Alhamisi, 14 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wanachoma Quran nchini Denmark na Kufunga Misikiti na Shule za Kidini nchini Kyrgyzstan
(Imetafsiriwa)

Mnamo Julai 21, wanachama wa kikundi cha "Wazalendo wa Denmark" walichoma nakala ya Quran ya Noble mbele ya ubalozi wa Iraq jijini Copenhagen. Walidai kwamba kitendo hiki cha kufedhehesha kilikuwa ni majibu ya kuchomwa kwa ubalozi wa Sweden nchini Iraq.

Tunakukumbusheni kwamba mnamo Julai 19, polisi wa Sweden waliruhusu kuchomwa kwa Quran mbele ya ubalozi wa Iraq jijini Stockholm, na mmoja wa washiriki aliikanyaga Quran hiyo chini ya miguu yake. Matokeo yake, mnamo Julai 20, Iraq ilivamia ubalozi wa Sweden jijini Baghdad na kuuwasha moto. Inafaa kukumbuka kuwa wale waliopanga kitendo hicho nchini Sweden hata walichoma moto na kuichafua Quran siku ya Idd al-Adha. Kwa kuwa viongozi wa Waislamu na mashirika ya Kiislamu wameshindwa kusonga zaidi ya kulaani kwao tasa kwa kawaida kwa matukio kama haya, maadui wa dini hii wanaendelea na vitendo vyao viovu bila ya kizuizi.

Kwa mfano, badala ya kutumia fursa ya kupinga uanachama wa NATO wa Sweden, Uturuki, chini ya uongozi wa Erdogan, iliruhusu hili kutokea. Ama kwa serikali ya Iraq, wametishia kuwakamata watu waliochoma moto Ubalozi wa Sweden!

Na sasa, serikali ya Kyrgyzstan inasimama kati ya wale waliochoma Quran na imekuwa ikifunga misikiti na shule ambazo Quran inafundishwa. Wanajaribu kuhalalisha hili kwa kunukuu kanuni za afya. Kwa mfano, shule mbili katika kijiji cha "Suzuk" zilifungwa mwaka huu kwa kisingizio cha kukosa vibali sahihi. Kwa kuongezea, misikiti 60 katika mji wa Jalal-Abad ilifungwa kwa sababu ya kukosa vibali, na mengine iliarifiwa na Kamati ya Usalama ya Kitaifa ya Kyrgyzstan. Msikiti wa "Sarkhsi" katika mji wa Karasu pia ulifungwa, ukidaiwa kukosa kufuata kanuni za afya, na Waislamu walizuiliwa kutekeleza swala za Ijumaa humo.

Hasa wakati wa likizo ya msimu wa joto, wakati maelfu ya wazazi wanasimama sambamba kupeleka watoto wao misikitini na shuleni, na ambapo maeneo ya ibada na elimu yamejaa, ikifichua haja ya misikiti zaidi, misikiti yetu na shule zetu zinabaki kulengwa na serikali. Kusudi lililo nyuma ya hatua hii ya serikali sio chochote bali ni kuwasaidia wabeberu makafiri katika vita vyao dhidi ya dini! Je! Tueleweje, kwa mfano, uwepo wao miongoni mwa watu wakati wa swala ya Idd, wakati kwa upande mwingine, wanafunga Nyumba za Mwenyezi Mungu? Hili si lolote ila ni unafiki. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْماً غَضِبَ اللهُ عَلَيْهِمْ مَا هُمْ مِنْكُمْ وَلاَ مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ]

“Huwaoni wale walio fanya urafiki na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uwongo, na hali kuwa wanajua.” [ Al-Mujadila:14]

Ndio, leo hali ya Waislamu imefikia hali kama hiyo ya kusikitisha. Watawala wa sasa wa nchi zaidi ya 60 za Kiislamu wameshindwa kulingana na hata kucha za khalifa Abdul Hamid II. Alipinga utekelezwaji wa mchezo wa kuigiza wa Voltaire wa "Ushabiki Sugu" ambao ulimtukana Mtume (saw) nchini Ufaransa na Uingereza. Khalifa Abdul Hamid, ambaye alikuwa alijua yaliyomo kwenye mchezo huo, aliionya serikali ya Ufaransa kwamba endapo mchezo huo utafanywa, matokeo yake yangekuwa mabaya. Ufaransa mara moja ilisimamisha uchezaji mchezo huo. Baadaye, mchezo huo ulikwenda Uingereza kwa uchezwaji. Pindi onyo kutoka kwa Khalifa lilipofika Uingereza, serikali ya Uingereza ilijibu, "Tikiti zimeshauzwa, na kuuzuia ingekiuka uhuru wa raia wetu." Katika hatua hiyo, Sultan Abdul Hamid II alitoa agizo lifuatalo: "Hii ndio amri yangu kwa umma mzima wa Kiislamu! Uingereza inataka kumdhalilisha Mtume (saw), na kwa hivyo ninatangaza Jihad dhidi yake..." Pindi Waingereza waliposikia hivyo, walisahau uhuru wao wa maoni na mara moja walibatilisha uchezwaji wa mchezo huo.

Na kwa hivyo, sababu ya kudhalilishwa kwa Waislamu leo iko katika ukweli kwamba watawala wa nchi za Kiislamu hawajibu ipasavyo uhalifu wa makafiri. Kiuhalisia, kupambana na vitendo vyao viovu sio kukashifu na kulaaniwa tu, lakini kwa kuhamasisha majeshi na kuyataka mataifa mengine kufanya vivyo hivyo. Waislamu wengine wote lazima pia waonyeshe kutoridhika kwao na vitendo hivi vya makafiri, kushutumu khiyana ya watawala, na kujaribu kuishawishi rai jumla katika nchi zao wenyewe na ulimwenguni kote.

Ewe Mwenyezi Mungu, waweka mbali Waislamu na uvivu! Turuzuku hivi karibuni kuregeshwa kwa Khilafah Rashida ambayo hairuhusu kudhalilishwa kwa maadili ya Kiislamu!

H. 7 Muharram 1445
M. : Jumanne, 25 Julai 2023

Hizb-ut-Tahrir
Kyrgyzstan

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Kumbukumbu ya Miaka 97 ya Kuvunjwa kwa Khilafah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu