamba, Amerika ilizitumia nchi za Kiislamu - Pakistan, Afghanistan, Saudi Arabia na Iran - ili kuharakisha kuporomoka kwa Muungano wa Kisovieti. Kujiondoa kwa haraka kwa Amerika kunalipa sifa chaguo jengine kuzingatiwa na Washington nalo ni kudhibiti wakati huo huo kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu nchini Afghanistan na kuhamisha machafuko hadi Asia ya kati na hivyo kupelekea hali ya kutokuwa na utulivu Urusi katika mipaka ya Urusi na China.

Amerika Yasema Maslahi Yake ya pamoja na Pakistan Yanakwenda Mbali zaidi ya Afghanistan

Huku Amerika ikiitambua Pakistan kama "msaidizi muhimu na wa maana" inapokuja suala la Afghanistan, maslahi ya pande zote mbili yamekwenda mbali zaidi hapo, Redio ya Pakistan ilimnukuu msemaji wa Wizara ya Kigeni ya Amerika Ned Price akisema katika kikao kifupi na waandishi wa habari mnamo siku ya Alhamisi. Aliongezea kwamba Amerika na Pakistan zimekuwa na maslahi ya pamoja kuhusu Amani na utulivu wa Afghanistan, na "juhudi zetu za pamoja zitaleta Amani na usalama huko." Lakini, Price alisema, maslahi hayo ya pamoja ya Amerika na Pakistan yamekwenda mbali zaidi ya Afghanistan na yanajumuisha mipango na hatua pana za kupambana na ugaidi na kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano ya watu kwa watu.

"Pakistan ni mshirika muhimu katika rubaa nyingi," alisema. Msemaji huyo wa Wizara ya Kigeni alisisitiza kwamba majirani wote wa Afghanistan wanahitajika kuwajibika kwa pamoja kwa ajili ya "utulivu wa kudumu wa kisiasa [katika nchi] na kusitisha mapigano [kati ya serikali ya Afghan na Taliban]." Aliongezea kwamba Amerika itahakikisha kwamba majirani wote wa Afghanistan wamecheza dori ya manufaa kwa nchi hiyo. Matamshi ya Price yamejiri wakati ambapo kujitoa kwa Amerika kutoka Afghanistan kuko katika hatua za mwisho na nchi ipo katika ukingo wa kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ikizama katika machafuko kutokana na mashambulizi ya Taliban. Hali iliyopo kuna uwezekano wa kupekelea kutizama upya mafungamano kati ya Pakistan na Amerika, ambapo ilikuwa dhahiri wakati Waziri Mkuu Khan waziwazi alipotumbilia mbali uwezekano wa kurusu Amerika kuwa na kambi yoyote ya kijeshi na kulitumia eneo lake kwa hatua ya aina yoyote ndani ya Afghanistan. "Hatuwezi kuruhusu hilo. Hatuwezi kabisa kuruhusu kambi yoyote, au hatua yoyote kutokea eneo la Pakistan kwenda Afghanistan.”

“Kamwe haiwezekani. Waziri Mkuu huyo aliiambia Axios kupitia HBO katika mahojiano mwezi uliopita. Aliyasema hayo hayo alipohojiwa na Washington Post akisema kwamba: "Hili hatuwezi kulimudu. Tumeshalipa gharama kubwa mno. Wakati huo huo, endapo Amerika, nchi yenye nguvu kubwa zaidi katika historia, haikuweza kushinda vita ndani ya Afghanistan baada ya miaka 20, itaweza vipi kufanya hilo kutoka katika kambi zilizoko katika nchi yetu?" [chanzo: The Dawn]

Khan anafahamu vizuri kwamba Amerika—dola kuu ya kipekee duniani imeshindwa vibaya nchini Afghanistan. Lakini badala ajipe nguvu kupitia ukweli huu na afanyekazi na Taliban kuiunganisha Afghanistan na kuunda wasaa muhimu kumaliza uingiliaji wa Magharibi, Khan anaendelea kulalamikia kuhusu shinikizo la Magharibi. Chini ya Khilafah Rashidah, Pakistan itaiunganisha Afghanistan na dola zote tano muhimu za Asia ya Kati ili kumaliza kwa kudumu uingiliaji wa Magharibi na Mashariki katika kanda hii.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu