Jumamosi, 14 Muharram 1446 | 2024/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tukio la Bek-Abad: Mateso na Mashtaka ya Uongo
(Imetafsiriwa)

Huduma ya Usalama wa Taifa ya Kyrgyz iliwakamata wasichana wawili wenye umri wa miaka 16 na 19 katika kijiji cha Bek-Abad katika eneo la Suzak, na wanatuhumiwa kubadilisha bendera ya dola katika maeneo kadhaa. Mbali na ukaguzi huo uliofanyika mnamo Mei 31 na Juni 4, uliopelekea dada 4 wa Kiislamu kuwekwa chini ya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo binafsi, mama mwenye umri wa miaka 45 wa mmoja wa dada hao aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo aliendelea kuzuiliwa ili asimwache bintiye yake peke yake mikononi mwa madhalimu hao. Aidha, mjomba wa dada huyo mwenye umri wa miaka 29 alipigwa na kuteswa kwa nguvu za umeme. Kisha walionyesha video ya mjomba akiteswa kwa dada huyo na kutishia kumfanyia vivyo hivyo. Kwa sababu ya uoga na mshtuko aliokuwa nao dada huyo, alilazimika kukiri kosa hilo na kutekeleza kile ambacho vyombo vya usalama vilimtaka akiri. Kwa mujibu wa mashahidi walivyosema, washtakiwa hao waliteswa, na waliona jinsi wafanyikazi wa mashirika hayo walivyotumia nguvu kwao.

Siku kadhaa kabla, wafanyikazi wa Huduma ya Usalama wa Taifa ya Kyrgyz katika kijiji hicho waliwakamata wanachama wa Hizb ut Tahrir ambao waliobeba Da’wah kwa mashtaka ya uongo. Mamlaka rasmi wakati huo zilijaribu kulihusisha tukio hilo na Hizb ut Tahrir kwa kubadilisha habari. Hasa kwa vile maafisa wa usalama walikuwa wamefunga kamera katika maeneo ya hafla siku mbili kabla ili kutekeleza vitendo vyao vya uchokozi.

Kupitia haya yote, inaweza kuhitimishwa kuwa watawala wa nchi hii waliamua kuzidisha vita dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa vitendo vya uchokozi. Hizb ut Tahrir, Hizb ya kisiasa, inafichua ufisadi wa watawala na usimamizi wao mbaya wa watu. Kwa hiyo, unawakuta wanataka kuufanya utawala huo kuwa wa kidikteta, wakiwatupia tuhuma za uongo wanachama wa Hizb na kuongeza mateso. La kusikitisha, madhalimu hawakuwahurumia dada zetu Waislamu; waliwafanya wahanga wa matendo yao ya uchokozi.

Enyi watawala, je mnatumaini, kwa kuwaweka kina dada hao gerezani, kuhalalisha kushindwa kwenu kuwatawala watu? Je, ujasiri wenu unatosha tu kuuonyesha dhidi ya kina dada dhaifu? Je, watawala wa nchi hii wanaojichukulia kuwa ni Waislamu na kuswali mbele ya watu siku za sikukuu wanapaswa kushambulia heshima ya Waislamu?

Hamtafanikiwa. Hii ni kwa sababu jamii ya Kyrgyz inageukia kwenye Dini yake zaidi na zaidi kila siku na inajifunza Uislamu kama mfumo. Watu wa Kyrgyz wanaweza kutofautisha kati ya ukweli na uongo na hawatafuata matendo ya kuchukiza ya serikali.

Hizb ut Tahrir kamwe haijawahi kusitisha kazi yake ya kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu, licha mateso ya madhalimu. Historia ya maelfu ya ndugu zetu waliopata ulemavu kwa sababu ya kuteswa kikatili katika magereza ya mtawala dhalimu Karimov inashuhudia hili.

Watawala lazima watambue kwamba serikali nyingi zimejaribu kuitesa Hizb ut Tahrir lakini, shukrani zote kwa Mwenyezi Mungu, zilishindwa. Hivyo basi, ukamataji huo haitakomesha wanachama wa Hizb ut Tahrir, bali kinyume chake, utawatia nguvu katika njia ya kufikia malengo yao. Tunaamini kwa dhati maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) «لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي عَلَى الدِّينِ ظَاهِرِينَ، لِعَدُوِّهِمْ قَاهِرِينَ، لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَالَفَهُمْ إِلَّا مَا أَصَابَهُمْ مِنْ لَأْوَاءَ حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ كَذَلِكَ» “Kundi katika Ummah wangu hawataacha kuidhihirisha Dini, dhidi ya adui yao, hawatawadhuru wanaowatelekeza. Watasalia katika hali hiyo mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu.”

Kwa hiyo, sera ya ukandamizaji na vitisho haiwezi kuvunja dhamira na utashi wa wanachama wa Hizb ut Tahrir kufanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Ama kwa madhalimu hawataweza kuuzima moto wa nyoyo zao. Hili liko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur 24:55].

H. 7 Dhu al-Hijjah 1445
M. : Alhamisi, 13 Juni 2024

Hizb-ut-Tahrir
Kyrgyzstan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu