Jumatano, 07 Dhu al-Hijjah 1443 | 2022/07/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya habari 01/05/2020

Vichwa vya Habari:

Virusi vya Korona: Trump Aendelea Kushikilia Nadharia kuwa Maabara ya China Ndio Chanzo cha Virusi vya Korona 

Kiongozi wa Dubai Atoa Mchango wa tani 60 za Vifaa Tiba vya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi (PPE) kwa Shirika la Huduma za Afya la Uingereza

Pakistan ina Tatizo la Utegemezi, asema Waziri Mkuu Imran Khan

Maelezo:

Virusi vya Korona: Trump Aendelea Kushikilia Nadharia kuwa Maabara ya China Ndio Chanzo cha Virusi vya Korona 

Rais wa Amerika Donald Trump ameonekana kupingana na vyombo vyake vya kijasusi kwa kudai kwamba ameona ushahidi unao onesha kuwa virusi vya korona vimeanzia katika maabara moja ya China. Mwanzoni afisi ya mkurugenzi wa ujasusi wa kitaifa nchini Amerika ilisema bado inaendelea kuchunguza chanzo cha virusi. Lakini afisi hiyo ilisema imethibitisha kwamba virusi vya korona "havikutengezwa na mwanadamu au kuundwa kwa mnyumbuko wa jeni". China imeikataa nadharia ya maabara na kushutumu majibu ya Amerika kuhusu virusi vya Korona. Tangu kujitokeza nchini China mwaka jana, virusi hivi vimeua watu 230,000 kote duniani ikiwemo watu 63,000 waliokufa nchini Amerika. Mnamo Alhamisi katika ikulu ya White House, Bwana Trump aliulizwa na mwandishi mmoja wa habari: "Je, hadi kufikia sasa umeona chochote kinacho kupa kiwango cha juu cha imani kwamba Taasisi ya uchunguzi wa virusi ya Wuhan ndio chanzo cha virusi hivi ?" "ndio, nimeona. Ndio, nimeona," Rais huyo alisema, bila ya kufafanua. "Na nafikiri Shirika la Afya Duniani [WHO] linapaswa kuona aibu kwa sababu limekuwa kama wakala wa mahusiano ya umma kwa China." Baadaye alipo ombwa kufafanua kauli yake, alisema : "Siwezi kukwambia hilo.

Siruhusiwi kukwambia hilo." Pia aliwaambia waandishi wa habari: "Ima wawe (China) wamefanya makosa, au vilianza tu kimakosa kisha wakatengeza vyengine, au je, kuna mtu yeyote aliyefanya kitu chochote kimakusudi kwa malengo fulani? "Sifahamu vipi magari, vipi watu hawakuruhusiwa kusafiri ndani ya China, lakini waliruhusiwa kusafiri sehemu nyinginezo za dunia. Hilo ni swali baya sana, hilo ni swali gumu kwa wao kulijibu." Gazeti la New York Times liliripoti mnamo Alhamisi kwamba maafisa wakuu wa ikulu ya White House waliiomba jamii ya kijasusi kuchunguza iwapo virusi vilikuja kutoka katika maabara ya utafiti ya Wuhan. Taasisi za ujasusi pia zimepewa kazi ya kuthibitisha kama China na WHO zilizuilia taarifa za awali kuhusu virusi hivi, maafisa ambao hawakutajwa majina waliliambia shirika la habari la NBC. Katika taarifa nadra ya umma, Afisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa, inayosimamia taasisi za upepelezi wa Amerika, mnamo Alhamisi ilisema inakubaliana na "itifaki pana ya kisayansi" kuhusu machimbuko kimaumbile ya virusi vya Korona . "Mashirika ya kijasusi yataendelea kuchunguza vikali habari zinazo ibuka na ujasusi ili kuthibitisha iwapo mkurupuko huu ulianza kupitia kukaribiana na wanyama walio ambukizwa au ikiwa ni matokeo ya ajali iliyotokea katika maabara ya Wuhan." Ilikua ni jibu la mwanzo la wazi kutoka kwa ujasusi wa Kiamerika kufichua nadharia za khiyana – kutoka Amerika pamoja na China – kwamba virusi hivi ni silaha za kibaolojia. [Chanzo: BBC]

Trump anailaumu China kwa kuficha sio tu mapungufu yake pekee, bali pia anafanya maandalizi ya uchaguzi mkuu mnamo Novemba. Kupitia kuigawanyia lawama China kuhusiana na janga la virusi vya Korona, Trump anataraji kupata uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa ngome za chama chake cha Republican katika uchaguzi wa uraisi ujao.

Kiongozi wa Dubai atoa Mchango wa tani 60 za Vifaa Tiba vya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi (PPE) kwa Shirika la Huduma za Afya la Uingereza

Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al-Maktoum amechangia tani 60 za vifaa tiba maalumu vya kujikinga wakati wa kutibu wagonjwa wa Korona kwa Uingereza, kwa mujibu wa afisi ya habari ya Dubai. Sheikh Mohammed amenunua vifaa tiba hivyo kutoka kwa wafanyi biashara nchini China na kuvitoa kama msaada kwa shirika la Huduma ya Afya ya Kitaifa ya Uingereza. Ndege zilizo beba shehena ya vifaa hivyo kutoka China ziliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow jijini London mnamo Alhamisi mchana, ndege nyingine nyingi zinatarajiwa kuwasili uwanjani hapo katika siku zijazo. Msemaji wa Sheikh Mohammed alisema  mchango huo umetolewa kwa sababu ya "uhusiano mzito na wa muda mrefu" kati ya mtawala wa Dubai na Uingereza" na kwamba “ atajitahidi kwa juhudi zote kuhakikisha wafanyakazi wa afya wa Uingereza wako salama,”  BBC iliripoti . Vifaa tiba hivyo vinajumisha barakoa, mavazi maalumu ya kuzuia maaambukizi na vifaa vingine muhimu, Afisi ya Habari ya Dubai ilisema. Uingereza bado ipo katika marufuku ya kutoka nje tangu tangazo la Boris Johnson la Machi 25, huku ikiwa na visa 171,253 vya maambukizi vilivyo thibitishwa na vifo 26,771 vilivyo tangazwa mnamo Alhamisi. Wafanyakazi wa afya wanahangaika kutokana na upungufu wa vifaa vya kujikinga na virusi na wameiomba serikali kujitahidi zaidi ili kuwapatia vifaa hivyo kwa madaktari waliomsitari wa mbele katika kutoa huduma [Arab News]

Umma wa Kiislamu unateseka kutokana na majanga tofauti tofauti ikiwemo virusi vya Korona, na  Dubai inaamua kutoa msaada wa vifaa tiba kwa Uingereza. Uingereza imekuwa ikiongoza katika vita dhidi ya Uislamu—bila ya kutaja kushirikiana na Imarati kuchochea vita nchini Yemen—katika nchi nyingi za Waislamu.

Pakistan ina Tatizo la Utegemezi, asema Waziri Mkuu Imran Khan

Huku Pakistan ikikabiliana na virusi vya korona na ongezeko la idadi ya maambukizi, Waziri Mkuu Imran Khan amesihi haja ya kujenga miundombinu ya afya ya kutegemewa yake yenyewe. “Virusi vya Korona vimeonyesha wazi kwamba Pakistan inahitajika kujenga miundombinu yake yenyewe ya tiba na kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje,” aliongezea Imran. Akizungumza wakati alipotembelea maonyesho ya COMSTECH jijini Islamabad mnamo Jumatano, Waziri Mkuu Imran alisema: “Tunatatizo la utegemezi; hatujiamini, hatuja piga hatua katika elimu-uchumi kwa sababu hatujawekeza katika elimu na utafiti. Wapakistani wanafanya vizuri nje ya nchi; kwa nini mfumo huo msiutengeneze hapa?” “Tunatakiwa kuweka kuangazia ujenzi wa miundomsingi yetu ya afya hivyo tutakuwa tumejiandaa na hali ya dharura yoyote itakayojitokeza baadaye,” alisema na kuongezea kwamba janga la virusi vya Korona limetoa fursa ya kuzalisha mashine za upumuaji ndani ya nchi na vifaa tiba vya kujikinga na maambukizi kwa sio kila kitu kiagizwe kutoka nje.  Maana ya COMSTECH ni Kamati Simamizi ya Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu katika shughuli za Kisayansi na Teknolojia miongoni mwa nchi wanachama wa OIC. “Ni hivi sasa tu — kwa upungufu wa kiulimwengu— ambapo tumegundua kwamba utengenezaji wa mashine za kusaidia upumuaji sio jambo gumu.  Nchi iliyo na uwezo wa kutengeneza mabomu ya nyuklia, itashindwa vipi kutengeneza mashine za kusaidia kupumua?” alisema.

Kitendo cha Khan kujiingiza katika mikopo ya IMF kinasisitiza zaidi utegemezi wa Pakistan kwa dola za kigeni na taasisi zao. Hili linaonyesha kwamba maneno ya Khan yanapingana na vitendo vyake, huku akiitumbukiza zaidi Pakistan katika mtego wa madeni.

#Covid19    #Korona       كورونا#

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 14 Juni 2020 22:20

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu