- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari: 19/10/2022
Vichwa vya Habari:
• Blinken Adai China Yataka Kuichukua Taiwan
• Marubani wa Zamani wa Uingereza Washawishiwa Kulisaidia Jeshi la China
• Xi Afungua Bunge la Kitaifa la Congress
Maelezo:
Blinken Adai China Yataka Kuichukua Taiwan
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken mnamo Jumanne alidai kuwa China inatazamia kuichukua Taiwan "katika ratiba ya matukio ya haraka zaidi" na kuituhumu Beijing kwa kutaka kubadilisha hali iliyopo katika Mlango wa Bahari wa Taiwan. Blinken hakutoa ushahidi wa madai hayo lakini alisisitiza kwamba "kumekuwa na mabadiliko katika mbinu kutoka Beijing kuelekea Taiwan katika miaka ya hivi karibuni." Kumekuwa na ongezeko la shughuli za kijeshi za China pambizoni mwa Taiwan, lakini hilo lilikuja katika majibu ya moja kwa moja kwa Spika wa Bunge Nancy Pelosi (D-CA) na wajumbe wengine wa Congress wanaozuru kisiwa hicho. Rais Xi Jinping wa China alikariri katika Kongamano kuu la CCPs kwamba sera ya Beijing ya kutafuta "kuungana tena kwa amani" na Taiwan lakini hakutoa uamuzi wa matumizi ya nguvu kama chaguo. Xi alionya dhidi ya "uingiliaji kutoka nje" juu ya suala hilo, na maafisa wengine wa China wameonya wazi kwamba msaada zaidi wa Marekani kwa "vikosi vya uhuru" vya Taipei vinaweza kusababisha vita.
Marubani wa Zamani wa Uingereza Washawishiwa Kulisaidia Jeshi la China
Marubani wa zamani wa jeshi la Uingereza wanashawishiwa hadi China kwa pesa nyingi ili kupitisha utaalamu wao kwa jeshi la China, inadaiwa. Hadi marubani 30 wa zamani wa jeshi la Uingereza wanafikiriwa kwenda kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China. Uingereza inatoa tahadhari ya kijasusi kuwaonya marubani wa zamani wa kijeshi dhidi ya kufanya kazi kwa jeshi la China. Juhudi za kuwasaka marubani zinaendelea na zimekuwa zikiongezeka hivi karibuni, maafisa wa Magharibi wanasema. Msemaji mmoja kutoka Wizara ya Ulinzi alisema mafunzo na uajiri wa marubani hayakiuki sheria yoyote ya sasa ya Uingereza lakini maafisa nchini Uingereza na nchi zengine wanajaribu kuzuia shughuli hiyo. "Ni kifurushi chenye faida kubwa ambacho kinatolewa kwa watu," alisema afisa mmoja wa Magharibi, akiongeza kuwa "pesa ndio kichocheo kikubwa". Baadhi ya vifurushi vinafikiriwa kuwa na thamani kama ya £237,911 ($270,000). Marubani hao waliostaafu wa Uingereza wanatumiwa kusaidia kuelewa jinsi ndege na marubani wa nchi za Magharibi zinavyofanya kazi, maelezo ambayo yanaweza kuwa muhimu iwapo kutatokea mzozo wowote, kama vile kuhusu Taiwan. "Wao ni kundi la watu wanaovutia sana kupitisha ujuzi huo," afisa mmoja wa Magharibi alisema. "Inachukua marubani wa Magharibi wenye uzoefu mkubwa kusaidia kukuza mbinu na uwezo wa jeshi la anga la China." Msemaji mmoja wa Waziri Mkuu Liz Truss alisema serikali inachukua "hatua madhubuti" kukomesha uwindaji watu hawa na "kulinda usalama wetu wa kitaifa".
Xi Afungua Kongamano la Kitaifa
Rais wa China Xi Jinping alifungua Kongamano la 20 la Kitaifa la Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa kutoa ripoti ya kazi, ambayo ilisisitiza malengo ya kawaida ya sera ya Xi kwa China. Sehemu kubwa ya ripoti hiyo ililenga katika kuumarisha mfumo huo katika nyanja zote za jamii, ikiwa ni pamoja na sehemu nzima ya kujenga thaqafa ya ujamaa. Ripoti hiyo ya kazi inapendekeza kwamba Chama kizingatie kujenga utamaduni wa utaifa na mfumo unaounga mkono CPC katika elimu, anga ya mtandao, mahakama, burudani, jeshi na kwingineko. Hii inaashiria uhafifu kwa sekta nyingi za viwanda, kwani mfumo utaendelea kupuuza shughuli bora za soko wakati pande hizo mbili zikigongana. Fauka ya hayo, kushikilia madaraka kwa Xi kunaonekana kuwa salama, huku ripoti hiyo ikiambatana kwa karibu na vipaumbele vyake mwenyewe vya kuitawala China katika muongo mmoja uliopita. Ripoti hiyo pia ilidhihirisha mtazamo wa kuzingirwa kwa mambo ya nje na masuala ya ndani, na ilitoa angazo dogo la mageuzi ya kiuchumi. Baada ya muongo mmoja madarakani Xi amejitahidi kukabiliana na masuala ya msingi ya China ya vita vya kibiashara na China, Taiwan na uhamisho kwa mtindo mwingine wa kiuchumi. Xi anaonekana kulenga kudumisha mshiko wake mwenyewe wa madaraka.