Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kisha Nini Kinachofuata, Enyi Waislamu? Je! Mnasubiri nini baada ya kushuhudia kile kilichotokea huko Gaza? Je! Sio wakati wa nyinyi kusonga na kuitikia amri ya Mola wenu Mlezi kwa kusimamisha Khilafah Rashida?
(Imetafsiriwa)

Siku chache tu zilizopita, kumbukumbu ya kuvunjwa Dola ya Kiislamu baada ya miaka 103, katika mwezi wa Rajab Tukufu, sanjari na maadhimisho ya Al-Isra Wal Mi'raaj mwezi huo huo. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ]

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Surat Al-Isra:1].

Mwenyezi Mungu (swt) amenasibisha kati ya Masjid Al-Haram na Masjid Al-Aqsa katika uhusiano wa kiitikadi, wa milele katika Quran yake hadi Siku ya Kiyama. Walakini, inaomboleza na inaita mchana na usiku kwa ajili ya ukombozi wake kutoka kwa uvamizi wa umbile la Kiyahudi, mbele ya macho na masikio ya watawala wa Ruwaibidha (watepetevu) wa makasri, lakini hakuna wa kujibu.

Na maadhimisho haya yanapita, na mito ya damu inayotiririka kutoka kwa watoto wa Waislamu huko Gaza, na udhalimu na ukatili wa umbile ovu la Kiyahudi umeenea kwa wanadamu, mawe, na miti kwa msaada wa ukoloni wa Marekani na Ulaya na usaliti wa watawala wa Kiarabu na nchi za Waislamu. Hakuna mtu muongofu katika majeshi ya Waislamu anayeongoza majeshi ya Waislamu kuunusuru Uislamu na Waislamu kwa kuliangamiza umbile la Kiyahudi huko Palestina na kuirudisha yote katika ardhi za Uislamu.

Kwa zaidi ya karne moja, Ummah wa Kiislamu umekuwa ukikabiliwa na kipindi kibaya zaidi katika historia. Kuvunjwa kwa Khilafah kulikuwa matokeo ya juhudi chafu, miongo kadhaa ya kupanga njama, na khiyana kutoka kwa dola za kikoloni za Magharibi katika mapambano yao dhidi ya hadhara ya Kiislamu hadi leo. Kuvunjwa kwa Khilafah hakukuwa matokeo ya adha ya kisiasa inayofanywa na dola za kikoloni za Magharibi, lakini badala yake matokeo ya juhudi, njama, na khiyana kutoka kwa dola hizo. Ilikuwa ni jambo la kimaumbile kwa dola hizi za kikoloni za Kikafiri kuhifadhi mafanikio yao kwa kujitahidi kuzuia kurudi kwa Khilafah, ambayo walikuwa wameshaivunja.

Uhalisia ambao Ummah inakabiliwa nao leo, haswa baada ya Vita vya Gaza, unaonyesha kwamba Ummah wa Kiislamu sasa unazidi kuitazamia Khilafah, umoja wa Kiislamu, na utabikishaji wa Sharia katika nyanja zote za maisha. Utambuzi na kushikamana kwa Ummah kwa Uislamu leo ni makubwa zaidi kuliko hapo awali, na Ummah sasa amejiandaa kikamilifu kutoa muhanga mmoja baada ya mwingine kwa sababu ya Dini yake. Hili linasukumwa na fahamu zilizowekwa za aqeedah (itikadi) ndani yake na utambuzi wake wa kihisia kwamba hakuna wokovu kwake katika hali yake ya sasa isipokuwa kupitia kurudi Uislamu kupitia kusimamisha dola yake.

Hapa, ni muhimu kufafanua ukweli ufuatao:

1- Kwamba sisi ni Waislamu walioumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Uislamu umetuonyesha jinsi ya kuunda dola yenye nguvu, ikifafanua malengo yake ya juu ambayo yanastahiki heshima ya binadamu, ambayo inaweza kupatikana tu na dola inayotabikisha amri za Mola wa Walimwengu.

2- Hakika, Uislamu ndio dini ambayo Mwenyezi Mungu ameichagua kwa wanadamu, kwa hivyo hairuhusiwi kukubali itikadi zengine au mifumo yoyote iliyotungwa na mwanadamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَنْ يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِيناً فَلَنْ يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ]

Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.” [Surat Aal-i-Imran:85].

3- Khilafah ndio wajibu mkubwa ambayo kwayo faradhi kuu tatu zinapatikana: kusimamisha Dini, kuwaunganisha Waislamu, na kueneza Uislamu kote ulimwenguni. Ummah hauwezi kutimiza Uislamu na kuueneza isipokuwa wanapokusanyika chini ya mtu mmoja anayesimamisha Dini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ، لَقِيَ اللهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا حُجَّةَ لَهُ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»

“Yeyote mwenye kuondoa mkono wake kutoka katika utiifu (kwa Amiri) atakutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama akiwa hana hoja na yeye; na yeyote anayekufa na hana katika shingo yake ahadi ya utiifu (Bay’ah) amekufa kifo cha Kijahiliya.”

4- Dola za Kikafiri za Magharibi ni maadui wa Uislamu na watu wake. Uhusiano nazo lazima uwe ule wa kivita; Hazipaswi kuchukuliwa kama marafiki au washirika, na hazipaswi kuruhusiwa kuwa na uwepo au kambi za kijeshi nchini. Dola hizi, zikiongozwa na Marekani na Uingereza, hazisazi juhudi yoyote katika kuwauwa Waislamu, kupora utajiri wao, na kupanda mbegu ya mgawanyiko kati yao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَن يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً] 

wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surat An-Nisa:141].

5- Watawala wa nchi za Kiarabu na ardhi za Waislamu ni vibaraka wa Kafiri mkoloni na wafuasi wake. Ni maadui wa Ummah na Dini yake, na ndio kichwa cha Kafiri katika nchi za Waislamu. Hawasazi juhudi yoyote kuupiga vita Uislamu, kueneza ufisadi na uzinzi, kuuweka mateka Ummah wa maadui wa Uislamu, na kupuuza nusra yao kwa watu wa Gaza, ambayo iko dhahiri.

6- Asasi za kimataifa katika aina zao zote, kama vile Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama, Mahakama ya Haki ya Kimataifa, UNRWA, na nyenginezo, na pia taasisi za kikanda kama vile Ligi ya Kiarabu, Baraza la Ushirikiano la Ghuba, na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu, ni zana za dola za wakoloni wa Magharibi kudumisha utawala wao na kutekeleza mipango yao ya kupambana na Uislamu na kudumisha kutengana kwa Ummah wa Uislam na kunyimwa rasilimali zake.

7- Ukombozi wa Ummah kutokana na ukoloni unaweza kupatikana tu na vikosi halisi vya Ummah kusonga kuwapindua watawala madhalimu na kung’oa ushawishi wa ukoloni kutoka mizizi yake. Hili linahitaji kuunganishwa kwa vikosi vya Ummah ili majeshi ya Ummah yalingane na Uislamu na kujiunga na safu za Ummah, kutangaza kujitega kwao kutoka kwa serikali hizi za vibaraka, na kuharakisha kuzipindua na kuuacha huru Ummah kutokana na maovu yao.

Vita vya Gaza bila shaka vimethibitisha kwamba Ummah wa Kiislamu ni Ummah wa Jihad na Shahada, kupitia uthabiti wa watu wake na shujaa wake Mujadina ambaye alitikisa umbile oga la wanyakuzi wa Kiyahudi, licha ya idadi yao ndogo, rasilimali haba, na njama ya watawala. Kwa hivyo, tunawathibitishia Waislamu na wale ambao wana nguvu kati yao kwamba gharafa ya kafara watakayotoa kwa ajili ya kusimamisha Khilafah ni chini sana kuliko ile wanayolipa hivi sasa kwa sababu ya kukosekana Khilafah yao.

Enyi Waislamu, Watu wa Nguvu na Azma nchini Jordan:

Kadhia ya kufanya kazi kwa ajili ya kurudi kwa Khilafah ni kadhia nyeti ya Ummah, ambayo kwayo mtu lazima awe tayari kuchukua maamuzi ya uhai na kifo. Jaribio la dhati na kubwa, pamoja na wafanyikazi wanaofanya kazi mchana na usiku, linahitajika kuleta kurudi kwake kama nguvu kubwa ambayo huhifadhi nchi, watu wake, na utajiri wao. Kazi ya kivitendo kuelekea usimamishaji wake inahitajika kwamba watu wa nguvu na azma warudishe mamlaka kwa Waislamu na kuondoa mtu yeyote anayesimama kwa njia yao, iwe ni watawala, duara za ndani za ufisadi, au wasomi wenye madhara, na nyuma yao, msukumo wa ukoloni wa Magharibi. Tunaona kupatikana kwake kuwa karibu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu; Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt), na bishara njema ya mjumbe wake (saw). Ummah mzima unatarajia siku ambayo dola yao itaregeshwa, kuwaokoa watu wa Palestina, Gaza, Al-Aqsa, na Waislamu wote wanaokandamizwa duniani.

H. 6 Sha'aban 1445
M. : Jumanne, 16 Aprili 2024

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Jordan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu