Masuluhisho Yaliyopendekezwa kwa Gaza ya baada ya Vita
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Huku vita vya mauaji ya halaiki vya umbile la Kiyahudi, kwa uungaji mkono muovu wa Marekani ya Magharibi, vikiendelea dhidi ya watu wa Gaza kwa zaidi ya miezi mitano, na wahanga wake kufikia zaidi ya mashahidi na majeruhi 100,000, pamoja na kuangamizwa kwa sehemu kubwa ya majengo yake, kuna mazungumzo mengi kuhusu miradi ya massuluhisho ya kile kitakachokuja baada ya vita vya Gaza na jinsi mambo yatakavyokuwa kisiasa kulingana na mipango ya dola za kikoloni zikiongozwa na Marekani.