Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Je, ni Nani Mashahidi wa Akhera? Na ni Nani Mwenye Kulilipa Deni la Shahidi?
Kwa Asmaa Fawzi Mohammad
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu alaykom wa Rahmatullah wa Barakatuh Sheikh wetu muheshimiwa,

Imetajwa katika kitabu "Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu 2", ukurasa wa 165 chini ya mada "Shahidi"… kuhusiana na shahidi wa Akhera: (Msimamo (sahih) kwa mujibu wa yale yaliyotoka kwa Muslim ni kuwa wako aina tano nao ni: anaye kufa kwa ugonjwa wa tauni (al-mat'un), anaye kufa kwa ugonjwa wa kuendesha (mabtun), anaye zama na kufa maji, anaye kufa kwa kuporomokewa na kufinikwa na kifusi (al-hadm), na anaye kufa akinyanyua neno la Mwenyezi Mungu nje ya uwanja wa vita.)

Huku ikisimuliwa katika Hadith nyInginezo kuwa mashahidi hao wamefungika wawe ndani ya njia ya Mwenyezi Mungu katika uwanja wa vita … kama ilivyo tajwa katika Hadith: Imesimuliwa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Amir kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«خَمْسٌ مَنْ قُبِضَ فِي شَيْءٍ مِنْهُنَّ فَهُوَ شَهِيدٌ: الْمَقْتُولُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْغَرِقُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْمَبْطُونُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْمَطْعُونُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالنُّفَسَاءُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ»

“Mambo matano mtu atakapo kufa kwa moja katika hayo basi yeye ni shahidi: anayeuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; anaye kufa kwa kuzama majini katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; anaye kufa kwa ugonjwa wa tumbo katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; anaye kufa kwa tauni katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; na mwanamke anaye kufa kwa mazazi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi.” [Sahih]

Swali: Je, kuna uhusiano wowote baina ya Hadith hizo mbili au je, kuna mgongano? Tafadhali fafanua jambo hili, kwa heshima zote stahiki.

Swali la pili: Vilevile imesimuliwa katika muktadha huo huo wa mada ya shahidi. Hadith iliyosimuliwa na Abdullah bin Amr bin Al-'As kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«يُغْفَرُ لِلشَّهِيدِ كُلُّ ذَنْبٍ إِلَّا الدَّيْنَ»

“Shahidi husamehewa kila dhambi isipokuwa deni.”

Swali ni: ikiwa Shahidi alishindwa kulipa deni lake baada ya shahada yake … ni nani anayepaswa kulilipa deni lake baada ya shahada yake? Natanguliza shukrani.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah wa Barakatuhu:

Kwanza: Kuhusu mashahidi:

1. Muslim amesimulia kutoka kwa Abu Hurayra (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِطَرِيقٍ وَجَدَ غُصْنَ شَوْكٍ عَلَى الطَّرِيقِ فَأَخَّرَهُ فَشَكَرَ اللَّهُ لَهُ فَغَفَرَ لَهُ وَقَالَ الشُّهَدَاءُ خَمْسَةٌ الْمَطْعُونُ وَالْمَبْطُونُ وَالْغَرِقُ وَصَاحِبُ الْهَدْمِ وَالشَّهِيدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ»

“Pindi mtu alipokuwa akitembea njiani aliona tawi lenye mwiba njiani akaliondoa kisha Mwenyezi Mungu akamshukuru na akamsamehe. Akasema: mashahidi ni aina tano: anaye kufa kwa ugonjwa wa tauni (al-mat'un), na anaye kufa kwa ugonjwa wa tumbo (al-mabtun), na anaye kufa kwa kuzama majini, na mtu anaye kufa kwa kuporomokewa na jengo na kufinikwa na kifusi na shahidi anaye kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu ‘azza wa jalla.”  

2. Imesimuliwa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Amir kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«خَمْسٌ مَنْ قُبِضَ فِي شَيْءٍ مِنْهُنَّ فَهُوَ شَهِيدٌ: الْمَقْتُولُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْغَرِيقُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْمَبْطُونُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْمَطْعُونُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالنُّفَسَاءُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ»

“Mambo matano mtu atakapo kufa kwa moja katika hayo basi yeye ni shahidi: anayeuliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; anaye kufa kwa kuzama majini katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; anaye kufa kwa ugonjwa wa tumbo katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; anaye kufa kwa tauni katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; na mwanamke anaye kufa kwa mazazi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi.” [Imeripotiwa na An-Nasa’i na Tabarani]

3. Hakuna mgongano, Hadith ya Muslim ni kamilifu (mutlaq):

«الْمَطْعُونُ وَالْمَبْطُونُ وَالْغَرِقُ وَصَاحِبُ الْهَدْمِ»

“anaye kufa kwa tauni (al-mat’un), anaye kufa kwa ugonjwa wa tumbo (al-mabtun), anaye kufa kwa kuzama majini, na mtu anaye kufa kwa kuangukiwa na jengo.” Ama ile Hadith nyengine, imefungwa (muqayyad) kwa maneno (katika njia ya Mwenyezi Mungu),

«وَالْغَرِيقُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْمَبْطُونُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ، وَالْمَطْعُونُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ شَهِيدٌ»

“Na anaye kufa kwa kuzama majini katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; na anaye kufa kwa ugonjwa wa tumbo katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi; na anaye kufa kwa tauni katika njia ya Mwenyezi Mungu ni shahidi.” Hivyo Hadith zote hizi huunganishwa kupitia kuitandaza iliyo kamilifu (mutlaq) juu ya iliyofungwa (muqayyad), hivyo basi wote hao ni mashahidi endapo watakuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kiashiria (Qareena) kinayapa maneno "katika njia ya Mwenyezi Mungu" maana yake, hivyo basi endapo itaashiriwa utoaji (nafaqa) (watoe katika njia ya Mwenyezi Mungu) au Jihad (wapigane Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu) basi hapo humaanisha kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu kabisa. Ama yale yaliyotajwa katika Sahih Bukhari kuwa Abu Musa (ra) amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je, mtu apiganaye kwa ajili ya ngawira, mtu apiganaye ili atajike na mtu apiganaye ili cheo chake kionekane. Ni yupi aliye katika njia ya Mwenyezi Mungu? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:  

«مَنْ قَاتَلَ لِتَكُونَ كَلِمَةُ اللَّهِ هِيَ الْعُلْيَا فَهُوَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ»

“Anaye pigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu kabisa basi yeye ndiye yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu.” … Lau maneno (katika njia ya Mwenyezi Mungu) yamemetajwa pasi na kiashiria (qareena) chochote.

Pili: ama swali lako kuhusu shahidi aliye na deni na akashindwa kulilipa kabla ya kifo chake, basi ulipaji wa deni hilo utaanguka juu ya warathi wake. Ikiwa warathi wake watashindwa kufanya hivyo, basi Dola italilipa kama ilivyo tajwa katika Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«أَنَا أَوْلَى بِكُلِّ مُؤْمِنٍ مِنْ نَفْسِهِ، مَنْ تَرَكَ مَالاً فَلِأَهْلِهِ، وَمَنْ تَرَكَ دَيْناً أَوْ ضَيَاعاً فَإِلَيَّ وَعَلَيَّ»

“Mimi niko karibu na waumini kuliko nafsi zao, anaye acha mali basi ni ya warathi wake, na anaye acha deni na wenye kumtegemea basi ni kwangu mimi na jukumu juu yangu.” [Imeripotiwa na Muslim] Vilevile Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) iliyopokewa na Abu Dawud kuwa Jabir amesema:

«كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لَا يُصَلِّي عَلَى رَجُلٍ مَاتَ وَعَلَيْهِ دَيْنٌ، فَأُتِيَ بِمَيِّتٍ فَقَالَ: أَعَلَيْهِ دَيْنٌ؟ قَالُوا: نَعَمْ دِينَارَانِ. قَالَ: صَلُّوا عَلَى صَاحِبِكُمْ. فَقَالَ أَبُو قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيُّ: هُمَا عَلَيَّ يَا رَسُولَ اللَّه،ِ قَالَ: فَصَلَّى عَلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا فَتَحَ اللَّهُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: أَنَا أَوْلَى بِكُلِّ مُؤْمِنٍ مِنْ نَفْسِهِ. فَمَنْ تَرَكَ دَيْنًا فَعَلَيَّ قَضَاؤُهُ، وَمَنْ تَرَكَ مَالًا فَلِوَرَثَتِهِ»

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikuwa hamswalii yeyote aliye kufa na deni. Maiti mmoja akaletwa kwake akauliza: ‘Je, ana deni?’ Wakasema: ‘Ndio, ana deni la dinar mbili.’ Akasema: ‘Mswalieni mwenzenu.’ Abu Qatadah akasema: ‘Nitazilipa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Kwa hiyo akakamswalia. Kisha Mwenyezi Mungu alipomfanya Mtume Wake tajiri kupitia ukombozi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), alisema: ‘Mimi niko karibu kwa kila muumini kuliko nafsi yake, anaye acha deni basi ni juu yangu kulilipa, na anaye acha mali basi ni ya warathi wake.”

Nataraji kuwa jibu hili litatosheleza maswali yote mawili, na Mwenyezi Mungu (swt) ni mjuzi zaidi na ni Mwingi wa hekima.

Ndugu yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Ijumaa, 29 Jumada I 1441 H
24/01/2020 M

Link ya jibu hili kutoka kwa ukurasa wa Facebook wa Amiri ni:

https://web.facebook.com/AmeerhtAtabinKhalil/posts/1262788063918262

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 24 Machi 2020 21:36

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu