Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa vya Habari 21/12/2022

Vichwa vya Habari:

Serikali ya Pakistan Yazindua Mpango wa Kitaifa wa Kuhifadhi Kawi

Moscow Yasema Sera za Marekani Zimeiweka Marekani na Urusi Ukingoni mwa ‘Mgongano wa Moja kwa Moja’

Taliban Yafunga Vyuo Vikuu kwa Wanawake

Maelezo:

Serikali ya Pakistan Yazindua Mpango wa Kitaifa wa Kuhifadhi Kawi

Waziri wa Ulinzi wa Pakistan Khawaja Muhammad Asif alisema serikali ya kifederali itazindua mpango wa kitaifa wa kuhifadhi kawi kupitia mipango kama vile kufungwa mapema kwa masoko, mikahawa na biashara zengine. Mpango huo mpya wa uhifadhi wa kawi unalenga kudhibiti tatizo la umeme nchini Pakistan, ambalo linatokana na uhaba wa gesi asilia, sera za kupunguza kiasi cha umeme katika baadhi ya majimbo na msukosuko mkubwa wa kawi nchini humo. Kama sehemu ya mpango mpya wa kuhifadhi kawi, serikali pia itatekeleza mfumo wa kuhimiza takriban 20% ya wafanyikazi kufanya kazi nyumbani, na pia kukuza uagizaji na utumiaji wa baiskeli za kielektroniki na taa zenye kuhifadhi kawi. Deni jumla la Pakistan limeripotiwa kukua hadi takriban rupia trilioni 4 (dolari bilioni 17). Haishangazi, kwamba mpango huo mpya unahatarisha kuongezeka kwa kutoridhika kwa watu wengi kwani utasababisha hasara kwa biashara na kutatiza zaidi shughuli za kiuchumi.

Moscow Yasema Sera za Marekani Zimeiweka Marekani na Urusi Ukingoni mwa ‘Mgongano wa Moja kwa Moja’

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilionya mnamo Jumatatu kwamba sera za Washington zimeifikisha Marekani na Urusi kwenye ukingo wa "mgongano wa moja kwa moja." Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova alitoa maoni hayo akijibu taarifa ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price, ambaye alisema wiki iliyopita kwamba Urusi inapaswa "kulaumiwa" kwa kuzorota kwa uhusiano wa Marekani na Urusi. Katika muda wote wa vita, maafisa wa Urusi wameweka wazi kwamba wanaamini kuwa hawapigani tu na vikosi vya Ukraine nchini Ukraine bali pia Marekani na NATO. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov hivi karibuni alisema kuwa Marekani na NATO "zinashiriki moja kwa moja" katika vita kwa kutoa silaha na kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine. Licha ya tathmini hii, Urusi kwa sasa haijachukua hatua zozote za kuirudisha nyuma Amerika. Kufichua tu hatua za Marekani kumefanya kidogo kubadilisha machafuko nchini Ukraine.

Taliban Yafunga Vyuo Vikuu kwa Wanawake

Taliban imetangaza kufungwa kwa vyuo vikuu kwa wanawake nchini Afghanistan, kwa mujibu wa barua ya waziri wa elimu ya juu. Waziri huyo anasema hatua hiyo ni hadi itakapotangazwa tena. Inatarajiwa kuanza kutumika mara moja. Pia inazuia upatikanaji wa elimu rasmi kwa wanawake, kwani tayari walikuwa wametengwa na shule nyingi za sekondari. Kumekuwa na mgawanyiko kati ya wanachama wa Taliban. Miongoni mwa wale wanaoamini wanahitaji kutoa taswira ya wastani kwa jumuiya ya ndani na wale wanaoamini wanahitaji kutimiza matakwa ya uungwaji mkono wa Taliban ambao wanahisi wamejitolea sana kwa jumuiya ya kimataifa. Nje ya rekodi, baadhi ya wanachama wa Taliban wamesema mara kwa mara wana matumaini na wanafanya kazi kujaribu kuhakikisha wasichana wanapata elimu. Taliban wanakabiliwa na changamoto kubwa tangu wachukue hatamu Agosti 2021, uchumi unaodorora na kutengwa kimataifa, elimu kihakika ndiyo jambo dogo zaidi kati ya wasiwasi wao.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu