Alhamisi, 19 Rajab 1444 | 2023/02/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Amiri wa Hizb ut Tahrir "Juu ya Maswali ya Wanaozuru Ukurasa Wake wa Facebook wa "Kifiqhi"

Jibu la Swali
Akili (‘Aql), Utambuzi (Idrak) au Fikra (Fikr)
Kwa: Atmani Atmani Atmani
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu Alaikum Sheikh wetu mheshimiwa: kuna tofauti gani kati ya rai iliyotangulia na maalumati yaliyotangulia katika njia ya kufikiri. Kwa kuzingatia kuwa fikra (fikr), utambuzi (idrak), au akili ('aql) hayatokei isipokuwa pamoja na vitu vinne: hisia, uhalisia, maalumati yaliyotangulia na ubongo ulio na uwezo wa kuunganisha. Je! Ni ipi tofauti kati ya rai zilizotangulia na maalumati yaliyotangulia katika kufasiri uhalisia?

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatu Allahi wa Barakatuh,

1- Kama ilivyoelezwa katika swali, akili ('aql), utambuzi (idrak), au fikra (fikr) ni uhamishaji hisia ya uhalisia kupitia hisia za mwili hadi kwenye ubongo pamoja na maalumati yaliyotangulia ambayo kwayo uhalisia huu hufasiriwa. Yaani, mchakato wa kiakili haukamiliki mpaka vitu vinne viwepo: uhalisia, hali ya kuuhisi uhalisia (hisia), ubongo unaofaa katika kuhusisha/kuunganisha (rabt), na maalumati yaliyotangulia juu ya uhalisia au yanayohusiana na uhalisia huo...

2- Ili kutafakari kuwepo kwa watu katika ardhi hii, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa Adam, amani iwe juu yake, maelezo yaliyotangulia ambayo yanaeleza hali halisi za sasa za dunia inayochunguzwa. Imeelezwa katika kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu III:

[Ama kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا]

“Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote” [Al-Baqarah: 31], maana ya haya ni vitu vilivyopewa majina sio lugha, yaani alimfundisha uhalisia wa vitu na sifa zake, ina maana alimpa habari anazozitumia kuhukumu vitu hivyo, kwa sababu kuhisi uhalisia hakujitoshelezi peke yake kuhukumu kitu na kuuona uhalisia wake, lakini ni jambo lisilokuwa na budi kuwa na taarifa za zilizotangulia ambazo kwazo uhalisia hufafanuliwa. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa amemfundisha Adam majina yaani vitu vilivyopewa majina, hivyo akampa maelezo ambayo kwayo anaweza kuvihukumu vitu anavyovihisi...] Mwisho.

3- Na ndipo fikra zikaibuka na kufuata kutoka kwa fikra ya mwanzo iliyotokea kwa Mwenyezi Mungu kumpa Adam maelezo yaliyotangulia, kisha akayatumia kueleza uhalisia wa kitu kilichokuwa kikichunguzwa pamoja na vipengele viwili alivyo navyo (ubongo na hisia), na maisha yakaendelea kujaa maeneo mapana ya fikra ... Hivyo, utambuzi sahihi wa jinsi mchakato wa kwanza wa kimantiki ulivyofanyika kwa mwanadamu bila shaka hupelekea kumwamini Mwenyezi Mungu (swt), na kwa hiyo mavuguvugu ya ukafiri ambayo hukataa kuwepo kwa Muumba hufafanua akili au mawazo kwa kuacha maalumati yaliyotangulia! Ingawa kufikiri juu ya uhalisia hakuwezi kufanyika bila ya kuwepo kwa maelezo yaliyotangulia yanayoueleza uhalisia, na hili linajulikana kwa udharura, lakini mavuguvugu ya makafiri, kama vile Wakomunisti, wanakanusha maalumati yaliyotangulia ili yasiwaongoze kumwamini Muumba, aliyempa Adam, amani iwe juu yake, maelezo yaliyotangulia ili kuasisi fikra ya mwanzo katika maisha haya na kisha mchakato wa kufikiri ukafuata. Hii ni kwa sababu kuuhisi uhalisia kwa ubongo hakuzalishi fikra bila maelezo yaliyotangulia kuelezea uhalisia unaohusika. Kuuhisi uhalisia na hisia pamoja na hisia pamoja na milioni hisia, bila ya kujali wingi wa aina ya hisia, huzalisha tu hisia, na hakuna fikra inayotokea kabisa. Bali ni lazima mtu awe na maelezo yaliyotangulia ambayo kwayo anaeleza uhalisia aliouhisi ili fikra itokee, na kisha mfuatano wa fikra, haswa fikra ya kwanza, hupelekea kwenye kumwamini Mwenyezi Mungu ambaye alimpa Adam, amani iwe juu yake, maelezo ya awali ...

4- Hii ni kuhusiana na maalumati yaliyotangulia. Ama kuhusu rai zilizotangulia, ni hukumu juu ya uhalisia ambao hapo awali ulitolewa na mtu, ima kwa kufanya kwake mchakato wa kifikra na hukumu yake juu ya uhalisia, au kupitia kupokea hukumu hizo kutoka kwa wengine kwa mafundisho au kusoma ... nk, maoni yaliyotangulia ni fikra juu ya uhalisia.

5- Kwa hivyo, tofauti kati ya maalumati yaliyotangulia na maoni yaliyotangulia inaweza kufupishwa katika tofauti kuu mbili:

Kwanza: Maoni yaliyotangulia ni fikra za awali za mtu ambazo ni hukumu juu ya uhalisia unaochunguzwa, kwa ujumla au kwa sehemu. Ama maalumarti yaliyotangulia, ndiyo yanayoweza kutumika kueleza uhalisia bila ya kuuhukumu, bali kuufasiri tu, na ni miongoni mwa mambo ya kuzalisha bila kwayo uzalishaji fikra hauwezi kufanywa.

Pili: Maoni yaliyotangulia ni hukumu kabla kuhusu uhalisia tunaotaka kuutafakari, ili kupata hukumu sahihi kwa maoni ya mwenye kufikiri, si sawa kutumika katika mchakato wa kimantiki. Kinachotumiwa ni maalumati tu yaliyotangulia, hivyo kuzuia kuwepo na kuingilia kati kwa maoni wakati wa mchakato wa kufikiri. Ikiwa maoni yaliyotangulia (kuhusu uhalisia) yalitumiwa inaweza kusababisha makosa katika utambuzi, kwa sababu yanaweza kutawala juu ya maelezo, na kupelekea tafsiri yake potofu, na hivyo makosa kutokea katika utambuzi. Hivyo basi, ni muhimu kutambua tofauti kati ya maoni yaliyotangulia na maalumati yaliyotangulia; ambapo, maalumati pekee ndio hutumika na sio maoni juu ya uhalisia unaopaswa kuchunguzwa... Imetajwa katika kitabu, cha at-Tafkeer, uk 21-3 (Katika ufafanuzi wa njia ya kimantiki (ya kufikiri). ), tofauti inapaswa kufanywa kati ya maoni yaliyotangulia tunayoyabeba juu ya jambo na maalumati yaliyotangulia juu yake au yanayohusiana nayo. Katika njia ya kimantiki, ni jambo lisilo budi kuwa hakuna maoni yaliyopo kuhusu uhalisia, bali cha muhimu ni uwepo wa maalumati yaliyotangulia kuhusu hilo au kuhusiana nalo. Kwa hiyo kinachopaswa kuwepo ni maalumati na sio maoni...)

6- Ifuatayo ni mifano miwili ya kuweka wazi yaliyotajwa juu:

a- Kwa mfano, ikiwa kitabu katika lugha ya kale ya Kisiria kitapewa mtu asiye na maalumati yaliyotangulia kuhusu lugha ya Kisiria, na hisia zake zote zikafanywa kuangukia kitabu hicho, kwa kuona na kugusa, na hii ikarudiwa mara milioni, bado hataweza kuelewa hata neno moja la kitabu isipokuwa apewe maalumati yanayofaa kuhusu lugha ya Kisiria. Baada ya hapo, ataanza kufikiri na kuelewa... Sio sahihi kusema hii ni maalum kwa lugha; na zimevumbuliwa na mwanadamu, kwa hivyo zinahitaji maalumati kuzihusu. Hii ni kwa sababu mada ni mchakato wa kimantiki, na uendeshaji wake ni mchakato wa akili, iwe katika utoaji hukumu, au katika kuelewa maana au katika kuelewa uhakika (Haqeeqah). Kwa hivyo, mchakato wa kimantiki ni mmoja katika kila kitu.

b- Ukitaka kujadili suala la kisiasa ili kupata maoni sahihi kuhusiana nalo, iwe kwa mfano, suala la Uturuki kuingilia matukio ya Libya, kutuma wapiganaji mamluki na kumuunga mkono al-Sarraj na serikali ya maridhiano na silaha na habari ... na kulikuwa na maoni ya hapo awali kwamba uungaji mkono wa Erdogan kwa vikosi vya serikali ya maridhiano ni kwa sababu ya mapenzi yake kwa Waislamu na wasiwasi wake kwa watu wa Libya na kwa sababu anaunga mkono harakati za Kiislamu za kisilaha na kuwapa msaada. .. nk., maoni haya ni hukumu juu ya suala unalotaka kulijadili na sio tu maalumati yaliyotangulia kulihusu, na uhalali wa utafiti unakuhitaji kuachana na maoni haya ya hapo awali na kulitafiti suala hilo ndani ya ushahidi wa kisiasa unaopatikana kwa umakini... na kisha kufikia maoni sahihi juu ya suala hilo.

Nataraji ufafanuzi huu utatosheleza, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwingi wa Hekima na Mjuzi Zaidi.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

04 Ramadhan 1442 H

16/04/2021 M

Link ya jibu hili kutoka kwa ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu