Jumamosi, 19 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kumbukumbu ya Miaka 97 ya Kuvunjwa kwa Khilafah 
(Imetafsiriwa)

Ndani ya mwezi wa Rajab, Waislamu bado wanaishi miaka 97 pasina dola. Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Hadith iliyosimuliwa na Bukhari kutoka kwa Abu Hurayrah alisema:

«وَإِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Kamanda (wa Waislamu) ni ngao kwao. Wanapigana na wanajilinda nyuma yake (kutokana na madhalimu na wakandamizaji).”

Tangu Waislamu wapoteze Khalifah wao, mataifa yanawashambulia kutoka kila pembe; na kuwavamia mfano wa walaji wanavyokiendea chakula. Maadui wameiondosha Shari’ah yetu na na kutufanya kuhisi machungu baada ya kuigawanya dola yetu moja na kuwa vijidola dhaifu, wanapora utajiri wetu na kumwaga damu zetu. Wamekiuka hadhi ya kibla cha kwanza kati ya vibla viwli, msikiti wa tatu kati ya misikiti Miwili Mitukufu na Masra ya Nabii ya Mwenyezi Mungu (saw)

Hakuna Muislamu aliyeokolewa kutokana na dhuluma na mauaji. Wanaendeleza mateso na mauaji kwa Waislamu wote wanaoishi ndani ya Syria, Iraq, Turkistan Mashariki, Burma na Afrika ya Kati…

Wakoloni makafiri wamechukua hatua mpya katika vita vyao dhidi ya Uislamu na Waislamu ndani ya nchi za Asia ya Kati kwa kubuni sintofahamu ndani ya jirani Afghanistan. Wameanza kuzidisha vita dhidi ya wote wale ambao wanabebea Da’wah ya kimfumo ikipelekea kwa utekelezaji wa “Uislamu laini.”

Katika vita hivi vinavyoendelea, udhalimu wa utawala haukuwasaza wanawake madhaifu. Wamekuwa hawahurumiwi katika kukamatwa, kudhalilishwa na kutishiwa na kubakwa na kuuwawa kwa wanawake Waislamu na kuwatupa gerezani licha ya kuwa ni kina mama walio na watoto. Watawala wa Asia ya Kati wamezindua kampeni pana dhidi ya vijana wanaofuga ndevu na dhidi ya wanawake wanaovaa Khimar (kitambaa cha kichwa), na kupelekea kuwadhibiti vijana kuhudhuria msikitini kwa umri fulani na kuwapiga marufuku wanafunzi wasichana kutovaa Khimar. Kundi hili la watawala vikaragosi hawakutekeleza kampeni hii pekee bali pia wamewazuia wazazi kutowapa watoto wao majina ya Kiislamu!

Kudhalilika na kutaabika kwa Waislamu hakukuishilia hapo tu bali ni kama mayatima katika meza za madhalimu. Nchi zao zimevunjiliwa mbali, heshima zao kudhalilishwa, hadhi zao kukiukwa, utajiri wao kuporwa, matukufu yao kunajisiwa, mipaka yao kubuniwa, maisha yao kuwekwa mbali na sheria za Mwenyezi Mungu. Na watawala wao wamekuwa watiifu kwa Magharibi, wakiwa na hamu ya kulinda maslahi ya ukoloni wa mabwana zao Makafiri. Hivyo basi, maneno ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) ni ya kweli kwamba tumekuwa kama povu, kama povu katika mto, licha ya kwamba idadi yetu ni kubwa! 

Licha ya uvamizi wa ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi mkoloni na kudhibiti uvamizi wake kupitia thaqafa yake ndani ya karne ya 19 Miladi na kuishambulia kwa miongo kadhaa kwa kuzipotosha fikra za Uislamu.

Licha ya yote haya, Mwenyezi Mungu ameupa Ummah wa Kiislamu sauti za kunyanyuka zinazodai Khilafah ya Kiislamu na nchi za Waislamu zinashuhudia kazi ya Shabab wa Hizb ut Tahrir kuanzia Indonesia hadi Malaysia, Pakistan, Uturuki, Syria, Lebanon, Palestina, Asia ya Kati…

Lakini, hakuna Uislamu pasina dola huru, ambayo inatawala kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu ameleta wahyi na kuharamisha kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu ameharamisha na kuhalalisha kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu ameruhusu. Inawasimamia raia wake, Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwa mujibu wa Shari’ah na kudhamini maisha yao kwa uadilifu, usalama na ulinzi. Na wanadamu watafurahia kivuli cha nuru ya Uislamu na muongozo wake na watakombolewa kutokana na tawala dhalimu zilizo lazimishwa juu yao kwa ukoloni baada ya kuumwa na moto wake. Ummah wa Kiislamu utarudi kuwa Ummah bora uliowahi kutolewa kwa wanadamu ukibeba ujumbe wa Wahyi, utafutilia mbali vumbi la ufisadi wa ustaarabu wa kimada wa Kimagharibi unaofisidi na kuivunjilia mbali mwisho wake na kuwakomboa wanadamu kutoka katika najisi zake na kuwazunguka na uadilifu na huruma ya Uislamu:

Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمْ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لاَ يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]

Na Mtume (saw) alisema:

«إِنَّ اللهَ زَوَى لِي الأَرْضَ فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا، وَإِنَّ مُلْكَ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا»

“Mwenyezi Mungu alizivuta pembe za dunia kwa ajili yangu. Na nimezitizama mashariki na magharibi yake. Na nguvu za Ummah wangu zitafika katika pembe zote ambazo zimeletwa karibu nami.”

 

H. 22 Rajab 1439
M. : Jumatatu, 09 Aprili 2018

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu