Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 02/09/2022

Vichwa vya Habari:

  • Shirika la Intel la Ufaransa Kufuatilia Waislamu Juu ya mitazamo yao ya Kisiasa
  • Mafuriko Makali ya Pakistan Yaunda Ziwa Kubwa lenye upana wa kilomita 100 ndani ya Nchi, Picha za Satelaiti Zaonyesha
  • Marekani Yazuia Mauzo ya Baadhi ya Al Chips kwenda China huku Msako wa Teknolojia Ukizidi Kupamba Moto

Maelezo:

Shirika la Intel la Ufaransa Kufuatilia Waislamu Juu ya maoni yao ya Kisiasa

Idara ya upelelezi ya nchi ya Ufaransa imetayarisha faili za Waislamu wengi kwa kueleza uungaji mkono wao wa Jean-Luc Melenchon, kiongozi wa chama cha La France Insoumise, ambaye alionyesha upinzani dhidi ya chuki dhidi ya Waislamu, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari. Waislamu kadhaa wa Ufaransa wamefuatiliwa na kuorodheshwa na ujasusi wa Ufaransa kwa maoni yao ya kisiasa. Hili lilifichuliwa katika makala yaliyochapishwa mnamo Jumanne na kituo cha redio cha Europe 1, kikiripoti kwamba kimepata "barua ya siri kutoka kwa ujasusi wa Ufaransa." Kulingana na European 1, waraka huu "ulisambazwa kwa maafisa wachache wakuu, wanachama wa serikali, na hadi Elysee," baada ya kuandikwa katikati ya Mei, wiki tatu baada ya uchaguzi wa marudio wa rais ambao ulipiga muhuri ushindi wa Rais aliyeko mamlakani Emmanuel Macron. Kulingana na maelezo yaliyonukuliwa na vyombo vya habari, ujasusi wa nchi hiyo ulifikia hitimisho kwamba mgombea urais wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon, aliondolewa katika duru ya kwanza ya upigaji kura baada ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Macron na Marine Le Pen wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen, angefurahia "kura za Waislamu" nchini humo kutokana na kuungwa mkono na wale wanaoitwa "washawishi na wanaharakati wa Kiislamu" ambao "walikaribisha" na "kuwasilisha" "misimamo" yake. Imewataja Waislamu wengi nchini Ufaransa, ikiwemo wakili Rafik Chekkat, mwanachama wa chama cha Agir contre l'islamophobie (Hatua Dhidi ya Chuki dhidi ya Uislamu - ACI) na mwandishi wa habari huru Siham Assbague, ambao wote walitajwa kama "Wanaharakati wa Kiislamu," hasa kwa kuchukua msimamo dhidi ya chuki dhidi ya Waislamu au ukoloni. Mbali na Chekkat na Assbague, barua hiyo pia inawahusu Vincent Souleymane, Hani Ramadan, na Farid Slim, wote wanatajwa kama "wahubiri" au "maimamu" kutoka Ikhwan Muslimin. [Chanzo: TRT]

Ufaransa kama nchi nyingine za Magharibi ina mashaka makubwa na idadi ya Waislamu wake na haiwaamini Waislamu. Katika hali hii, Ufaransa ina wasiwasi kuhusu jinsi viongozi wa Waislamu wanaweza kuwashawishi Waislamu katika kura zao na kuhujumu mfumo wa kiliberali ulioenea unaopendekezwa na kipote cha warasilimali.

Mafuriko Makali ya Pakistan Yaunda Ziwa Kubwa lenye upana wa kilomita 100 ndani ya Nchi, Picha za Satelaiti Zaonyesha

Picha mpya za satelaiti zinazofichua kiwango cha rekodi ya mafuriko nchini Pakistan zinaonyesha jinsi Mto Indus uliofurika umegeuza sehemu ya Mkoa wa Sindh kuwa ziwa lenye upana wa kilomita 100 ndani ya nchi. Maeneo ya nchi kwa sasa yapo chini ya maji, baada ya kile maafisa wa Umoja wa Mataifa wamekitaja kuwa "monsoon on steroids" kuleta mvua kubwa zaidi katika kumbukumbu ya maisha na mafuriko ambayo yameua watu 1,162, kujeruhi 3,554 na kuathiri milioni 33 tangu katikati ya Juni. Picha mpya, zilizopigwa Agosti 28 kutoka kwa kihisia cha setilaiti cha MODIS cha NASA, zinaonyesha jinsi mchanganyiko wa mvua kubwa na Mto Indus uliofurika ulivyojaza sehemu kubwa ya mkoa wa Sindh Kusini. Katikati ya picha, eneo kubwa la rangi ya samawati iliyokolea linaonyesha Mto Indus ukifurika na kumwaika eneo la karibu kilomita 100 (maili 62) kwa upana, na kuyageuza yaliyokuwa mashamba ya kilimo kuwa ziwa kubwa la ndani. Ni mabadiliko ya kushangaza kutokana na picha iliyopigwa na satelaiti hiyo hiyo tarehe kama hiyo hiyo mwaka jana, ambayo inaonyesha mto huo na vijito vyake vilivyomo katika kile kinachoonekana kwa kulinganisha na bendi ndogo, nyembamba, ikionyesha kiwango cha uharibifu katika moja maeneo ya nchi yaliyoathirika zaidi. Mvua za masika za mwaka huu tayari ndizo mvua nyingi zaidi nchini tangu rekodi zilipoanza mwaka wa 1961, kulingana na Idara ya Hali ya Hewa ya Pakistan, na msimu bado ungali umebakia mwezi mmoja. Katika majimbo yote ya Sindh na Balochistan, mvua imekuwa 500% juu ya wastani, ikikumba vijiji na mashamba yote, ikiharibu majengo na kuangamiza mazao. Katika mahojiano na CNN Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardari alisema alitembelea Sindh na kujionea jinsi mafuriko yalivyosababisha watu katika vijiji na miji yote kuhama makaazi. "Ni vigumu kupata ardhi kavu. Kiwango cha janga hili ... watu milioni 33, hiyo ni zaidi ya wakaazi wa Sri Lanka au Australia," alisema. "Na ingawa tunaelewa kuwa uhalisia mpya wa mabadiliko ya tabianchi unamaanisha hali mbaya zaidi ya hewa, au mvua za masika, mawimbi ya joto kali zaidi kama tulivyoona mapema mwaka huu, kiwango cha mafuriko ya sasa ni ya hali mbaya zaidi. Hakika tunatumai huu sio uhalisia mpya wa tabianchi." [Chanzo: CNN]

Licha ya mafuriko kuwa ya viwango vya janga uzembe wa uongozi wa kiraia na kijeshi hauwezi kufichwa chini ya zulia. Pakistan kwa jiografia yake inakabiliwa na matetemeko ya ardhi na mafuriko, na mamlaka zimekuwa na miongo kadhaa kuandaa kukabiliana kwao na dharura ya maafa na pia kutatua athari za mabadiliko ya tabianchi. Lakini inaonekana kana kwamba mamlaka hazijafanya lolote tangu mafuriko makubwa ya mwisho ya mwaka 2010, na sasa zinang’ang’ana kukabiliana nayo. Kinachotakiwa ni uongozi wa dhati utakaoweka maslahi ya wananchi mbele kuliko maslahi binafsi ya tabaka tawala.

Marekani Yazuia Mauzo ya Baadhi ya Al Chips kwenda China huku Msako wa Teknolojia Ukizidi Kupamba Moto

Kupigwa marufuku kwa mauzo ya Nvidia na AMD kunaashiria ongezeko kubwa la juhudi za Marekani za kudhibiti uwezo wa teknolojia ya kijeshi ya China huku taharuki zikizidi kutanda Taiwan, mtengezaji wa Chip Nvidia ilisema kuwa maafisa wa Marekani waliiambia ikome kusafirisha chips mbili za juu za kompyuta kwa kazi ya kijasusi kwa China, hatua ambayo inaweza kulemaza uwezo wa makampuni ya Kichina kufanya kazi ya juu kama utambuzi wa picha. Kampuni hiyo Jumatano ilisema marufuku hiyo, ambayo inaathiri chipsi zake za A100 na H100 zilizoundwa ili kuharakisha kazi za kujifunza kwa mashini, inaweza kuvuruga ukamilishaji wa utengenezaji H100, chip kuu ya Nvidia ilitangaza mwaka huu. Nvidia ilisema maafisa wa Amerika waliiambia sheria hiyo mpya "itashughulikia hatari kwamba bidhaa zilizofunikwa zinaweza kutumika, au kuelekezwa, 'matumizi ya mwisho ya kijeshi' au 'mtumiaji wa mwisho wa kijeshi' nchini China." Ilipoulizwa maoni, idara ya Biashara ya Amerika haikusema ni vigezo gani vipya imeweka kwa chips za AI ambazo haziwezi kusafirishwa tena kwenda China lakini ilisema inahakiki sera na utekelezaji wake unaohusiana na China "kuondoa teknolojia ya hali ya juu kutoka kwa mikono ya kimakosa." Ingawa hatuko katika nafasi ya kuelezea mabadiliko maalum ya sera kwa wakati huu, tunachukua mbinu ya kina kutekeleza hatua za ziada zinazohitajika zinazohusiana na teknolojia, matumizi ya mwisho, na watumiaji wa mwisho ili kulinda usalama wa kitaifa wa Marekani na maslahi ya sera ya kigeni,” msemaji mmoja aliiambia Reuters. Tangazo hilo linaashiria ongezeko kubwa la msako wa Marekani dhidi ya uwezo wa kiteknolojia wa China huku taharuki zikiibuka juu ya hatma ya Taiwan, ambako chips za Nvidia na karibu kila kampuni nyingine kuu ya chip zinatengenezwa. Msemaji mmoja wa hasimu AMD aliiambia Reuters kuwa kampuni hiyo imepokea masharti mapya ya leseni ambayo yatazuia chips zake za kijasusi za MI250 kusafirishwa kwenda China, lakini inaamini kuwa chipsi zake za MI100 hazitaathirika. Bila chips za Kimarekani kutoka kwa makampuni kama vile Nvidia na AMD, mashirika ya Kichina hayataweza kutekeleza kwa gharama nafuu utengezaji kompyuta wa hali ya juu unaotumika kwa utambuzi wa picha na maneno, kati ya kazi zengine nyingi. Utambuzi wa picha na usindikaji wa lugha asilia ni kawaida katika programu za watumiaji kama vile simu mahiri (smart phones) zinazoweza kujibu maswali na kupachika picha. Pia zina matumizi ya kijeshi kama vile kupekua picha za satelaiti kwa ajili ya silaha au kambi za kijeshi na kuchuja mawasiliano ya kidijitali kwa madhumuni ya kukusanya taarifa za kijasusi. [Chanzo: The Guardian]

Vita vya teknolojia vilivyoanzishwa na Rais Trump vinaendelea bila kusitishwa chini ya utawala wa Biden. Amerika inafanya kila iwezalo kupunguza kasi ya maendeleo ya kiteknolojia na kijeshi ya China, haswa katika maeneo yanayohusishwa na semiconductors zinazounga mkono AI kwa matumizi ya kijeshi. Njia pekee ya China ni kuunda safu yake huru, ikanzia utengenezaji wa chips za hali ya juu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu