Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mdororo wa Kiuchumi Unaonukia, na Nuru ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Mwaka huu, tunapokabiliana na kupanda kwa bei, kuongezeka kwa gharama ya maisha, kupungua kwa akiba na kuongezeka kwa utovu wa usawa wa mapato, inaaminika sana kwamba uchumi wa dunia unaelekea kwenye mdororo na hali ya uchumi kwa mamilioni ya watu itakuwa mbaya zaidi. Ingawa muda halisi wa mdororo wa uchumi ni vigumu kutabiri, kuna mambo kadhaa ambayo yanaonyesha kwamba mdororo uko kwenye upeo wa macho.

Moja ya viashiria vikuu ni hali ya sasa ya soko la ajira, ambayo imekuwa ikionyesha dalili za udhaifu katika miezi ya hivi karibuni. Hata makampuni makubwa ya teknolojia kama Google na Amazon yaliondoa kazi 30,000 kwa pamoja zikitaja uchumi usio na uhakika. Zaidi ya hayo, kushuka kwa soko la nyumba na kupungua kwa akiba ya watumiaji ni ishara za mapema za mdororo ujao wa kiuchumi. Deni la kadi za mkopo limeongezeka kwa 15% katika mwaka uliopita, ongezeko kubwa zaidi katika zaidi ya miongo miwili, ikionyesha upotevu wa akiba na kutegemea zaidi deni ili kufidia kuongezeka kwa gharama ya maisha. Sababu nyingine inayoonyesha kushuka kwa uchumi kunakuja ni hali ya sasa ya soko la hisa. S&P 500 imekuwa ikikabiliwa na marekebisho makubwa katika miezi ya hivi karibuni, na wachambuzi wengi wanatabiri kuwa soko linaweza kuendelea kuanguka katika miezi ijayo. Zaidi ya hayo, soko la dhamana pia linaonyesha dalili za udhaifu huku mavuno kwenye bondi za muda mrefu yakishuka hadi viwango vya chini vya kihistoria.

Wataalamu wengi wanatabiri kuwa kushuka kujako kwa uchumi kutakuwa tofauti na siku zilizopita. BlackRock, meneja mkubwa zaidi wa mali duniani, ameonya kuhusu mdororo unaokaribia. Katika ripoti iliyopewa jina la 2023 Global Outlook, ilisema watunga sera hawataweza tena kuyanusuru masoko kama vile walivyofanya wakati wa kushuka kwa uchumi uliopita na itasababisha mtikisiko zaidi wa soko kuliko hapo awali. Hata BlackRock hivi majuzi imepunguza 3% ya wafanyikazi wake ikitoa mfano wa “mazingira ya soko ambayo hayajawahi kutokea.” Pia, Morgan Stanley, Benki ya Amerika, na Benki ya Deutsche zimeonya kuwa hisa za Marekani zinaweza kushuka kwa zaidi ya 20% mwaka huu kutokana na kuzorota kwa uchumi na hatari za pesa taslim zinazochochewa na ongezeko la viwango vya riba vya Hifadhi ya Shirikisho. Hata Benki ya Dunia ilisema kwamba “ukuaji wa kimataifa umepungua hivi kwamba uchumi wa dunia unakaribia kuporomoka kwa hatari.”

Katika mfumo wa kibepari, serikali ina uwezo wa kuchapisha sarafu inapohitajika ambayo inaweza kusababisha mfumko wa bei ikiwa usambazaji wa pesa utaongezeka kwa kasi sana. Kwa mfano, Marekani ilisukuma matrilioni ya dolari ili kuimarisha uchumi baada ya kuanguka kwa soko kutokana na COVID-19 na ilifanya vivyo hivyo mwaka wa 2008 baada ya soko la nyumba kuanguka. Baadaye, viwango vya riba vilipunguzwa hadi karibu sifuri ili kuanza ukuaji wa uchumi. Sasa, pamoja na kupanda kwa mfumko wa bei, Hifadhi ya Hazina ya Kifederali ya Marekani imepandisha viwango vya riba ili kudhibiti mfumko wa bei na kudhibiti usambazaji wa pesa. Tangu kuanguka kwa soko mnamo 2020 kutokana na COVID-19, takriban dolari trilioni 16 zimechapishwa kwa njia iso eleweka ili kusaidia mfumo dhaifu wa kiuchumi wa “karatasi za choo”.

Maumbile ya mzunguko wa panda shuka hizi ni ndio asili ya mfumo wa Kibepari. Kwa kiasi kikubwa, ukubwa na utokeaji mara kwa mara wa mizunguko hii inaweza kutofautiana, hata hivyo, katika miongo michache iliyopita utokeaji mara kwa mara wa matukio haya umeongezeka. Fedha za zisizo na thamani ya dhati na viwango vya riba vina mchango mkubwa katika hali ya kuyumba kwa uchumi wa mzunguko wa kimataifa. Zaidi ya hayo, kuyumba kwa sekta ya fedha na msukumo wa kudumu unaochochewa na deni la kuongeza Pato la Taifa hauzingatii mgawanyo wa mapato na utajiri miongoni mwa watu. Huku mfumko wa bei ukiwa juu kwa miaka 40, kupanda kwa gharama za maisha na chakula, kupungua kwa akiba na mishahara isiyolingana na mfumko wa bei, watu wa kawaida hawawezi kujikimu na tofauti katika mlimbikizo wa mali inaendelea kuongezeka. Takwimu zinaonyesha kuwa masuala haya ndiyo msingi wa Ubepari na sio tu ‘sera mbaya.’

Kwa hivyo, kama Waislamu tuna mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu wa kuutoa kwa ulimwengu kama suluhisho pekee kwa wanadamu. Mtazamo wa Uislamu juu ya tatizo la kiuchumi na masuluhisho yake umejengwa juu ya fahamu ya kipekee na hauko sawa na Ubepari. Kwa mfano, chini ya Uislamu, mfumo wa fedha unategemea kiwango cha mfumo wa madini mawili ya dhahabu na fedha. Dalili ya hili ni kwamba Uislamu umehusisha dhahabu na fedha na hukmu za Shari’ah zilizowekwa kama Zaka, fedha za damu (diyah), wizi, ubadilishanaji sarafu, nk. Mtume Muhammad (saw) anasema: «وَأَنَّ فِي النَّفْسِ المُؤْمِنَةِ مِاْئَةٍ مِنَ الإِبِلِ ، وَعَلَى أَهْلِ الْوَرِقِ أَلْفُ دِينَارٍ»na kwa nafsi iliyoamini (ikiuawa) ni ngamia mia moja, na kwa wenye dhahabu Dinari elfu moja (Ibn Qudamah, Al-Mughni)

Kiwango cha madini mawili ya dhahabu na fedha kina thamani halisi na hivyo huondoa uundaji wa mikopo, kutengeneza/kuchapisha sarafu kwa hali isiyoeleweka na huondoa mizunguko mikubwa ya mfumko wa bei. Usambazaji wa pesa sokoni unadhibitiwa na unahusishwa moja kwa moja na kiasi cha dhahabu na fedha kilicho katika hifadhi ya Bait ul-Mal (Hazina ya Dola). Mfumko wowote wa bei unaoweza kutokea utatokana na mipangilio ya usambazaji na mahitaji na sio kwa sababu ya sera za fedha, kama tunavyoona leo. Zaidi ya hayo, kwa kuwa thamani ya sarafu inahusishwa na dhahabu na fedha, hutoa kiwango cha ubadilishanaji kisichobadilika kati ya sarafu tofauti na kuzuia kushuka kwa ghafla kwa thamani ya sarafu. Kwa kweli, kiwango cha madini mawili huleta uthabiti wa kiuchumi, thamani halisi, na ukuaji endelevu bila kuongezeka kwa mzunguko panda shuka.

Muundo wa kiuchumi wa Kiislamu unazingatia ugavi wa mali badala ya uzalishaji tu. Mkazo juu ya uchumi halisi na masoko ya fedha, kama tunavyoona leo, itakuwa marufuku. Fedha (kuongeza mtaji) inacheza sehemu katika uchumi, bila shaka, lakini inafanywa kupitia ushirikiano wa biashara unaolenga kuzalisha faida na kugawanya hasara. Marufuku ya Riba huondoa sekta za sasa za kifedha ambazo zimejengwa juu ya deni na vyombo haribifu vya kifedha. Kwa kuongezea, kuramishwa kwa Riba kunasaidia kuondoa mrundiko wa mali. Zakat pamoja na marufuku ya kuhodhi na ukiritimba vyote vinachangia katika ugavi mpya wa mtaji na hivyo kuhimiza ukuaji wa uchumi. Uislamu umeweka sheria kwamba mali isiruhusiwe kuzunguka miongoni mwa matajiri pekee. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَا أَفَاءَ اللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Na mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao hamkuyakimbilia mbio kwa farasi wala ngamia. Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu.” [Al-Hashr: 6].

Hayo hapo juu ni mukhtasari tu wa mfumo wa uchumi wa Kiislamu ambao kwa sasa hautekelezwi kivitendo. Matunda ya kweli ya mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu hayawezi kupatikana mpaka mfumo kamili wa Uislamu yaani Khilafah usimamishwe. Muundo huu wa kiuchumi unafanya kazi sanjari na mifumo ya kijamii, kimahakama, na kisiasa ya Uislamu. Kutekeleza baadhi ya sera za kiuchumi za Kiislamu ndani ya mfumo wa sasa wa Ubepari ni jambo lisilo la kiakili na linashusha thamani mfumo wa Kiwahyi wa Mwenyezi Mungu (swt). Dini yetu inatekelezeka katika zama zote na Hukmu zake zilizoamriwa na Mwenyezi Mungu ni suluhisho kwa masuala yetu ya kiulimwengu.

Hizb ut Tahrir imejitolea juhudi zake kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Miongoni mwa nguvu zake ni kuelewa utaratibu wa sasa wa kiulimwengu na mfumo wake wa kiuchumi. Zaidi ya hayo, tunatoa mipango ya jinsi ya kuhama kutoka mfumo wa sasa wa uchumi hadi mfumo wa Kiislamu pamoja na katiba yake na muundo unaotawala. Fasihi yetu ya kina juu ya mambo haya inatoa ruwaza mapya kwa ulimwengu. Ruwaza mpya kwa Umma wetu na ulimwengu, unaoishi chini ya hukmu ya Mwenyezi Mungu سبحانه وتعالى, ukiongoza ulimwengu kwa amani, ustawi, na wokovu kesho Akherah. Ruwaza mpya inayotaka kuutoa ulimwengu kutoka katika giza la Ubepari na kuupeleka kwenye nuru ya Uislamu. Hivyo, tunauomba Ummah kuweka imani na hofu yake kwa Mwenyezi Mungu (swt) Pekee na kusubutu kufikiria mustakbali mpya.

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Al-A’raf: 96].

H. 12 Rajab 1444
M. : Ijumaa, 03 Februari 2023

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu