Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la Khilafah 2023

(Imetafsiriwa)

Chicago, Mei 13, 2023 - Hizb ut Tahrir / Amerika ilifanya Kongamano lake la kila mwaka la Khilafah kwa mafanikio. Hafla hii ni sehemu ya kampeni ya kimataifa ya kukumbuka kuondolewa kwa Khilafah mwaka 1924. Ni wito wa kimataifa kwa Waislamu ulimwenguni kote kusimama na kutimiza wajibu wa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt), kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume wetu (saw). Kongamano la mwaka huu-lenye kichwa " "Migogoro na Njia Panda... Udharura wa Uislamu Kuuokoa Ulimwengu"- lilijikita katika mada za familia, uchumi, na hali ya kisiasa ya jamii yetu iliyozama katika mgogoro na kusimama kwenye njia panda. Kongamano hili lilitoa ufahamu muhimu katika masuala ya sasa ya kijamii yanayotoa changamoto kwa familia ya Kiislamu kwenye migogoro ya kiuchumi na kisiasa inayofichua hali ya mambo ya Marekani. Kongamano hilo lilikutana na mvuto mkubwa na maoni chanya kutoka kwa mamia ya waliohudhuria na maelfu ya washiriki mtandaoni. Uungwaji mkono huu wa nguvu unaonyesha kujitolea kwa Ummah kwa Uislamu na hamu ya Ummah kuishi na kuongozwa na Uislamu katika changamoto zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa zilizo mbele yetu.

Kongamano hili lilianza kwa kusomwa Qur'an Tukufu, kisha kufuatiwa na hotuba ya kuvutia ya Ndugu Zaki Tahir, kutoa ufahamu wa kina wa changamoto zinazokabili jamii ya Kiislamu kutokana na kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa LGBTQ na ajenda ya ufeministi. Hotuba yake ilitoa mikakati ya kivitendo kusaidia familia za Kiislamu kuwalinda watoto wao, na kuwapa uwezo wa kupinga fahisha inayojaribu kuiangamiza familia ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema ndani ya Quran,

[يَا أَيُّهَا ٱلَّذِينَ آمَنُوا۟ قُوا۟ أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا]

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto” [At-Tahrim:6]. Alieleza jinsi kushikamana na Qur’an Tukufu na Sunnah kutaipa uwezo jamii wa kusimamisha Dini yao dhidi ya ufisadi huu.

Samer Abu Omar alifuata kwa kuzungumzia mgogoro wa kiuchumi unaoikumba Marekani na dunia hivi sasa. Akizungumzia kuongezeka kwa mwanya wa utajiri, kupanda kwa mfumko wa bei, na changamoto kwa msukosuko wa kiuchumi wa Marekani, aliangazia jinsi Uislamu unavyotoa masuluhisho yanayoweza kuhimili majanga mengi ya kiuchumi ambayo mara kwa mara yanausibu ubepari.

Dada Safia Rasheed, katika hotuba yake “Wanawake wa Kiislamu Simameni dhidi ya Ajenda ya Ufeministi,” iliangazia nguvu na utu wa wanawake wa Kiislamu uliojengwa juu ya msingi wa Uislamu. Aliwashajiisha kusimama kidete dhidi ya nguvu yoyote inayohujumu heshima ya wanawake wa Kiislamu. Alifichua jinsi ubepari unavyomnyonya mwanamke ili kunufaisha maslahi yao ya kifedha dhidi ya maslahi ya ustawi wa familia.

Katika hotuba yake "Himaya Inayoporomoka: Mgogoro wa Kisiasa wa Amerika," Ndugu Diwan Abu Ibrahim aliangazia jinsi Amerika inavyopambana na mgawanyiko wa kisiasa uliokithiri. Alizungumzia jinsi makosa ya sera ya kigeni ya Amerika yameongeza mzigo wa kifedha kwa deni la kitaifa na kuwezesha kuongezeka kwa ulimwengu wa nchi nyingi. Hotuba hii inaangazia jinsi Amerika inavyosimama katika njia panda muhimu, na kukabiliwa na kuanguka kwa utawala na kuhama kuelekea katika ulimwengu wa pande nyingi.

Kongamano lilihitimishwa kwa hotuba ya kufunga ya Haitham Ibn Thbait, ambaye alisisitiza haja ya jamii ya Kiislamu kujitia nguvu kwa imani yao kwa Mwenyezi Mungu (swt) katika nyakati hizi zenye changamoto. Kongamano hili litasaidia kuiwezesha jamii ya Kiislamu kwa elimu ya jinsi ya kukabiliana na majanga ya leo.

Hizb ut Tahrir (Chama cha Ukombozi) ni chama cha kisiasa cha Kiislamu cha kiulimwengu. Lengo letu ni kusimamisha Uislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu na kupeleka ujumbe wa Uislamu kwa wanadamu kupitia kusimamishwa tena kwa Khilafah. Nchini Marekani, tunaishajiisha jamii ya Kiislamu kutetea Uislamu na kufanya kazi nasi na kutuunga mkono katika kazi yetu ya kimataifa.

H. 27 Shawwal 1444
M. : Jumatano, 17 Mei 2023

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu