Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 04/01/2023

Vichwa vya Habari:

China Yagundua Teknolojia ya Hali ya Juu ya Microchip kama Pigo kwa Vikwazo vya Magharibi

Hasira ya Wapalestina juu ya Ziara ya Waziri wa Mrengo wa Mbali wa Kulia ya Eneo Takatifu

Uingereza Kutangaza IRGC kuwa Kundi la Kigaidi

Maelezo:

China Yagundua Teknolojia ya Hali ya Juu ya Microchip kama Pigo kwa Vikwazo vya Magharibi

China imegundua mbinu ya usanifu wa microchip ambayo hapo awali ilikuwa imebobewa tu na nchi za Magharibi, katika pambano ambalo linaweza kudhoofisha vikwazo. Faili za hati miliki zinaonyesha kuwa Huawei imepiga hatua katika mbinu muhimu ya utengenezaji wa chip, na hivyo kuongeza matarajio kwamba kampuni hiyo inaweza hatimaye kuanza kutengeneza baadhi ya microchip ndogo na zenye nguvu zaidi kipeke yake. Maendeleo kama haya yatairuhusu Beijing kuvuka vikwazo vya Magharibi. Washington, Brussels na London kwa sasa zote zinazuia ufikiaji wa chip za kompyuta zilizotengenezwa na Magharibi nchini China kwa hofu kwamba taifa hilo la Kikomunisti linaweza kukuuza uwezo mpya wa kijeshi zaidi ya uwezo wa majeshi ya Magharibi kupinga. Jibu la China kwa udhibiti wa mauzo ya nje wa Marekani lilikuwa ni kulalamika tu kwa WTO na jibu thabiti zaidi lilihitajika. China sasa imejibu kwa kishindo kikubwa, mpira sasa umerudi upande wa uwanja wa Marekani.

Hasira ya Wapalestina juu ya Ziara ya Waziri wa Mrengo wa Mbali wa Kulia ya Eneo Takatifu

Waziri wa usalama wa taifa wa mrengo mbali wa kulia wa ‘Israel’, Itamar Ben-Gvir, aliingia katika nyua za Msikiti wa Al-Aqsa katika Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu. Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha Ben-Gvir akizuru ua na maelezo mazito ya usalama. Wapalestina wamelaani ziara ya waziri wa mrengo wa mbali kulia wa Israel katika eneo takatifu kama "chokozi isiyo na kifani". Waziri wa Usalama wa Taifa Itamar Ben-Gvir, ambaye ametoa wito wa kuwepo mkazo zaidi dhidi ya Wapalestina, alizunguka eneo hilo akiwa amezingirwa na polisi. Ziara ya Bw Ben-Gvir ilikuwa ni kitendo chake cha kwanza hadharani tangu serikali, inayoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kuapishwa. Bw Ben-Gvir, kiongozi wa chama cha Otzma Yehudit (Jewish Power) amekuwa akisema kwa muda mrefu kwamba anataka kuleta mabadiliko ya sheria ili kuruhusu ibada ya Kiyahudi kwenye eneo hilo. Hakuna dalili kwamba Bw Ben-Gvir alisali wakati wa ziara ya Jumanne. "Mlima wa Hekalu uko wazi kwa kila mtu," aliandika tweet, akiifuatisha na picha yake akiwa amezungukwa na ukuta wa askari wa usalama yenye Kuba la Mwamba la dhahabu nyuma.

Uingereza Kutangaza IRGC kuwa Kundi la Kigaidi

Uingereza inapanga kulipandika jina Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kama kundi la kigaidi. Ubandikaji huo utafanya iwe vigumu kwa Uingereza na Iran kufanya maendeleo katika mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Uingereza ndiyo nchi ya hivi punde zaidi ya Ulaya kufikiria kuiita IRGC kama shirika la kigaidi, na huku silaha za Iran zikihamia Urusi na ukandamizaji dhidi ya maandamano dhidi ya serikali ukiendelea. Tangazo hilo lilikuja baada ya IRGC kuwakamata raia saba wa Iran na Uingereza ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano na maandamano ya kuipinga serikali yanayoendelea nchini Iran, na London pia hivi karibuni ilifichua njama 10 zinazohusishwa na IRGC za kuwateka nyara au kuua watu nchini Uingereza mnamo 2022.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu