Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari: 26/07/2023

Wazayuni Wapitisha Sheria ya Mfarakano

Maelfu ya wahafidhina wametia saini matangazo ya kuapa kutoendelea kuripoti kazini ikiwa sheria ya kufanyia marekebisho mahakama itapitishwa. Mnamo Jumatatu 26 Knesset ya Wazayuni (Bunge) ilipitisha sheria yenye utata sana ya kupunguza nguvu za Mahakama Upeo. Mswada unaoitwa "wenye busara" uliidhinishwa kwa kura 64 hadi 0, baada ya upinzaji kususia kura ya mwisho. Lakini vita bado havijamalizika na vitaendelea kwa miezi kwani kesi kadhaa za kuomba rufaa Mahakama ya Upeo kubatilisha sheria mpya hazitafanyika. Marekebisho ya mahakama yalilaaniwa na maafisa wa serikali ya Marekani na kutoka kwa Wazayuni walio ughaibuni. Wana wasiwasi kuwa vyama vya kidini vya kitaifa na vya Orthodox vilivyoshirikishwa na Netanyahu vitaweza kuunda sera yenye nguvu zisizo dhibitiwa. Uamuzi huo unaleta miezi ya mtikisiko, na rais wa 'Israel' akiwaonya viongozi wa kisiasa kwamba nchi hiyo ilikuwa "katika hali ya dharura ya kitaifa". Marekebisho yenye utata yaliitenga Israel, na kusababisha moja ya machafuko mabaya zaidi ya nyumbani katika historia ya nchi hiyo. Mamia ya maelfu ya waandamanaji waliandamana mabarabarani kila wiki tangu kuanza kwa mwaka kulaani kile wanachosema ni shambulizi juu ya demokrasia. Wakuu wa zamani wa huduma za usalama za Israel, majaji wakuu, na takwimu maarufu za kisheria na wafanyibiashara wote wametoa sauti dhidi ya mageuzi ya serikali, ambayo wanayaona kama unyakuzi wa mamlaka wa Netanyahu na washirika wake wa mrengo wa kulia.

Mashambulizi ya Droni ya Ukraine

Ikulu ya White House ilisema haikuunga mkono Ukraine kuzindua mashambulizi ndani ya Urusi baada ya droni mbili kutoka kwa majengo ya Ukraine yaliyoharibiwa huko Moscow mnamo Jumatatu, 26 Julai. "Kama jambo la jumla hatuungi mkono mashambulizi ndani ya Urusi," msemaji wa White House Karine Jean-Pierre aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa waandishi wa habari. Droni moja iligonga karibu na makao makuu ya ulinzi ya Urusi kwa pigo la mfano ambalo lilisisitiza ufikaji wa droni kama hizo, na afisa mwandamizi wa Ukraine alisema kutakuwa na mashambulizi zaidi. Mashambulizi haya yanakuja nyuma ya shambulizi la droni, kwenye kiti cha mfumo wa kisiasa wa Urusi, Kremlin mnamo mwezi Mei. Urusi imeng’ang’ana kukabiliana na mashambulizi ya droni ua Ukraine huku Ukraine ikiendelea kuyazindua ndani kabisa katika eneo la Urusi.

OIC Yaisimamisha Sweden

Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu limesimamisha hadhi ya mjumbe maalum wa Sweden juu ya msururu wa kuchomwa kwa Quran huko Stockholm ambao ulizua hasira na maandamano ya watu katika nchi kadhaa za Waislamu. Shirika hilo lilikuwa na mataifa 57 yenye Waislamu wengi lilisema kusimamishwa huko ni kwa sababu ya "kupewa leseni na mamlaka za Sweden ambazo iliwezesha udhalilishaji wa mara kwa mara wa utukufu wa Quran na nembo za Kiisilamu." Waandamanaji nchini Iraq walivamia ubalozi wa Sweden na serikali ya Iraq ikakata mahusiano ya kidiplomasia na Sweden. Uchomaji hadharani wa Quran nchini Denmark mnamo Ijumaa 21, Julai ulizua maandamano zaidi nchini Iraq, baadhi yao yakiwa na vurugu. Waandamanaji walikabiliana na polisi wakati walipojaribu kuvamia Eneo la Kijani jijini Baghdad ambapo ubalozi wa Denmark uko, na huko Basra, waandamanaji walichoma moto vifaa vya mradi wa madini wa Baraza la Wakimbizi la Denmark. Wizara ya Mambo ya nje ya Denmark ililaani kuchomwa kwa Quran. "Kuchoma maandiko matakatifu na nembo nyenginezo za kidini ni kitendo cha aibu ambacho kinakosea heshima dini ya wengine," ilisema. "Ni kitendo cha uchochezi kinachoumiza watu wengi na kusababisha mgawanyiko kati ya dini na tamaduni tofauti tofauti." Iliongeza, hata hivyo, kwamba "uhuru wa kujieleza na uhuru wa mkusanyiko lazima uheshimiwe." OIC, inajumuisha mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta duniani na mzalishaji wa gesi. Inajumuisha mataifa ambayo yalitoa dhamana kwa Magharibi wakati wa mgogoro wa kiuchumi mnamo 2008. Licha ya nguvu hii yote, walikusanyika kusimamisha tu wa uanachama wa Sweden pekee huku Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) kikishambuliwa.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu