Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 13/10/2021

Vichwa vya Habari:

• Msaada wa Kibinadamu kwa Afghanistan

• Mazungumzo kati ya Amerika na Urusi

Maelezo:

Msaada wa Kibinadamu kwa Afghanistan

Amerika imekubali kutoa misaada ya kibinadamu kwa Afghanistan iliyo ukingoni mwa janga la kiuchumi, huku ikikataa kutoa utambuzi wa kisiasa kwa watawala wapya wa nchi hiyo. Taliban imesema mazungumzo yaliyofanyika jijini Doha, Qatar, "yalikwenda vizuri," huku Washington ikitoa misaada ya kibinadamu kwa Afghanistan baada ya kukubali kutounasibisha msaada huo na kutambuliwa rasmi kwa Taliban. Taarifa ya Amerika ilikuwa na ufafanuzi machache, ikisema tu kwamba pande hizo mbili "zilijadili utoaji wa msaada  mkubwa wa kibinadamu wa Amerika, moja kwa moja kwa watu wa Afghanistan." Amerika iliweka wazi kuwa mazungumzo hayo hayakuwa njia yoyote ya utangulizi wa kutambuliwa kwa Taliban, ambao waliingia madarakani Agosti 15 baada ya serikali ya washirika wa Amerika kuporomoka. Msemaji wa Wizara ya Kigeni Ned Price aliyaita majadiliano hayo "yaliowazi na ya kitaalam," huku upande wa Amerika ukisisitiza kwamba Taliban watahukumiwa kwa vitendo vyao, sio maneno yao tu. "Ujumbe wa Amerika ulizingatia wasiwasi wa usalama na ugaidi na upitaji salama kwa raia wa Amerika, raia wengine wa kigeni na washirika wetu wa Afghani, na pia juu ya haki za binadamu, ikiwemo ushiriki wa kihakika wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za jamii ya Afghanistan," alisema katika taarifa moja. Huku Amerika ikipasha misuli na Taliban hii kihakika ni kuwaweka kwenye uongozi mfupi, Amerika imekuwa ikijadiliana na Taliban kwa zaidi ya muongo mmoja na kutia saini mkataba wa amani nao. Iliwafungulia njia ya kuchukua mamlaka mnamo Agosti lakini sasa inajaribu kuwasilisha picha ya taifa ambalo lina uhusiano wa kimasharti na Taliban.

Mazungumzo kati ya Amerika na Urusi

Mahusiano kati ya Urusi na Amerika huenda yakawa mabaya zaidi kufuatia mazungumzo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili ambayo yanaleta maendeleo machache kuliko ilivyotarajiwa hapo awali, Naibu Waziri wa Kigeni wa Moscow Sergey Ryabkov amesema. Hukumu hiyo inajiri baada ya Naibu Waziri wa Kigeni wa Amerika Victoria Nuland kuwasili nchini humo mnamo Jumatatu kufanya mazungumzo ya siku tatu na maafisa wa Urusi. Mnamo siku ya Jumanne, vyombo vya habari vya ndani ya nchini viliripoti kuwa mazungumzo kati ya Nuland na Ryabkov yalikuwa yanaporomoka huku wanadiplomasia hao wakipapambana kupata msingi wa pamoja. Mapema wiki hii, Moscow iliondoa vikwazo kwa Nuland, ambayo ilimruhusu waziri huyo mdogo wa kigeni wa Amerika kuingia nchini humo kwa ajili ya mkutano na wenzake wa Urusi. Wakati mazungumzo yangali yanaendelea, Ryabkov amesema kuwa Moscow haitaki taharuki kati ya Urusi na Amerika kuongezeka zaidi na kuomba vizuizi vya kimataifa viondolewe. Uangalifu hasa uliwekwa katika maswala yanayohusu misheni za Urusi na Amerika kwenye maeneo ya kila mmoja. Upande wa Urusi ulisisitiza kuwa vitendo vya uhasama dhidi ya Urusi havitabaki bila kujibiwa, lakini Moscow haitafuti kuongezeka zaidi. "Tunapendekeza kuondoa vizuizi vyote vilivyoletwa na pande zote mbili katika miaka michache iliyopita," alisema. Imekuwa kawaida kwa Amerika kushinikiza maafisa kutoka mataifa mengine ili kuwapa ofa ambayo hawawezi kuikataa. Amerika ilifanya hivi kwa Urusi nchini Syria na sasa Amerika inataka Urusi ifanye kazi nayo katika mkakati wake kwa China kwa kuipatia Kremlin nafasi katika kadhia za kiulimwengu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu