Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya habari 20/04/2020

Vichwa vya habari:

Virusi vya korona vitaongeza idadi maradufu ya watu wenye njaa

COVID-19: Misikiti nchini Pakistani kubakia wazi kwa ajili ya swala wakati wa mwezi wa Ramadhan licha ya Kusambaa kwa virusi vya Korona

Shirika la Fedha Duniani (IMF) linasema 'Uzuiaji Mkubwa wa watu majumbani' utaathiri uchumi wa dunia kwa kiwango kibaya sana tangu kutokea kwa mporomoko wa kiuchumi wa kiulimwengu

Maelezo:

Virusi vya korona vitaongeza idadi maradufu ya watu wenye njaa

Usambazaji wa chakula duniani kote “utavurugika kwa kiwango kikubwa” kutokana na virusi vya korona, na watu wenye matatizo makubwa ya njaa wataongezeka maradufu, hadi pale serikali zitakapo chukua hatua, baadhi ya kampuni za chakula zilionya. Unilever, Nestlé na PepsiCo, pamoja na mashirika ya wakulima, makundi ya kiraia, ya kielimu, na Umoja wa Mataifa yameawaandikia viongozi wa ulimwengu, kuwaambia waache mipaka yao wazi kwa ajili ya biashara ili kuzisaidia jamii kutokana na hatari, na kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa chakula kulingana na mazingira. Makundi hayo yamezitaka serikali “kushirikiana kwa pamoja kuzuia janga la virusi vya Korona lililogeuka na kuwa janga la chakula na la kibinadamu”. Kuacha biashara ziendelee itakuwa ni muhimu, kwa kuwa itasaidia kuimarisha usambazi wa chakula na kuwalinda wakulima kutoka katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea, wanasema. Nchi zenye uwezo mkubwa zaidi duniani (G20) zinapata ongezeko la shinikizo kuchukua hatua: Kundi la washindi wa kiuchumi wa tuzo za Nobel na maafisa wakuu wa zamani wa benki ya maendeleo waliandikia jumuiko la nchi hizo wakishauri kwamba trilioni za dolari zitahitajika kusaidia nchi zinazoendelea ili kupambana na janga la virusi vya korona. Wiki hii zaidi ya viongozi wa zamani 100, ikiwa ni pamoja na Tony Blair, Gordon Brown na Nicolas Sarkozy, pia nao wamezitaka G20 kuchukua hatua za haraka kupambana na virusi hivi au kuhatarisha kujirudia upya kwa mikurupuko. Hata hivyo, hatua walizo kubaliana ni chache. Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limeendelea kuhofu kwamba, ingawa mavuno ni mazuri na kuna uzalishaji wa chakula cha kutosha kulisha dunia nzima, vikwazo vya usafirishaji bidhaa nje na ushuru uliowekwa na baadhi ya serikali zitasababisha uhaba. Onyo kali kutoka kwa viongozi wa viwanda vinavyozalisha chakula limekuja kufuatia baadhi ya nchi kuanza kupiga marufuku baadhi ya vyakula. Kupunguza harakati za watu, kutokana na zuio la kutotoka nje, pia inatishia kupunguza nguvukazi mashambani katika wakati muhimu wa mwaka kwa mazao mengi. “Hatari ya uvurugikaji mkubwa wa usambazaji wa chakula katika miezi ijayo inazidi kuongezeka, haswa kwa nchi zenye watu wenye kipato kidogo wanaotegemea uagizwaji wa chakula kutoka nje, nyingi kati ya hizo zipo kusini mwa jangwa la sahara,” viongozi wa viwanda vya vyakula walionya katika barua yao. Bandari na mipaka lazima viachwe wazi kwa ajili ya biashara ya chakula, wasihi, zile nchi kubwa zinazo safirisha nje chakula “lazima ziweke wazi kwamba zitaendelea kuyasambazia kikamilifu masoko na wateja wa kimataifa”. [Chanzo: gazeti la The Guardian]

Endapo zuio la kiulimwengu la kutoka nje halitaondolewa hivi karibuni, watu wengi zaidi watakufa kwa njaa kuliko kufa kwa virusi vya korona. Na kwa mara nyingine tena itakuwa ni janga lililosababishwa na mwanadamu!

Shirika la Fedha Duniani (IMF) linasema 'Uzuiaji Mkubwa wa watu majumbani' utaathiri uchumi wa dunia kwa kiwango kibaya sana tangu kutokea kwa mporomoko wa kiuchumi wa kiulimwengu

"Zuio kubwa zaidi la watu kutotoka nje" lililo chochewa na janga la virusi vya korona litaathiri vibaya uchumi tangu kutokea mporomoko mkubwa wa kiuchumi wa kiulimwengu na hali itazidi kuwa mbaya zaidi kama haitadhibitiwa, Shirika la Fedha Duniani liliweka wazi mnamo siku ya Jumanne. Katika takwimu za IMF, pato jumla la ulimwengu litashuka kwa asilimia 3 mwaka huu, endapo itadhaniwa kwamba tisho la janga hili litafifia katika nusu ya pili ya mwaka huu. Mafanikio ya hatua za kudhibiti na usaidizi wa sera imara huenda yakalisukuma pato jumla kurudi katika hali yake kwa asilimia 5.8 mnamo 2021, hazina hiyo ilisema katika ripoti yake ya kiuchumi ya kiulimwengu iliyotoka hivi karibuni. Utabiri huo ulipiku kupungua kwa asilimia 0.1 ya pato jumla kuliko shuhudiwa mnamo 2009 wakati wa kilele cha mgogoro wa kifedha. Pato jumla la Amerika linatarajiwa kupungua kwa asilimia 5.9 mnamo 2020 kabla ya kurudia hali ya kawaida na kukua kwa asilimia 4.7 mwaka utakaofutia, tathmini ya IMF, iliongezea kwamba kanda ya Ulaya itaanguka kiuchumi kwa asilimia 7.5 kabla ya kurudi katika hali ya kawaida mwaka 2021. "Janga hili halina mfano wake," Gita Gopinath, mshauri wa kiuchumi wa IMF, aliandika katika utangulizi wa ripoti yake, aliongezea, "kama ilivyo katika vita au mizozo ya kisiasa, haijulikani muda wa kuisha kwa tatizo hili." Hata katika nukuu za IMF, hatari ya tatizo la kiuchumi ni kubwa mno. Shirika hilo limeweka wazi mambo matatu ambayo endapo dunia itapambana nayo dhidi ya virusi vya korona, maradhi yanayo sababishwa na virusi vya korona, yatapotea. Ikiwa janga litadumu kwa mwaka mzima wa 2020 uchumi utafikia asilimia 3 kinyume na matarajio, kulingana na IMF. Athari za mkurupuko wa awamu ya pili utalisukuma pato jumla hadi takriban asilimia 5 chini ya kiwango cha hazina hiyo mwakani, hivyo kufutilia mbali utabiri wake wa kurudi taratibu kwa hali ya kawaida ya kiuchumi. Katika mambo matatu mabaya yaliyo orodheshwa na IMF, kudumu kwa tatizo hili mwaka 2020 na kuibuka tena mwaka ujao kutarudisha nyuma takriban asilimia 8 ya uzalishaji wa kiulimwengu chini ya kiwango chake cha mwaka wa 2021. Kurefuka huku kwa janga hili kutasababisha upungufu mkubwa wa pato jumla la uchumi wa ulimwengu kwa miaka miwili na huenda hata ukawa mbaya zaidi kwani madeni ya umma yataongezeka na kuacha "tishio la ziada," shirika hilo lilisema . "Nchi nyingi zinakabiliana na majanga mawili yanayo jumuisha mshtuko wa kiafya, matatizo ya ndani ya kiuchumi, mahitaji makubwa kutoka nje, kupungua kwa viwango vya rasilimali, na kuanguka kwa bei za bidhaa," IMF ilisema katika ripoti yake. "Matokeo ya hatari zaidi yanapaswa kutarajiwa." [Chanzo: Business Recorder]

Ulinganishaji wa IMF kati ya janga hili na ule mporomoko mkubwa wa kiuchumi wa kiulimwengu hapa sio mahali pake. Kufungwa kwa uchumi kuliko sababishwa na virusi vya korona ni kwa mara ya kwanza, na haijawahi kutokea katika historia. Wamagharibi wamesimamisha shughuli zote za kiuchumi ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi hivi. Kama Wamagharibi wangewahi mapema kutekeleza uwekaji masafa ya kijamii baina ya mtu kwa mtu, na kufuatilia waliokutana na waathiriwa basi hatua ya kufunga shughuli za kiuchumi haingetokea.

COVID-19: Misikiti nchini Pakistani kubakia wazi kwa ajili ya swala wakati wa mwezi wa Ramadhan licha ya Kusambaa kwa virusi vya Korona

Pakistan imeruhusu swala za jamaa misikitini chini ya maelekezo makali. Rais wa Pakistan Dkt. Arif Alvi alishindwa kuzuia shinikizo lililotolewa na umoja wa viongozi wa kidini wakati wa mkutano mrefu uliofanywa pamoja nao kupitia njia ya mtandaoni katika jiji la Islamabad na pia kutoa maelekezo ya  swala za Taraweh na swala za Ijumaa wakati wa mwezi wa Ramadhan ingawa idadi ya mambukizi na vifo inazidi kuongezeka. Vifo vinavyo sababishwa na virusi vya korona nchini Pakistan vimeongezeka hadi kufikia 167 huku idadi jumla ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi vya korona ikiongezeka hadi kufikia 8175 na waliopona wakiwa ni 1868. Punjab imesalia kuwa ndio kitovu cha maambukizi ikiwa na jumla ya wagonjwa 3649 ikifuatiwa na Sindh yenye jumla ya wagonjwa 2537, Khyber Pakhtukhwa 1137, Balochstan 376, Gilgit Baltistan 25, Islamabad 171 na eneo la Kashmir linalotawaliwa na Pakistan likiwa na wagonjwa 48. Rais Alvi katika makubaliano na Ulamaa (wasomi wa dini) alitangaza mikakati 20, ikiwa ni pamoja na maelekezo ya namna ya uhudhuriaji misikitini katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, aliwashauri waumini kuchukua tahadhari wakati wa utekelezaji wa ibada ili kupambana na janga la korona. Raisi Arif Alvi alisema kwamba misikiti yote nchini itabaki wazi kwa ajili ya utekelezaji wa swala za Taraweh wakati wote wa Ramadhan. Aliwashauri wananchi na viongozi wa kidini kuwa na nidhamu na kuchukua tahadhari dhidi ya janga la korona wakiwa wanaenda misikitini. Raisi alisisitiza kwamba watu wa Pakistan wanahitaji kuwaona viongozi wao wa kisiasa na kidini wakiwa na mshikamano na ikiwa kutakuwa na migogoro basi madhara yatakuwa makubwa zaidi. “Tumetafuta mapendekezo kutoka kwa serikali za mikoa kujumuisha mtazamo wao pindi zinapotoa maamuzi kuhusiana na hili,” Raisi alisema, akiongezea kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani Ejaz Shah yuko na mawasiliano na serikali hizo za mikoa kushughulikia hili, Geo TV iliripoti. Baada ya mazungumzo na wasomi wa kidini, Raisi Alvi alitangaza pia miongozo 20 ambayo ni lazima ifuatwe misikitini kama sehemu ya kuchukua tahadhari kuhakikisha usalama na kudhibiti kusambaa kwa virusi vya korona. “mafanikio ya mikakati hii hayategemei serikali au viongozi wa dini pekee bali kwa kila mmoja wetu,” aliongezea. [chanzo:  The Gulf News]

Tangu kuanza kwa janga la virusi vya korona, Serikali ya Pakistan imekuwa ikibaki nyuma, na ilichukua hatua pekee baada ya serikali za Kimagharibi kuchukua hatua. Hakuna haja ya uzuiaji mkali wa watu majumbani, ikiwa wagonjwa na watu walio hatarini kuambukizwa wametengwa na jamii. Jamii iliyo salia inaweza kuendelea  na shughuli zake kama kawaida, ikiwa ni pamoja na shughuli za kiuchumi na swala za jamaa.

#Covid19    #Korona     كورونا#

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu