Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Majazi Kiasili Yanaweza kuwa Katika Nomino (Jina) Jumla Pekee

Kwa: Tariq Abu Oraiban (Abu Ali)

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu Alaikum Sheikh wetu, na Mwenyezi Mungu akusaidie kwa lile limridhishalo Allah na Mtume wake.

Niruhusu niulize swali, licha ya shughuli zako nyingi, lakini inatosha kwangu kuwa wewe ndiye unaye aminiwa kwa kujibu:

Katika kitabu cha Utambulisho wa Kiislamu Juzuu ya 3, imetajwa kuwa majazi hayawezi kuwa katika herufi, na pia imetajwa kuwa aina mojawapo ya utekelezwaji wa majazi ni ziada, na kutoa mfano, ambao ni aya hii:

 [لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ]

“…hapana kitu kama mfano wake…” [Ash-Shura: 11[. Hapa herufi (ك) (kaaf) ni ziada, sasa je hii si majazi katika herufi? Tafadhali fafanua kadhia hii, Mwenyezi Mungu akujazi kheri.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Kamwe haikutajwa katika kitabu Utambulisho wa Kiislamu kuwa majazi hayafanyiki katika herufi, bali imeelezwa kuwa majazi kwa dhati yake yaweza tu kuwa katika nomino jumla na hayawezi kuwa katika herufi au kitendo katika vigawanyo vyake vyote, wala kuvuliwa katika vigawanyo vyake vyote, wala nomino halisi. Kimsingi majazi hayawezi kuwepo katika yote haya, lakini yanakuwepo kwayo kama natija. Imefafanuliwa katika kitabu hicho kwa nini majazi katika vitu hivi kimsingi hayapo na kwamba yanakuwepo tu kama natija.   

Na nakunukulia yale yaliyo elezwa kuhusiana nayo katika kitabu Utambulisho wa Kiislamu Juzuu 3, katika mlango wa "Maana Halisi na Majazi":

(Majazi katika maneno yanaweza kuwa katika dhati, yaani asili, na yanaweza kuwa katika natija. Majazi katika dhati yanaweza tu kuwa katika nomino jumla yanayo ashiria dhati halisi ambayo hutekelezeka kwa vitu vingi pasi na mazingatio yoyote kwa sifa nyinginezo, kama neno 'simba' kwa mtu shujaa, na neno 'kuuwa' kwa kipigo kikali, na hayawezi kuwa kwa mengine yasiyo kuwa hayo. Na mambo ambayo kwayo majazi kimsingi hayawezi kuwepo ni: 

Mojawapo: herufi. Majazi hayawezi kuwa katika herufi kwa sababu haiashirii maana yake kipeke yake, bali haileti maana isipokuwa kwa kutaja utumizi wake, kwa hivyo kwa kuwa haileti maana kipeke yake, majazi hayawezi kuwepo ndani yake, kwa sababu kuwepo kwake ni tagaa la maneno kutoa maana yenye faida. Na ama natija ya kuwepo majazi katika herufi, yaweza kuwa kwa kutumia neno lililo ambatanishwa nayo kimajazi, hapo majazi hayo hupanuka kutoka katika maneno yaliyo ambatanishwa kwa herufi hizo, kama maneno ya Mwenyezi Mungu Ta'ala:  

 [فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُواً وَحَزَناً] “Basi wakamuokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni …”, kwa kuwa kutoa ufafanuzi wa kumchukua kupitia kuwa adui ni majazi, hivyo kutumika kwa herufi ya illah (لِ) pia ni majazi, hivyo majazi yalikuja katika herufi kufuatia kile kilicho ambatanishwa nayo, lakini majazi hayo kiasilia hayakuwepo katika herufi hiyo.

Pili: kitenzi katika vigawanyo vyake vyote, na nomino iliyo vuliwa katika vigawanyo vyake vyote, kama mpigaji na mfano wake, kwa sababu kitenzi hicho na nomino iliyo vuliwa kwacho hufuata asili yake ambayo ni endelevu ima iwe katika maana yake halisi au majazi. Hivyo, kumwita mtu mpigaji baada au kabla ya kupiga ni majazi, kwa sababu kutumia kipigo katika hali hii kama kusema: "fulani ana kipigo" ni majazi na sio halisi.

Tatu: nomino halisi, kwa sababu ikiwa imekarabatiwa (مُرْتَجَل) au kubadilishwa bila ya uhusiano (na sifa), hapana shaka kuwa hayo si majazi, na ikiwa imebadilishwa kwa uhusiano kama ikiwa mtu atamwita mwanawe Mubarak ikimaanisha aliye barikiwa kwa baraka iliyo fuatana na mimba au mazazi yake, pia itakuwa si majazi, kwa sababu ikiwa itakuwa ni majazi basi atazuiwa kumwita baada ya kutoweka kwa uhusiano huo, na hali (ya majina) haiko hivyo ambayo yaonyesha kuwa sio majazi) Mwisho.

Ni wazi kutokana na nasi hii kuwa majazi yapo ndani ya herufi ila hayapo kimsingi, yaani, sio kiasili. "kwa sababu herufi haileti maana kipeke yake bali haileti maana isipokuwa kupitia kutaja kusudio la utumizi wake, kwa hivyo kwa kuwa haileti maana kipeke yake, majazi hayawezi kuwepo ndani yake kwa sababu kuwepo kwake ni tagaa la maneno kutoa maana yenye faida" lakini endapo maneno yaliyo ambatanishwa na herufi yatatumika kimajazi hapo majazi hayo yatapanuka hadi kwa herufi hizo, kwa hivyo majazi katika herufi yanafuata yale yaliyo ambatanishwa nayo.

Sasa tuje katika mfano ulioutaja katika swali hili kuhusu uwepo wa majazi katika herufi, ambapo imeelezwa katika kitabu cha Utambulisho wa Kiislamu Juzuu 3 katika mlango "Maana Halisi na Majazi": pindi unapo zungumzia matumizi ya majazi na aina zake, ambapo yafuatayo yametajwa pamoja na aina ya tisa:

(Aina ya tisa: ziada, na hilo ni pindi mazungumzo yangali yanaweza kupangiliwa vizuri kupitia kuondoa neno lake moja, hivyo wanahukumu hiyo kuwa ni ziada kama maneno ya Mwenyezi Mungu Ta'ala

 [لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ] “…hapana kitu kama mfano wake…”]Ash-Shura: 11[, inamaanisha : (لَيْسَ مِثْلَهُ شَيْءٌ) hakuna mfano wake; hii inaitwa majazi ziada, kwa sababu herufi (ك) (kaaf) ni ziada, kwa kuwa lengo lilikuwa kukataa mithili sio mithili ya mithili, kwa sababu (ك) (kaaf) humaanisha mithili, hivyo basi inawajibisha mithili kwa Mwenyezi Mungu Ta'ala na hili haliwezekani, hivyo (ك) (kaaf) ni lazima iwe ni ziada ili kuthibitisha zaidi.) Mwisho.

Katika mfano huu, majazi katika herufi (ك) (kaaf) katika maneno ya Mwenyezi Mungu Ta'ala كَمِثْلِهِ "kama mithili yake" sio majazi kidhati yake, yaani, kiasili lakini majazi yalikuwa katika natija; hii ni kwa sababu matumizi ya herufi (ك) (kaaf) ndio yaliyo na majazi hayo, na yanapanuka kutoka kwayo hadi herufi (ك) (kaaf). Hivyo basi herufi (ك) (kaaf) hutoa faida ya mithili kwa maana yake halisi, lakini ikiwa herufi (ك) (kaaf) katika sentensi hii itafanywa kutoa maana yake halisi, sentensi hii itakuwa na makosa kwa sababu hapo itamaanisha kuwa kuna mithili kwa Mwenyezi Mungu Ta'ala na kuwa kitu hichi mithili sio kama kitu chengine yaani, hakifanani na kitu chengine. Lakini haya sio makusudio ya ayah hii, bali maana ya ayah hii ni kuwa hakuna mithili ya Mwenyezi Mungu."

Hivyo basi, ayah hii yamaanisha: (لَيْسَ مِثْلَهُ شَيْءٌ) "hakuna kitu mithili yake", na maana hii ya ayah yawajibisha kuielekeza herufi (ك) (kaaf) kutoka kutoa maana ya mithili hadi kutoa faida ya kusisitiza yaani kuielekeza kutoka maana halisi hadi maana ya kimajazi kwa sababu ya muundo huo, yaani, kwa sababu ya sentensi hiyo. Neno "كمثله" "kama mithili yake" kihakika linaashiria "mithili ya mithili", lakini kimajazi linaashiria "mithili" kutokana na natija ya kuambatanishwa ziada pekee yaani, kuichukulia herufi (ك) kaaf kuwa ziada.  Maana hii ya kimajazi ya neno "كمثله" "kama mithili yake" inawajibisha kuwa herufi (ك) kaaf izingatiwe kama ziada, na kuichukulia kuwa ziada ni majazi kwa sababu imeelekezwa kutoka katika maana yake asili, ambayo ni mithili ya sio mithili, ambayo inapaswa kuwa ziada kwa ajili ya kusisitiza. Majazi katika neno "mithili yake" katika sentensi yote yamepanuka hadi herufi (ك) kaaf yaani, yamepanuka kutoka viambatanishwa vya herufi hiyo hadi herufi hiyo.      

Tamati ni kuwa majazi yaliyotajwa katika ayah

[لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ] “…hapana kitu kama mfano wake…”, kwa kuikadiria herufi (ك) kaaf kuwa ziada ni natija ya majazi ambayo yaweza kuwepo katika herufi, kwa sababu ziada ya herufi (ك) kaaf iliwajibishwa na sentensi ("… hakuna kitu mithili yake…"); hivyo basi, herufi (ك) kaaf ilielekezwa kutoka kutoa maana ya mithili kutokana na muundo ambao kwao herufi (ك) kaaf iliekwa, yaani, majazi yalitokea ndani yake kwa sababu ya sentensi hiyo ilimo wekwa ndani yake.

Nataraji jambo hili liko wazi sasa.

Tafadhali pokea salamu zangu.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

28 Rabi’ I 1441

Jumatatu, 25 Novemba 2019

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:31

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu