Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Mapinduzi ya Kijeshi Nchini Guinea

(Imetafsiriwa)

Swali:

(Baraza la Kijeshi la Guinea lilitangaza kuwa litaanza, kuanzia kesho, Jumanne 14/9/2021, mfululizo wa mikutano na vikosi vya kisiasa, asasi za kiraia na wawakilishi wa kampuni za madini, ikiwa ni maandalizi ya kuunda serikali nchini ... Dar Al-Hilal 12/9/2021) mnamo Jumapili jioni, 5/9/2021, Conakry-Guinea ilishuhudia mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Kanali wa Kikosi Maalum Mamady Doumbouya, ambaye alitangaza kupitia hotuba ya runinga kukamatwa kwa Rais wa nchi hiyo Alpha Conde, kuvunjwa kwa Bunge na serikali, kusitishwa kwa katiba na kufungwa kwa mipaka. Ni nani aliye nyuma ya mapinduzi haya? Je! Yanahusiana na mzozo wa kimataifa juu ya nchi hii?

Jibu:    

Ili kufafanua maoni sahihi juu ya suala hili, tunakagua mambo yafuatayo:

1- Kiongozi wa mapinduzi, Kanali Mamady Doumbouya, alisema kwenye runinga ya serikali ya Guinea kufuatia mapinduzi mnamo Jumapili jioni, 5/9/2021: (Tuliamua kuvunja taasisi na serikali na kufunga mipaka ya ardhi na anga, na kuwaelekea wale wanaopenda kumaliza kazi zao katika hali ya kawaida) na akatoa wito (wanajeshi wakae katika kambi zao) na kushikilia (serikali inahusika na hali mbaya, unyanyasaji wa haki, kukandamiza raia, kutoheshimu demokrasia na siasa za maswala ya kiutawala pamoja na umaskini uliokithiri na ufisadi), alisema (tuliamua kumkamata Rais Alpha Conde, (mwenye umri wa miaka 83). Na kutangaza kubadili maafisa wa jeshi kwa magavana wa majimbo. Siku iliyofuata, kiongozi wa mapinduzi aliahidi, katika mazungumzo yaliyopeperusha katika runinga, pia (kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kusimamia kipindi cha mpito).

Hakukifafanua kipindi hicho cha mpito. Aliwaita mawaziri na maafisa wakuu wa serikali kwenye mkutano naye na kuwatishia wale ambao walishindwa kuhudhuria kwamba atachukulia kama "uasi dhidi ya Bunge la Kitaifa na Kamati ya Demokrasia", ambalo ni jina lililochaguliwa na Kikosi Maalum kujirejelea. Wanajeshi bila heshima waliwaongoza maafisa hao hadi makao makuu ya jeshi katika mji mkuu, Conakry. Alisema, "Hatutakabidhi siasa kwa mtu mmoja tena, lakini tutaikabidhi kwa watu," na akasema, "Sote tutakaa chini kuandika katiba ambayo inazingatia ukweli ambao unaweza kutatua shida zetu" ... Yote hii inaonyesha hamu yake ya kutawala sasa na baada ya kipindi cha mpito.

2- Wacha tupige hatua nyuma na kukumbuka kile kilichotokea mwishoni mwa 2008, wakati kikundi cha kijeshi kilichoongozwa na Kapteni Moussa Camara kilifanya mapinduzi kwa saa nne baada ya kutangazwa kifo cha Rais wa Jamhuri ya Guinea, Jenerali Lansana Conte. Halafu walitangaza kuwa (hawana nia ya kuendelea madarakani kwa zaidi ya miaka miwili hadi uchaguzi wa rais utakapofanyika mwishoni mwa 2010), na tukataja maelezo ya mapinduzi hayo katika jibu la swali tarehe 26/12/2008 na tukaelezea kuwa Amerika ilikuwa nyuma ya mapinduzi hayo, na hii ilithibitishwa baadaye. Kwa kweli, uchaguzi ulifanyika mnamo Novemba 2010 na Alpha Condé alishinda. Alikuwa akipinga utawala wa Jenerali Lansana Conte, kibaraka wa Ufaransa. Alpha Condé anajulikana (na anaelezewa kama mpinzani wa kihistoria, kwani alipinga serikali zote zilizopishana Guinea tangu uhuru wake mnamo 1958, na kupelekwa uhamishoni Ulaya. Kwa kuongezea, alihukumiwa kifo na kufungwa kabla ya kuingia madarakani mnamo 2010. Al-Jazeera 24/10/2015). Alionekana kama mkombozi wa Wa-Guinea kutoka kwa dhuluma iliyofanywa na vibaraka wa Ufaransa. Wakati wanajeshi wanaounga mkono Amerika walipofanya mapinduzi mnamo 2008, msimamo wake ulikuwa wastani kwao. Badala yake, aliwataka wafanye uchaguzi kama walivyoahidi. Hakika, uchaguzi ulifanyika na Alpha Conde alishinda. Alichaguliwa tena mnamo 2015 na muda wake unamalizika mnamo 2020. Hana haki ya kugombea muhula wa tatu kulingana na katiba, kwa hivyo aliirekebisha kwa kufanya kura ya maoni ya umma mnamo 2019; hii iliruhusu kufanyika kwa uchaguzi mnamo Oktoba 2020, ambao alishinda wakati wa maandamano ya upinzani dhidi ya kura ya maoni na uchaguzi, na pia tuhuma za udanganyifu. Walakini, Mahakama ya Katiba ilitoa uamuzi mnamo Disemba 2020 ikithibitisha ushindi wa Conde dhidi ya wapinzani wake ambao walikuwa wamewasilisha malalamiko kwake. Mtu huyo alikuwa akijiamini mwenyewe na alifurahia uungwaji mkono mkubwa, kwa hivyo hakuwazia kuwa atapinduliwa, kwani jeshi lilikuwa pamoja naye.

3- Kisha mapinduzi haya yakafanyika dhidi yake mnamo 5/9/2021 na akakamatwa. Majibu ya kimataifa na ya kikanda kwa mapinduzi yaliyotokea yalifafanua ni nani alikuwa nyuma ya mapinduzi haya:

A- Amerika ilijibu vikali kuhusu mapinduzi haya ya kijeshi. Taarifa iliyotolewa na wizara yake ya mambo ya nje, kupitia kwa msemaji wake, Ned Price, ambaye alisema: "Amerika inalaani matukio ya leo huko Conakry. Vurugu na hatua zozote za ziada za kikatiba zitapunguza tu matarajio ya Guinea ya amani, utulivu, na ustawi." Taarifa hiyo iliongeza "Vitendo hivi vinaweza kupunguza uwezo wa Amerika na washirika wengine wa kimataifa wa Guinea kuunga mkono nchi hiyo wakati inapita njia kuelekea umoja wa kitaifa na mustakabali mwema kwa watu wa Guinea."

“Tunasisitiza pande zote ziache vurugu na juhudi zozote zisizoungwa mkono na Katiba na zizingatie sheria. Tunasisitiza himizo letu kwa mchakato wa mazungumzo ya kitaifa kushughulikia haja za raia kwa utulivu na kwa uwazi kuwezesha njia ya amani na ya kidemokrasia kwa Guinea kufikia uwezo wake kamili ... Tovuti rasmi ya Wizara ya Kigeni ya Amerika, Reuters 6/9/2021," alisema, akionyesha kwamba mapinduzi haya hayana masilahi ya Amerika, tofauti na mapinduzi ya serikali mnamo 2008, ambayo majibu yake yalikuwa dhaifu na haikuyalaani kabisa. Badala yake, ilisema wakati huo: "Tunafanya kazi na washirika wetu katika ukanda huo na nchi nyengine katika kanda hiyo na Jumuiya ya Afrika kuhamasisha taasisi za Guinea kuchukua hatua zote kuhakikisha mabadiliko ya amani na kidemokrasia". Maoni haya yalikuwa yakipendelea wanamapinduzi wakati huo. Lakini wakati huu ililaani mapinduzi na kuyazingatia kama vurugu na kutishia kupunguza msaada kwa Guinea na kudai uzingatiaji wa katiba, njia ya kidemokrasia na sheria, sio utawala wa jeshi.

B- Wakati Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ilitoa taarifa dhaifu na isiyo wazi baada ya mapinduzi ikisema: (Paris "inajiunga na wito wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kulaani jaribio la kutwaa mamlaka kwa nguvu" mnamo Jumapili na "kudai kurudi kwa utaratibu wa kikatiba" AFP 6/9/2021). Maoni haya ni ya kuliwaza maoni ya umma ambayo yanakataa mapinduzi, sio ya kikweli. Haikulazimisha kurudi kwa Rais Conde madarakani, na haikuwatishia waasisi wa mapinduzi kwa adhabu. Msimamo wake ulikuwa mtulivu kuliko wakati mapinduzi yalipofanyika nchini Mali dhidi ya kibaraka wake Ibrahim Keita; ilidai arudi madarakani, na ililaani mapinduzi ya Mali kwa viwango vya juu zaidi. Urais wa Ufaransa ulisema: (Rais Macron anafuatilia kwa karibu hali hiyo na analaani jaribio la uasi linaloendelea), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Le Drian alisema: (Ufaransa inalaani kwa nguvu kabisa tukio hili zito). Tumetaja maelezo ya mapinduzi ya Mali katika jibu la swali mnamo 1/9/2020. Lakini mapinduzi ya Guinea hayakuhukumiwa na urais wa Ufaransa, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa haikuilaani kando, lakini ilisema kwamba inajumuisha sauti yake kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ambayo inaonyesha kutokuwa na hamu kwa hukumu hii, na inaonekana kana kwamba inafuata kikundi hiki kisichofaa cha utawala! Yote hii inaonyesha kwamba Ufaransa ilikuwa nyuma ya mapinduzi ya hivi karibuni huko Guinea.

C- Ikiwa tutajifunza historia ya kiongozi wa mapinduzi, tutakuwa na hakika kuwa Ufaransa ilikuwa nyuma yake. Kama ilivyoripotiwa katika magazeti ya Ufaransa, kiongozi wa mapinduzi, Mamady Doumbouya, ambaye alizaliwa mnamo 1980, alisoma na kufunzwa katika Shule ya Jeshi huko Sumore, magharibi mwa Ufaransa, na kupata diploma katika masomo ya juu ya jeshi, na kupata kuaminika kwa maafisa wa Ufaransa. Alipandishwa cheo cha ukoplo, na alijiunga na jeshi la Ufaransa katika Jeshi la Kigeni, ambalo lilianzishwa hapo zamani mnamo 10/3/1831. Wakati huo huo, Doumbouya alishiriki katika Jeshi la Ufaransa katika vikosi kadhaa vya jeshi la Ufaransa katika nchi anuwai, kwa uaminifu kwa Ufaransa, hadi aliporudi Guinea baada ya miaka 15. Aliteuliwa mkuu wa vikosi maalum mnamo 2018, na mnamo 2019 alipandishwa cheo cha kanali. Habari ilianza kuvuja mwaka jana juu ya hamu ya kanali anayetaka kuongeza nguvu na ushawishi wa vikosi maalum anavyoongoza kwa gharama ya Wizara ya Ulinzi. Kulikuwa na habari mnamo Mei iliyopita juu ya yeye kupanga mapinduzi, ambayo alikamatwa, lakini serikali ilikanusha. Inaonekana kwamba haikuwa jaribio la mapinduzi, bali ni mahitaji ya kutenganisha vikosi vyake maalum kutoka kwa Wizara ya Ulinzi, na kwa sababu hii Rais Conde au serikali hawakuwa na sababu za kutosha juu yake, na hawakuweza kuyathibitisha na walipendelea kumweka chini ya usimamizi wao, kwani hakuweza kutenganisha Vikosi Maalum kutoka kwa Wizara ya Ulinzi na kuwa na chombo huru ambacho angeweza kutekeleza kile alichokusudia.

4- Mapinduzi hayo yalisababisha kupanda kwa bei ya aluminium katika masoko ya ulimwengu na kufikia bei yake ya juu kwa miaka kumi, kwa sababu ya hofu ya usumbufu wa usambazaji, ikizingatiwa kuwa Guinea ndio mzalishaji mkubwa wa bauxite ulimwenguni, ambayo hutumiwa katika uzalishaji wa aluminium. Kiongozi wa mapinduzi alijaribu kuwahakikishia washirika wa kigeni na wawekezaji kwamba viongozi wapya wa Conakry watadumisha ahadi zao kwao kuendelea na shughuli za kawaida nchini. (Baraza la kijeshi linaloongozwa na Kanali Mamady Doumbouya litakutana na wakuu wa vyama na viongozi wa madhehebu Jumanne ijayo, huku watakutana Jumatano na asasi za kiraia na wawakilishi wa kidiplomasia, na Alhamisi watakutana na wakuu wa kampuni za madini zinazofanya kazi nchini Guinea na kisha vyama vya waajiri. Guinea ni moja ya nchi tajiri katika madini ya bauxite ambayo hutumiwa katika utengenezaji wa aluminium, na ina migodi ya kuchimba chuma, dhahabu na almasi, lakini ni moja ya nchi masikini zaidi duniani. Mapinduzi nchini Guinea yalisababisha kupanda kwa bei ya aluminium katika masoko ya ulimwengu hadi viwango vyake vya juu kwa miaka, na Baraza la Jeshi lilitaka kuwahakikishia washirika wa Guinea kuwa shughuli za uzalishaji hazitakoma na ahadi hizo zitaheshimiwa ... Dar Al- Hilal 12/9/2021).

5- Inajulikana kuwa kampuni hizi hupora madini haya na madini mengine mengi nchini Guinea na haziachi kitu kwa watu wake, wakati wanateseka na umaskini, kukandamizwa na kuenea kwa magonjwa. Guinea inachukuliwa kuwa moja ya nchi tajiri zaidi na malighafi zake nyingi, lakini idadi ya watu ni miongoni mwa maskini zaidi ulimwenguni! Kumbuka kuwa idadi kubwa ya raia ni Waislamu. Lakini ni nchi ambayo ilitawaliwa na Ufaransa na ikapewa uhuru wake rasmi mnamo 1958, lakini ushawishi wa Ufaransa ulibaki ndani yake. Iliunda serikali, jeshi, watawala na kituo cha kisiasa na ilibaki kudhibiti uchumi na kuufanya utamaduni wake kuwa mkuu nchini. Amerika ilikuja kushindana na Ufaransa na kuiondoa huko na kuibadilisha kwa kupanua ushawishi wake, kupora utajiri wa nchi hiyo. Lengo la nchi za kibepari za Kimagharibi ni ukoloni wa Afrika tu, na hawavutiwi na mwamko wa nchi hiyo na maendeleo na kushughulikia shida za watu. Kushinda serikali, watawala au viongozi wa jeshi nchini hutumika kama njia ya ukoloni, kwa hivyo wamefarijika kutoka kwa kutuma majeshi yao kuimiliki kama zamani, kwa sababu ya kupatikana kwa uwezekano wa kupanua ushawishi wao na ukoloni kwa njia ya kununua watu binafsi katika vituo vya kisiasa au vya kijeshi. Utawala, watawala, au maafisa wanaposhindwa, hufanya mapinduzi ya kijeshi kama wakoloni wanavyotaka, kisha mlango hufunguliwa kwa ukoloni na kupanua ushawishi. Kwa hivyo, mzozo wa kimataifa utaendelea kuwaka kati ya mataifa ya kikoloni juu ya mataifa madogo, haswa barani Afrika. Watu hawawezi kuondoa uovu huu ulioenea isipokuwa kwa kurudi kwa Uislamu katika kutawala kwa kusimamisha Khilafah Rashida katika nchi moja au zaidi za Kiislamu, itakayowashinda wakoloni, kuzikomboa nchi zote kutokana na ukoloni wao, kurudisha utajiri kwa watu wake, kugawanya mapato yake juu yao, na kuwaamsha.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

"…Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [Ar-Rum: 4-5].                                               

6 Safar Al Khair 1443 H

13/9/2021 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu