Jumatano, 06 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari 11/10/2023

Wazayuni Wajiandaa kwa Uvamizi wa Gaza

Maafisa wa Kizayuni wameiita 7 Oktoba sasa huko 9/11 wakati Hamas na makundi mengine ya upinzani yalizindua operesheni kutoka ardhini, baharini na hewani dhidi ya 'Israel'. Wapiganaji wa Hamas waliingia maili 15 ndani ya umbile la Kiyahudi na kuchukua kambi za kijeshi, vituo vya polisi na mateka wengi. Uvamizi huu wa kujasiri uliishtua 'Israel' na wengi wakijaribu kupanda ndege kuondoka 'Israel'. Upinzani wa Palestina ulichukua zaidi ya mateka 150, hasara kubwa zaidi kwa umbile hilo. Huku 'Israel' ikijiandaa kwa uvamizi wa Ukanda wa Gaza, viongozi wa Magharibi waliushutumu upinzani wa Palestina kama ugaidi. Watawala wa Waislamu kando na taarifa za amani na kupunguza ghasia walifanya kichache. 'Israel' sasa inakabiliwa na matarajio ya vita vya mijini na majeruhi wengi licha ya nguvu zake za kijeshi.

‘Israel’ Yasema, Haina Ushahidi Iran ilihusika katika Shambulizi la Hamas

Maafisa wa 'Israel' wamesema hawana ushahidi kwamba Iran ilihusika katika shambulizi la Hamas kusini mwa 'Israel' baada ya ripoti moja kutoka Jarida la Wall Street kudai maafisa wa Iran walisaidia kupanga operesheni hiyo. "Hatuna ushahidi au thibitisho" kwamba Iran ilihusika, msemaji wa Kikosi cha Ulinzi cha 'Israel' (IDF) Meja Nir Dinar aliiambia POLITICO. Dinar aliacha wazi uwezekano kwamba Tehran alihusishwa na shambulizi hilo, akisema, "Kwa sababu tu huna ushahidi huo haimaanishi kuwa Iran haiko nyuma yake." Rear Adm. Daniel Hagari, msemaji mwengine wa IDF, alitoa maoni kama hayo. "Iran ni mchezaji mkuu, lakini bado hatuwezi kusema iwapo ilihusika katika upangaji au mafunzo," Hagari alisema. Ripoti hiyo ya Jarida la Wall Street ilidai Iran iliipa Hamas idhini kwa shambulizi hilo wakati wa mkutano huko Beirut wiki iliyopita, lakini Barakeh alisema hakuna mtu yeyote kutoka kwa Amri Kuu ya Kijeshi au Afisi ya Kisiasa ya Hamas iliyekuwa katika mji mkuu wa Lebanon wiki iliyopita. Alikubali kwamba Iran hapo awali iliisaidia Hamas lakini alisema tangu Vita vya Gaza vya 2014, kundi hilo limekuwa linatengeneza makombora yake na kuwapa mafunzo wapiganaji wake. Barakeh alisema alishangaa kwamba shambulizi hilo, lililopewa jina la "Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa," lilifanya uharibifu mkubwa kwa 'Israel.' "Tulishangazwa na kuanguka huku kukubwa," alisema. "Tulikuwa tunapanga kupata mafanikio na kubadilishana wafungwa nao. Jeshi hili lilikuwa ni kitisho feki."

Idadi Inayokua ya Watu wa Ukraine Yapinga Vita

Kura ya hivi karibuni iligundua kuwa idadi ya Waukraine wanaotaka kupigana na Urusi hadi mwisho wa vita imepungua hadi 60%. Rais Volodymyr Zelenskyy ana udhibiti thabiti juu ya vyombo vya habari nchini Ukraine, na serikali yake imewalenga wapinzani dhidi ya kupigana vita. Matokeo ya uchunguzi wa Gallup yaliyotolewa mnamo Jumatatu yanaonyesha uungaji mkono wa "Kupambana hadi Vita Vitakaposhindwa" imepungua hadi 60% kutoka 70% mwaka jana. Idadi ya Waukraine wanaotaka kutafuta azimio la kidiplomasia imeongezeka kutoka 25% hadi 31% katika miezi 12 iliyopita. Uungaji mkono wa kupata mwisho wa vita una nguvu katika maeneo ambayo mapigano yanaendelea. Idhini inayofifia ya mapigano inajiri wakati msimu wa joto wa Ukraine ulisababisha majeruhi makubwa na manufaa madogo ya eneo. Waungaji mkono wa magharibi wa Kiev walijua operesheni za kijeshi haziwezi kufanikiwa na zinaweza kusababisha majeruhi wa hali ya juu. Mnamo Agosti, gazeti la Washington Post liliripoti kufeli kujibu mapambano kumesababisha kuvunika moyo.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu