Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Ukweli wa Shambulizi la Angani la Amerika la Hivi Karibuni Nchini Syria!
(Imetafsiriwa)

 Swali:

Katika toleo letu la tarehe 11/4/2018, juu ya mkutano wa Putin, Rouhani na Erdogan, lilieleza kuwa watatu hawa wanatekeleza maslahi ya Amerika nchini Syria ya kuweka utawala wa kisekula chini ya ushawishi wa Amerika. Hivyo basi, Putin anafanya kazi nchini Syria kwa mawasiliano na Amerika na kwa ajili ya kuihudumia. Ni yapi yaliyoko nyuma ya shambulizi la Amerika nchini Syria usiku wa leo licha ya ukweli kuwa Putin ana vikosi eneo la Tartous na Hameim? Ni vipi itafanya kazi kwa mawasialino na Amerika wakati Amerika inayashambulia majeshi yake nchini Syria? Na ni vipi kutakuweko na muungano kati ya Amerika, Uingereza na Ufaransa ilhali maslahi yao yanatofautiana? Tafadhali fafanua hili, Jazaka Allah Khair, na samahani kwa kasi ya swali. 

Jibu:

1-  Kwanza, nataka kusahihisha sehemu ya swali. Amerika haikushambulia maeneo ya Urusi nchini Syria. Hili liko wazi katika taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi asubuhi ya leo, 14/4/2018, bali ilishambulia pambizoni mwa maeneo yake na karibu sana nao, ambapo Urusi ilinyamaza kimya japokuwa inadai kuwa ndiye mmiliki na msimamizi wa nchi na watu wa Syria!

2- Mashambulizi hayo ya Amerika zaidi ni hatua za kinidhamu kwa Urusi kuliko kuwa tu ni shambulizi kwa silaha za kemikali za Syria. Takriban maeneo kumi yalishambuliwa macheo ya leo. Lakini, baadhi ya maoni ya wajuzi wa kijeshi katika vyombo vya habari asubuhi ya leo walisema kuwa machache kati ya maeneo haya ni viwanda vya kemikali au vituo vya utafiti, lakini mengi yao ni maeneo ya kijeshi.

3- Ama kuhusu kutiwa adabu Urusi; licha ya huduma zake nchini Syria kwa manufaa ya Amerika, Urusi ilighuriwa na kiburi kiasi. Ilijaribu kufanya matendo yake nchini Syria kwa mazingira ya kiburi kana kwamba ndiyo yenye kushikilia hatamu za uongozi nchini Syria, na ikapita mipaka iliyo ruhusiwa, mipaka ya kazi yake, ambayo ni kumakinisha ushawishi wa Amerika nchini Syria, na sio kuipiku Amerika. Hii ndio sababu shambulizi hilo lilifanywa zoni ya Urusi, karibu na maeneo yake ili kupunguza kimo cha Urusi. Na endapo itateleza tena na kufanya kazi yake nchini Syria ili kuibuka kama kitovu cha nguvu na ushawishi, basi Amerika itasimama mbele ya uso wake kwa nukta ya kuitusi, kama balozi wa Urusi jijini Washington alivyosema kuwa shambulizi hilo la Amerika lilikuwa ni matusi kwa Putin binafsi na wala si kwa Urusi pekee!   

4- Lakini ni kwa nini shambulizi hilo lililengwa kuitusi Urusi zaidi kuliko kuyashambulia maeneo ya Syria? Ni kwa sababu “kubweka” kwa Trump kulichukua siku chache tu kabla ya shambulizi hilo. Ilikuwa ni ujumbe kwa serikali (ya Syria) kuondoka maeneo yake; ndio sababu hasara zilikuwa za kuhusika hata ingawa makombora yaliyo rushwa yalikuwa zaidi ya makombora 100. Uzito wake haukuwa mgeni kwa serikali (ya Syria) kwani ishazoea kutusiwa. Hufedheheshwa na ishazoea kufedheheshwa, na hii ndio hali kwa vibaraka; mabwana zao hawaoni madhara ya kuwapiga kila maslahi ya mabwana zao yanapo hitaji hilo. Matukio mengi katika historia yanaonesha hili na Amerika ilifanya hili mwaka jana baada ya matukio ya Khan Shaykhun. Hivyo basi, hili si jipya kwa vibaraka, bali wamepewa “mafunzo” ya kukubali hili. Baya zaidi ni kuwa baada ya kichapo hicho, kibaraka huyo anasherehekea ushindi huo! Lakini, tunacho hitaji kuzingatia ni uzito wake juu ya Urusi, ambayo iliondoa vyombo vyake vingi, na kuondoka baadhi ya maeneo ili kukimbia shambulizi tarajiwa. Ingawa mashambulizi hayo yalikuwa karibu na maeneo yake na kwa kudai kwake kuwa ndiye msimamizi nchini Syria, haikuweza kutumia himaya yake ya angani kujibisha shambulizi hilo kama ilivyo tangaza Wizara ya Ulinzi ya Urusi leo mchana!    

5- Katika taarifa ya afisa wa Urusi asubuhi ya leo, alitangaza kuwa Urusi itawasilisha malalamishi kwa Baraza la Usalama, na kwa hakika iliwasilisha, na Baraza la Usalama liliamua kukutana leo saa tisa mchana kwa majira ya GMT. Yaani, Urusi ilifanya lile ambalo dola dhaifu hufanya, ambapo chaguo pekee lao wanapo kumbana na uvamizi ni kulalamika tu. Kwa hakika Urusi ilishambuliwa, ingawa kambi zake hazikulengwa.  Hii ni kwa sababu ilikuwa inazunguka na kuranda randa ovyo nchini Syria, ikijizuzua kwa hisia za ukubwa iliokuwa nao katika Umoja wa Kisovieti, kwa hivyo shambulizi hili, kama lilivyo tajwa juu, lilikuwa ni kwa ajili ya kuipunguza kimo chake, na kuiweka mahali pake inapostahili. Urusi haikusubutu kuchukua hatua ya kimada dhidi ya shamulizi hilo. Hivyo basi, ubwege wa kisiasa wa Urusi unaonesha; wanafanya juhudi zaidi nchini Syria, ilhali sio wenye usimamizi, uamuzi uko mikononi mwa Amerika. Hawakupata funzo kutoka kwa miaka yao mingi nchini Misri ambapo “kwa kipigo cha ncha ya kalamu” Sadat aliwafurusha nje ya Misri; hii ni kwa sababu Amerika ndiyo aliyokuwa msimamizi, lakini Warusi hawakutambua hili. Leo wamerudia tena hili hili nchini Syria; wanatekeleza vitendo vya kinyama kwa manufaa ya wengine, kutokana na chuki yao kwa Uislamu na Waislamu. Maafa haya, yanayo tekelezwa na Urusi, Amerika ikisimama nyuma yake; hayatafutika katika mabongo ya Waislamu, na mambo yatabadilika siku moja, twaomba iwe karibuni.

6- Lakini yaliyo tajwa katika swali hili kuhusu muungano kati ya Amerika, Uingereza na Ufaransa, kihakika sio muungano kwa sura ya kuunda muungano baina ya dola na kupingana na dola nyenginezo, bali, huku (kushiriki) kulikuwa kwa idhini ya Amerika, kama ilivyo tokea nchini Iraq na Syria, kwa kuundwa kwa muungano wa kimataifa chini ya kisingizio cha kupambana na ugaidi, ambapo Amerika ilikubali kuihusisha Uingereza na Ufaransa katika muungano huo. Tayari tumeshataja hili kwa kina katika matoleo yetu ya nyuma.

7- Lililo uchungu zaidi ni kuwa nchi zenye ushawishi duniani zinaingilia mambo ya biladi zetu na kuwa wasimamizi juu yake, huku sisi tukiwa hatuna dola inayo tuunganisha na kuregesha utukufu wetu. Vyenginevyo, Amerika ingetambua, kwa maneno na vitendo, namna ilivyo lipa (ada ya trafiki) ilipo ingia katika bahari ya Mediterenia kwenda kwa Gavana (Wali) wa dola ya Kiuthmani nchini Algeria. Na Ufaransa pia ingetambua namna ilivyo itisha msaada kwa Khalifah wa Waislamu, Suleiman Al-Qanoni, kumuokoa mfalme wake aliyetekwa nyara. Na Uingereza ingetambua namna ilivyokuwa ikiomba msamaha kwa Balozi wa dola ya Kiuthmani jijini London kwa kutusiwa Mtume na msanii mmoja. Na yote haya yalitokea wakati gani? Wakati ambao Khilafah Uthmaniya ilikuwa imefikia nukta yake ya udhaifu wa mwisho, ndipo ikakubali msamaha huo, vyenginevyo majibu yangekuwa makali zaidi.

Kila Muislamu ni lazima atoe bidii yake katika kufanya kazi na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah na hukmu ya Allah, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na hapo ndipo Uislamu na Waislamu watakuwa washindi, na ukafiri na makafiri watakuwa wadhalilifu.

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿

“…Na siku hiyo Waumini watafurahi* Kwa Nusra ya Allah, humnusuru amtakaye na Yeye ndiye Mwenye nguvu Mrehemevu.” [Ar-Rum: 4-5]

27 Rajab 1439 H

Jumamosi, 14/4/2018 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 21:20

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu