- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari 28/10/2022
Vichwa vya Habari:
- Rishi Sunak ndiye Waziri Mkuu wa Kwanza wa Uingereza mwenye asili ya Asian – Lakini huu sio huu Ushindi wa Maendeleo
- Mwanajeshi Mkuu wa Pakistan Atafuta Usawazishaji kati ya Marekani na China kabla ya Kustaafu
- Rais Xi wa China asema Yuko Tayari Kufanya Kazi na Marekani kwa ajili ya Manufaa ya Pamoja
Maelezo:
Rishi Sunak ndiye Waziri Mkuu wa Kwanza wa Uingereza mwenye asili ya Asian – Lakini huu sio huu Ushindi wa Maendeleo
Kwa maana hiyo, kupanda kwa Sunak ni mafanikio makubwa yasiyopingika, iwe unakubaliana na siasa zake au la. Bila kuwa na uwezo wa kudai aina yoyote ya historia ya kuwa mhamiaji mzuri zaidi, Sunak bado amekaidi uwezekano kama mtu wa Asia kufika nafasi ya juu zaidi nchini. Safari yake ni ukumbusho wa jinsi Waingereza weusi na kahawia wanapaswa kupigana dhidi ya mkondo ili kuchukuliwa kwa uzito. Lakini tukiinuka juu ya hila hizi za kisiasa, je kipindi hiki kwa kweli kinatwambia nini kuhusu mahusiano ya rangi nchini Uingereza? Kupanda kwa Sunak kumechoshwa na uchungu - kwa wengi, maoni yake magumu hayawakilishi haswa ni nani tuliyedhani angekuwa kiongozi wa kwanza wa Uingereza aliye na wazazi wahamiaji. Lakini wazazi wa Sunak walipohamia Uingereza kutoka Afrika mashariki katika miaka ya 1960, uteuzi wa waziri mkuu mwenye asili ya Asia haungewezekana. Ilikuwa wakati ambapo madirisha ya maduka ya pembeni yalivunjwa mara kwa mara na wafuasi wa National Front, na hotuba ya Enoch Powell ya "mito ya damu" iliashiria mustakabali mbaya wa wahamiaji nchini Uingereza. Baada ya 9/11, watu wa Asia wa kila dini walilengwa katika kampeni ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni ambayo ilishindwa kutofautisha dini na rangi ya ngozi ya mtu. Hata miaka mitano iliyopita, wazo kwamba ubaguzi wa rangi sio tatizo tena nchini Uingereza lilipuuziliwa mbali huku wimbi la uhalifu wa chuki za kibaguzi likichochewa na kura ya Brexit: kura ambayo Sunak amesema mara kwa mara kuwa anajivunia kuiunga mkono. Tukumbuke kuwa Sunak ni mfuasi mkubwa wa sera za Rwanda zinazofuatwa na Priti Patel, sera ambazo pengine zingewanyima wazazi wake kuwahi kuja Uingereza. Sunak, kama vile nyota wengine wengi weusi na hudhurungi wanaochipuka katika chama cha Conservative, anaonekana kuathirika kutokana na hali ya kuhisi haja ya kuonyesha kwamba wanaipenda Uingereza kidogo kiasi zaidi kuliko sisi wengine: kwamba wana jukumu maalum la kulinda nchi yao zaidi; kwamba lazima waonyeshe kiwango tofauti cha shukrani kwa ajili yake; na kwamba kwa namna fulani kuna hati ambayo lazima wote waisome ili kuwafurahisha wale ambao kisilika wanaweza kutowaamini. Milionea mkubwa Sunak, ambaye alisoma katika Chuo cha kipekee cha Winchester na baadaye akaowa katika utajiri wa mabilionea, anahisi haja ya kudharau historia yake ya upendeleo ili kupata uungwaji mkono zaidi. Lakini kila kitu kuhusu maisha na malezi yake ni kinyume na mamilioni ya watu wanaong’ang’ana kulipa bili, kulipa kodi na kununua chakula. [Chanzo: The Guardian].
Uchaguzi wa Sunak unathibitisha ukweli mbili. Kwanza, utawala wa Uingereza uko katika mporomoko na hauwezi kupata "wanasiasa wanati wa kizungu" wanaofaa kuendesha nchi. Pili, Sunak ni WOG wa kweli - muungwana mwenye mwelekeo mzuri aliye finyangwa na utawala huo ili kuendesha mambo yao.
Mwanajeshi Mkuu wa Pakistan Atafuta Usawazishaji kati ya Marekani na China kabla ya Kustaafu
Huku muda ukiyoyoma kufikia kustaafu kwake, mkuu wa jeshi la Pakistan mwenye uwezo mkubwa, Jenerali Qamar Javed Bajwa, alifanya ziara iliyocheleweshwa kwa muda mrefu jijini Washington mapema Oktoba. Wengine waliiona kama safari ya bahati nzuri. Wengine walikisia kuwa ni ishara kwamba anakusudia kusalia baada ya muhula wake kukamilika mwezi ujao, kama vile alivyoongezewa muda mwaka wa 2019.
Vyovyote vile, dhamira ya Bajwa ilikuwa wazi: kuendeleza uhusiano muhimu wa kidiplomasia uliodhoofishwa kwa miaka mingi ya kutokuwa na imani, katika wakati ambapo Islamabad inakabiliwa na dhoruba ya changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa, ikiwwemo msukosuko wa kisiasa uliochochewa Ijumaa iliyopita kwa kubatilishwa kwa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan kushikilia afisi ya umma.
Vyanzo vilivyo na ufahamu wa moja kwa moja wa mikutano ya jenerali ya hivi majuzi vinachora picha ya Pakistan ikiwa haitafuti chochote isipokuwa mpango mpya na Marekani – ule unaosawazisha mafungamano na China, kusaidia kupunguza mivutano na India na kukuza uchumi unaotatizika, huku ikidumisha mahusiano ya kijeshi. Kulingana na afisa mmoja anayefahamu mwenendo wa mikutano hiyo, Bajwa aliwasilisha ruwaza ya uhusiano wa nchi mbili "kama vile maelewano ya Wamarekani na Korea Kusini." "Aliwaambia kuwa tungependa kuwa mshirika wa kimkakati wa Marekani sio kwa jina, lakini kwa vitendo," afisa huyo alisema, akizungumza kwa sharti la kutotajwa. Ujumbe ulikuwa kwamba kunapaswa kuwa na "wavu mpana zaidi unaotuunganisha -- miundombinu, teknolojia, afya na biashara -- na sio tu mafungamano ya kijeshi na ulinzi ambayo tumeyategemea kwa miongo kadhaa." Akizungumzia hali mbaya ya kiuchumi ya Pakistan, afisa huyo alibainisha kuwa nchi hiyo inaweza kuwa "mshirika muhimu zaidi" ikiwa inafanya vizuri. "Kusema ukweli, tungependa [Wamarekani] kuwekeza ndani yetu." Huku Pentagon ikitoa taarifa fupi tu kuhusu ziara ya jenerali, kuadhimisha miaka 75 ya mahusiano ya kidiplomasia, Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa kanusho la wazi: Serikali ya kiraia ya Pakistan, na sio ya kijeshi ambayo imetawala nchi moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja tangu uhuru mnamo 1947, ndio “mzungumzi mkuu" wa Amerika. Mnamo Oktoba 13, Rais wa Marekani Joe Biden aliita Pakistan "moja ya mataifa hatari zaidi duniani," yenye "silaha za nyuklia bila mshikamano wowote." Karipio hilo lilitolewa kwenye kampeni, lakini liliisukuma Islamabad kumwita balozi wa Marekani. Siku iliyofuata, azimio la pande mbili liliwasilishwa katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, na kutangaza kwamba jeshi la Pakistan lilifanya mauaji ya halaiki mnamo mwaka 1971 dhidi ya raia wake. [Chanzo: Nikkei Asia]
Tabia ya Bajwa inasisitiza tu uhusiano uliopotoka wa bwana na mtumwa uliopo kati ya Amerika na Pakistan. Kipote cha mabwenyenye wa Pakistan hawawezi kufikiria ulimwengu bila Amerika na kuendelea kupeana ubwana zaidi wa Pakistan ili kuwafurahisha mabwana zao.
Rais Xi wa China asema Yuko Tayari Kufanya Kazi na Marekani kwa ajili ya Manufaa ya Pamoja
Rais Xi Jinping alisema China iko tayari kufanya kazi na Marekani kutafuta njia za kupata manufaa ya wote wawili, televisheni ya taifa ya China iliripoti mnamo Alhamisi, kabla ya uwezekano wa kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden nchini Indonesia. Kama dola kubwa, China na Marekani zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano ili kusaidia kuleta utulivu kwa dunia, Xi alisema katika ujumbe kwa hafla ya Kamati ya Kitaifa ya Uhusiano wa Marekani na China mnamo Jumatano. Nchi hizo mbili zimekuwa katika msuguano juu ya sera ya China kuhusu Taiwan, uhusiano wa China na Urusi na hivi karibuni zaidi, juhudi za Marekani kuzuia makampuni yake ya semiconductor kuuza teknolojia kwa makampuni ya China. Hivi majuzi China ilikasirishwa na msururu wa ziara za wabunge wa Marekani nchini Taiwan. China ilisema kuwa Marekani ilikuwa ikituma "ishara hatari" katika kisiwa hicho kinachotawaliwa kidemokrasia, ambacho China inadai kuwa ni chake. [Chanzo: Reuters]
Baada ya kuimarisha nafasi yake ya ndani, Xi anatoa ilani ya maridhiano kwa Marekani kwa lawama mpya. Inaonekana kwamba nguvu ya Amerika juu ya Urusi nchini Ukraine na ujanja wa kisiasa wa Amerika katika Asia Pasifiki inamlazimisha Xi kufikiria upya matarajio ya China katika eneo hilo. Hili linatarajiwa, kwani China haina dhamira ya kisiasa au uzoefu wa kihistoria wa kuwa na dola kubwa na kupambana na ukuu wa Marekani.