Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Hadith «إِنَّ الإِسْلامَ يَجُبُّ مَا كَانَ قَـبْلَهُ» “Hakika Uislamu Hufuta Yale Yalikuwa Kabla Yake”
Kwa: Salah Fawzi
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Ndugu Mpendwa, salamu njema kwako,

Katika kitabu, Kielelezo cha Katiba, Juzuu I, Kifungu 95

cha eleza yafuatayo:

(Ama kushughulika na kesi zinazodhuru Uislamu na Waislamu, hii ni kwa sababu Mtume aliamuru kuuawa kwa watu wachache waliosababisha madhara kwa Uislamu na Waislamu katika zama za Jahiliyyah baada ya ufunguzi wa Makka, na hivyo waliuawa hata kama walijifunga kwenye mapazia ya Al-Kaaba, kwa kujua kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, "إن الإسلام يجب ما قبله" “Hakika Uislamu Hufuta Yale Yalikuwa Kabla Yake” (imepokewa na Ahmad na Al-Tabarani kutoka kwa Amr b. Al-As); kwa maneno mengine, yeyote anayeudhuru Uislamu na Waislamu haingii katika riwaya hii)

Nimechunguza uhalisia wa watu hawa na nikagundua kuwa baadhi yao walikuwa Waislamu na wakaritadi na wengine hawakusilimu na waliuawa. Kwa hivyo, ambaye alikuwa Muislamu na akaritadi, kanuni msingi ni kwamba ataadhibiwa kwa uasi wake, na atakayebakia kuwa mshirikina na akawa miongoni mwa wanaoudhuru Uislamu na Waislamu ataadhibiwa kwa kifo au atasamehewa, kwa mujibu wa Imam (kiongozi) wa Waislamu anavyoona inafaa, kama ilivyoelezwa hapo juu katika kifungu hicho. Lakini katika hali zote mbili, Hadith: “Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake” haiwahusu, kwa sababu tunachojua ni kwamba Hadith: "إن الإٍسلام يجب ما قبله" “Hakika Uislamu Hufuta Yale Yalikuwa Kabla Yake” inawahusu wale ambao wamesilimu karibuni. Sasa kwa nini Hadith hii inanukuliwa kama dalili katika kifungu hiki, ikijulikana kuwa baadhi ya maswahaba walitumia upanga na kuwauwa Waislamu, kama vile Khalid bin Al-Walid? Na Wahshi bin Harb, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na Mtume (saw) hakuwafanya lolote baada ya kusilimu?

Barak Allah fik, Mwenyezi Mungu aziongoze hatua zako, na akuruzuku ushindi kupitia mikono yake. Salah Fawzi - Al-Quds Al-Sharif

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Inaonekana kuna mkanganyo katika kuelewa suala hilo, kama Hadith ya Mtume (saw) ambayo ilisimuliwa na Ahmad na al-Tabarani kutoka kwa Amr ibn Al-Aas «إِنَّ الإِسْلامَ يَجُبُّ مَا كَانَ قَـبْلَهُ» “Hakika Uislamu Hufuta Yale Yalikuwa Kabla Yake.” Inaashiria kuwa mtu yeyote anayesilimu kutoka kwa makafiri, chochote alichokifanya kabla ya Uislamu kuzingatiwa kama hakikutokea, yaani, hatawajibishwa kwa kile alichofanya kabla ya Uislamu. Kwa hivyo, kuingia katika Uislamu hufuta dhambi ambalo alikuwa amelifanya kabla ya Uislamu kwa sababu Uislamu unafuta kile kilichokuwa kabla yake ... lakini ukweli kwamba Mtume (saw) wakati wa ufunguzi wa Makka (aliruhusu damu kumwagwa (yaani Kuuwa) ya watu wachache ambao walikuwa wakiudhuru Uislamu na Waislamu katika nyakati za kabla ya Uislamu, damu yao iliruhusiwa kumwagwa (yaani kuuwawa kwao) hata kama wananing’inia mapazia ya Ka'ba), ambayo inaeleweka kwamba watabaki kuwajibika kwa kile walichowadhuru kwacho Waislamu, hata kama wamesilimu, kwa sababu maneno ya Mtume (saw): (وإن تعلقوا بأستار الكعبة) “Hata kama wananing’inia katika mapazia ya Ka’ba”. Hii yaashiria kwamba Mtume (saw) hakufanya takhsisi kusilimu kwao, bali aliamuru kuuwawa kwa hali yoyote. Tunafahamu kutokana na hilo kwamba wale wanaoudhuru Uislamu na Waislamu wataadhibiwa kwa yale wanayoyafanya, hata kama watasilimu, hivyo Hadith ya Mtume (saw): «إِنَّ الإِسْلامَ يَجُبُّ مَا كَانَ قَـبْلَهُ» “Hakika Uislamu Hufuta Yale Yalikuwa Kabla Yake.” Haiwajumuishi wao, kwani wako wako nje ya hadith hii, ikimaanisha kuwa madhara yoyote waliyoyasababisha kwa Uislamu na Waislamu, hafutwi na Uislamu, bali watawajibika kwayo, na mambo yao baada ya hapo ni juu ya Imam (kiongozi), akipenda, anawasamehe, na akipenda, anawaadhibu.

Uhalali wa ufahamu huu inaashiriwa kwa yale aliyoyapokea Al-Nasa’i katika Sunan yake kutoka kwa Mus’ab bin Sa’d kutoka kwa babake, aliyesema:

«لَمَّا كَانَ يَوْمُ فَتْحِ مَكَّةَ أَمَّنَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ النَّاسَ إِلَّا أَرْبَعَةَ نَفَرٍ وَامْرَأَتَيْنِ وَقَالَ اقْتُلُوهُمْ وَإِنْ وَجَدْتُمُوهُمْ مُتَعَلِّقِينَ بِأَسْتَارِ الْكَعْبَةِ عِكْرِمَةُ بْنُ أَبِي جَهْلٍ وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ خَطَلٍ وَمَقِيسُ بْنُ صُبَابَةَ وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعْدِ بْنِ أَبِي السَّرْحِ فَأَمَّا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ خَطَلٍ فَأُدْرِكَ وَهُوَ مُتَعَلِّقٌ بِأَسْتَارِ الْكَعْبَةِ فَاسْتَبَقَ إِلَيْهِ سَعِيدُ بْنُ حُرَيْثٍ وَعَمَّارُ بْنُ يَاسِرٍ فَسَبَقَ سَعِيدٌ عَمَّاراً وَكَانَ أَشَبَّ الرَّجُلَيْنِ فَقَتَلَهُ وَأَمَّا مَقِيسُ بْنُ صُبَابَةَ فَأَدْرَكَهُ النَّاسُ فِي السُّوقِ فَقَتَلُوهُ وَأَمَّا عِكْرِمَةُ فَرَكِبَ الْبَحْرَ فَأَصَابَتْهُمْ عَاصِفٌ فَقَالَ أَصْحَابُ السَّفِينَةِ أَخْلِصُوا فَإِنَّ آلِهَتَكُمْ لَا تُغْنِي عَنْكُمْ شَيْئاً هَاهُنَا فَقَالَ عِكْرِمَةُ وَاللَّهِ لَئِنْ لَمْ يُنَجِّنِي مِنْ الْبَحْرِ إِلَّا الْإِخْلَاصُ لَا يُنَجِّينِي فِي الْبَرِّ غَيْرُهُ اللَّهُمَّ إِنَّ لَكَ عَلَيَّ عَهْداً إِنْ أَنْتَ عَافَيْتَنِي مِمَّا أَنَا فِيهِ أَنْ آتِيَ مُحَمَّداً ﷺ حَتَّى أَضَعَ يَدِي فِي يَدِهِ فَلَأَجِدَنَّهُ عَفُوّاً كَرِيماً فَجَاءَ فَأَسْلَمَ وَأَمَّا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعْدِ بْنِ أَبِي السَّرْحِ فَإِنَّهُ اخْتَبَأَ عِنْدَ عُثْمَانَ بْنِ عَفَّانَ فَلَمَّا دَعَا رَسُولُ اللَّهِ ﷺ النَّاسَ إِلَى الْبَيْعَةِ جَاءَ بِهِ حَتَّى أَوْقَفَهُ عَلَى النَّبِيِّ ﷺ قَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ بَايِعْ عَبْدَ اللَّهِ قَالَ فَرَفَعَ رَأْسَهُ فَنَظَرَ إِلَيْهِ ثَلَاثاً كُلَّ ذَلِكَ يَأْبَى فَبَايَعَهُ بَعْدَ ثَلَاثٍ ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَى أَصْحَابِهِ فَقَالَ أَمَا كَانَ فِيكُمْ رَجُلٌ رَشِيدٌ يَقُومُ إِلَى هَذَا حَيْثُ رَآنِي كَفَفْتُ يَدِي عَنْ بَيْعَتِهِ فَيَقْتُلُهُ فَقَالُوا وَمَا يُدْرِينَا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا فِي نَفْسِكَ هَلَّا أَوْمَأْتَ إِلَيْنَا بِعَيْنِكَ قَالَ إِنَّهُ لَا يَنْبَغِي لِنَبِيٍّ أَنْ يَكُونَ لَهُ خَائِنَةُ أَعْيُنٍ»

“Siku ya ufunguzi wa Makka, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa msamaha kwa watu, isipokuwa wanaume wanne na wanawake wawili. Akasema: Wauweni, hata mkiwakuta wananing'inia pazia za Ka'aba. (Walikuwa) 'Ikrimah bin Abi Jahl, 'Abdullah bin Khatal, Miqyas bin Subabah na 'Abdullah bin Sa'd bin Abi As-Sarh. Abdullah bin Khatal alinaswa akiwa ananing'inia pazia za Ka'aba. Sa'id bin Huraith na 'Ammar bin Yasir wote wakamkimbilia, lakini Sa'id, ambaye alikuwa mdogo wa hao wawili, alifika hapo mbele ya 'Ammar, na akamuua. Miqyas bin Subabah alikamatwa na watu sokoni, na wakamuua. 'Ikrimah alisafiri baharini, na akashikwa na tufani. Wahudumu wa meli wakasema: 'Muelekeeni Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi, kwani miungu yenu (ya uwongo) haiwezi kukusaidia chochote katika hali hii.' 'Ikrimah akasema: 'Wallahi, kama hakuna kitu kilichokuja kuniokoa baharini isipokuwa ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu basi hakuna kitu chengine kitakachoniokoa ardhini. Ewe Mwenyezi Mungu, nakuahidi kwamba ukiniepusha na tatizo hili nitakwenda kwa Muhammad [saw] na kuweka mkono wangu ndani yake, na nina yakini kwamba nitamkuta ni mkarimu na mwenye kusamehe. Basi akaja, akasilimu. ‘Abdullah bin Sa’d bin Abi Sarh alijificha kwenye nyumba ya ‘Uthman bin Affan, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipowaita watu watoe kiapo chao cha utiifu, alimleta na akamsimamisha mbele ya Mwenyezi Mungu. Mtume [saw]. Akasema (Uthman): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kubali kiapo cha 'Abdullah.' Akainua kichwa chake na kumtazama mara tatu, akikataa utiifu wake kila mara, kisha akakubali utiifu wake baada ya mara tatu. Kisha akawageukia Maswahaba zake na kusema: Je! Wakasema: Hatukuwa tunajua yaliyomo moyoni mwako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kwa nini hukutuonyesha ishara kwa macho yako?' Akasema: "Haimfai Mtume kuwa macho yake yakhini."

Mtume (saw) aliwataka Waislamu wamuue Abdullah bin Abi al-Sarh ingawa alikuwa amekuja kwake kama Muislamu akiomba kutoa kiapo cha utiifu. Hii inaashiria kuwa damu ya watu hawa iliruhusiwa kumwagwa kwa ukamilifu wake, hivyo kuingia kwao katika Uislamu hakuwakinga na hilo, bali suala lao linarudi kwa Imam (kiongozi), na akitaka, anawaadhibu, na akipenda anawasamehe... Hivyo, ukweli kwamba Mtume (saw) hakuwaadhibu wale kutoka kwa makafiri waliosilimu na walikuwa wakiwadhuru Waislamu, kama ilivyo kwa Ikrimah bin Abi Jahl, kwa mfano itajumuishwa chini ya msamaha wa Imam (kiongozi), kama ilivyoelezwa katika kitabu “Taasisi za Dola katika Khilafah”: (Na kwa kuwa Mtume (saw) aliwasamehe baadhi yao baadaye, kama vile Mtume alivyomsamehe Ikrimah bin Abi Jahl. Hivyo basi, inajuzu kwa Khalifa kusimamisha kesi dhidi ya watu hawa au kuwasamehe).

Natumai kuwa hili litamaliza mkanganyiko katika kuelewa suala hili.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

17 Rabi ul Awwal 1445 H

2/10/2023 M

Link ya jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu